Watu
wawili akiwemo mlinzi wa nyumba moja mkoani Tanga, wamehukumumiwa kifungo cha
miaka 20 gerezani kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kupakua na
kuhifadhi meno ya tembo 114 yenye thamani ya sh. milioni 44,044 kinyume cha
sheria, anaripoti Mashaka Mhando, Tanga.
Washtakiwa hao ni Bw. Joseph Mwarabu na Bw. Richard Abdallah, ambapo
hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga,
Mairasaanane Kashonde.
Hakimu Kashonde alisema, washtakiwa walitiwa hatiani chini ya Sheria ya
Uhifadhi ya Wanyamapori kifungu cha 86 (i), (ii) C na Kifungu 14 D, cha sheria
ya uhujumu uchumi sura 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma hukumu hiyo, alisema washtakiwa hao walishiriki kushusha meno
hayo kutoka kwenye gari la jeshi na kuyahifadhi kwenye nyumba ambayo haikuwa mali yao.
“Mah a k ama ime s h in dwa kumhusisha mmiliki wa nyumba hiyo, Bw. Michael
Kijangwa ambaye wakati huo hakuwepo, hivyo mshtakiwa wa kwanza na pili mnatiwa
hatiani kwa kuhusika kikamilifu katika tukio hili,” alisema.
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Serikali, Veridiana Mlenza akiwa na
mwenzake Sabrina Joshi, waliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa washtakiwa
kwani matukio ya watu kukutwa na meno hayo yamekuwa yakiongezeka.
“Ni vyema mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine
kutokana na ongezeko la vitendo hivi,” walisema.
Washtakiwa hao walipotakiwa kujitetea, kila mmoja aliiomba mahakama
isiwape adhabu kali kwani wana familia ambazo zinawategemea.
Hakimu Kashonde alisema kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori, inatoa
fursa kwa hakimu kutoza faini mara kumi ya thamani ya nyara inayokamatwa kwa
mshtakiwa lakini aliwahukumu kifungo hicho iwe fundisho kwa wengine.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari Mosi 2010, katika Mtaa wa
Chumbageni, kwenye nyumba inayomilikiwa na Bw. Kijangwa na walikutwa wakiwa na
vipande hivyo.
Shtaka la pili ambalo lilikuwa likiwakabili washtakiwa hao, inadaiwa
Desemba 31, 2009, huko Chumbageni, walishindwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa
nyara za serikali kwenye nyumba ambayo walikuwa wakifanya kazi.
Hata hivyo, washtakiwa hao walikana na kudai meno hayo hayakuwa ya kwao
bali ya bosi wao Bw. Kijangwa ambaye kwa wakati huo alikuwa Lushoto na familia
yake ambako walikwenda kula sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Inadaiwa meno hayo
yalipelekwa katika nyumba hiyo iliyopo jirani na Hospitali ya Tumaini, eneo la
Chumbageni na gari la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na maofisa
wawili Desemba 31, 2009.
SI AJABU WALIOFUNGWA HAWAMILIKI CHOCHOTE NI SAWA NA WANABEBA MADAWA YA KULEVYA NI MAKONTEINA TU
ReplyDeletei like this blog and article
ReplyDeleteBEST AVAILABLE WAY TO FINANCIAL FREEDOM {upstoxfunding@yahoo.com}
ReplyDeleteAre you looking for financial freedom? Are you in debt, you need a loan to start a new business? Or you collapse financially, do you need a loan to buy a car or a house? Have you ever been rejected by your bank in ever finance? You want to improve your financial? You need a loan to pay off your bills pay off? No more looking, we welcome you for an opportunity to get all types of loans at a very affordable 3% interest rate for others. For information, contact us now by email at: {upstoxfunding@yahoo.com}
Do you have a bad credit? Do you need money to pay bills? Is it necessary to start a new business? Do you have an unfinished project due to poor funding? Do you need money to invest in any specialty that will benefit you? And you do not know what to do. We offer the following loans;both Personal loans [secure and unsecured], Business loans [secure and unsecured] ,combination loans ,Student loans,Consolidation loans and so many others.
Company name: UPSTOX FUNDING
Company Email: upstoxfunding@yahoo.com
Text/Call :+1(302) 273-5794.