14 June 2012

Mpinga akiri 'uchakachuaji' leseni


Na Anneth Kagenda

KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,  Mohamed Mpinga, amekiri kuwepo vitendo vya uchakachuaji leseni ambavyo ni moja ya sababu inayochangia ongezeko la ajali nchini.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Kamanda Mpinga alisema kuwa madereva wengi wanadanganya kuwa wamesea udereva katika vyuo mbalimbali kikiwemo VETA.


“Kuna matukio ya kufoji vyeti ambayo yamekuwa yakijitokeza katika vyuo mbalimbali kikiwamo VETA, utakuta mtu anafanya udanganyifu na kudai amesema katika chuo hiki wakati katika orodha ya waliohitimu hayumo.

“Tumekuwa tukikemea vitendo hivi na kuvitaka vyuo husika kutuletea orodha ya waliomaliza vyuoni baada ya wanafunzi kumaliza masomo yao ila vitendo hivi vitakoma,” alisema.

Alisema wale wananaondelea na tabia hiyo wakikamatwa sheria itachukua mkondo wake ambapo baadhi ya watu waliozungumza na Majira wakiwamo wamiliki wa vyuo vya udereva, walidai vitendo hivyo bado vinaendelea kwa madereva wengi kupata vyeti bila kuvisomea vyuoni.

1 comment:

  1. KAMA HAKUNA MBONA MARUBANI WAMEAMBIWA HAWANA UTAALAMU JE HAWAKUCHAKACHUA VYETI???

    ReplyDelete