14 June 2012
Madiwani Namtumbo ibueni miradi ya maendeleo -M/kiti
Na Kassian Nyandindi, Namtumbo
MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wametakiwa kuibua miradi ya kimaendeleo ambayo itakuwa na tija kwa wananchi.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Bw. Steven Nana, aliyasema hayo juzi mjini Namtumbo, mkoani hapa wakati akifafanua mambo mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Alisema hivi sasa halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hivyo ni vyema madiwani wawe na upeo mpana wa kutafuta njia mbadala za kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Bw. Nana aliongeza kuwa, madiwani wana nafasi kubwa katika hilo kama watashirikiana na wananchi kwenye kata zao badala ya kufanya maamuzi mbalimbali bila kuwashirikisha.
Alisema halmashauri nyingi nchini zinashindwa kujiendesha kwa sababu ya malumbano yasiyo ya lazima miongoni mwao hasa kwa watendaji hivyo kukwamisha maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment