26 June 2012

Timu ya Kivule veteran yapata vifaa


Na Peter Mwenda

MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa ametoa mipira na jezi kwa ajili ya timu ya veteran ya Kata ya Kivule, wilaya ya Ilala.

Akikabidhi vifaa hivyo mwakilishi wa mbunge huyo Ali Mwaiposa alisema amefurahi kuona wachezaji wa zamani wanarudi uwanjani kuweka afya zao vizuri.


Ali ambaye ni mume wa mbunge huyo alisema mazoezi yanasaidia kuweka miili katika hali ya kutonyemelewa na maradhi.

Katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Kivule Veteran, Jesse John alisema timu hiyo imeanza mazoezi chini ya kocha Quresh Ufunguo ambaye aliwahi kuichezea Simba akisaidiana na Fundi Kipande.

Alisema timu hiyo itakuwa inafanya mazoezi kila Jumamosi asubuhi na Jumapili katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Misitu, Kivule.

No comments:

Post a Comment