14 June 2012
POAC yamtaka Mkulu aombe radhi bungeni
Na Peter Mwenda
MBUNGE wa Mwibara, mkoani Mara, Bw. Kangi Lugola, amemtaka aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Mustapha Mkulo, alithibitishie Bunge juu tuhuma alizozielekeza kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), na kudai imehongwa na Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC).
Bw. Lugola aliyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma jana baada ya kuomba mwongozo wa spika na kudai kuwa, katika kikao cha Bunge lililopita, alimtaka Bw. Mkulo athibitishe kauli aliyowahi kuitoa bungeni akidai kamati hiyo ilihongwa sh. milioni 60 na CHC ili kupindisha ukweli lakini hakuwepo bungeni.
Alisema katika tuhuma hizo, Bw. Mkulo alimtaja Mwenyekiti wa POAC, Bw. Zitto Kabwe kuwa ameweka rehani ubunge wake kwa ajili ya rushwa hivyo kuishuka hadhi kamati hiyo.
“Kwa vile Bw. Mkulo yupo hapa, naomba Naibu Spika atoe mwongozo ili afute kauli yake ili kuweka kumbukumbu sawa au alete ushahidi bungeni,” alisema.
Katika majibu yake, Naibu Spika Bw. Job Ndugai alisema amepokea jambo hilo na atalitolea mwongozo kwa wakati muafaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Angekuwa mbunge wa upinzani angetakiwa asimame pale pale na kujieleza lakini sababu ni samaki papa basi inabidi amuite pembeni halafu tutasikia hilo limemalizwa nje ya vikao.
ReplyDelete