29 June 2012

Ulimboka sasa aitesa Serikali *Yashindwa kutoa tamko la waliogoma *Madaktati ICU wapigania maisha yake



Na Waandishi Wetu, Dodoma, Dar

SERIKALI imekiri kuchanganywa na tukio la kutekwa na kujeruhiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven Ulimboka, ambapo Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, jana alishindwa kutoa tamko la Serikali kuhusu madaktari waliogoma bungeni mjini Dodoma, kama alivyoahidi juzi.

Bw. Pinda aliahidi kutoa tamko hilo wakati akijubu swali la papo kwa hapo kutokana na swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe.

Pamoja na mambo mengine, Bw. Mbowe alitaka kujua Bw. Pinda anaizungumziaje kauli ya “litalo na liwe” na Serikali inachukua hatua gani za ziada kumaliza tatizo mgomo wa madaktari.

Juzi Bw. Pinda alilieleza bunge kuwa, Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kumaliza mgomo wa madaktari bila mafanikio na kuahidi kuwa kesho yake (jana), angetoa tamko la Serikali.


“Mheshimiwa Spika, nikiri kutamka liwalo na liwe lakini inawezekana neno hili limepewa tafsili  nyingi, kilichokuwa kikinusumbua, jambo hili lipo mbele ya Mahakama Kuu, kama nitatoa kauli ni dhahiri nitaonekana mtovu wa taratibu zetu kikatiba.

“Ndioa maana nikafika mahali nikasema, katika mazingira yaliyopo nikieleza kinachoendelea na tunataka kufanya nini, viongozi wa muhimili mwingine watanilaumu, alisema Bw. Pinda.

Bw. Pinda alilazimika kutoa ufafanuzi zaidi wa kauli ya “liwalo na liwe”, ambayo ilizua mjadala juzi bungeni huku Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee, akidai huenda ikawa na uhusiano na tukio la kutekwa Dkt. Ulimboka.

“Jana (juzi), nilimsikia dada yangu Mdee akiitafsili kauli hii vingine nikasema ni habari mbaya, wakati nikizungumze vile sikuwa nafahamu lolote bali nilichokisema, kilihusiana na mgomo wa madaktari na kuahidi kutoa kauli bungeni.

“Nilishauriana na vyombo vingine vya muhimili, ikaonekana
bado hatuwezi kutoa tamko wakati jambo hili limeahirishwa hadi mwezi ujao na mimi nikakubali ushauri huo,” alisema Bw. Pinda.

Bw. Pinda akizungumzia tukio la kutekwa Dkt. Ulimboka, alisema limemsikitisha na anamtakia kheri apone haraka kwani taratibu za kumaliza mgogoro uliopo ulikuwa ukienda vizuri.

“Kwanza nioneshe masikitiko yangu juu ya jambo hili na mimi namtakia kila la kheri apone haraka, ni bahati mbaya tu kwa sababu mchakato ulikuwa unaenda vizuri, tuliamini tungefika mahali tungeelewana vizuri tu, taarifa ambazo nimeletewa na mazingira ya tukio lenyewe yana utata mkubwa.

“Kila mtu ana hisia zake, wengine wanadhani ni Serikali...wengine vinginevyo...tumeagiza uchunguzi ufanywe haraka ili ukweli uweze kubainika, Dkt. Ulimboka tumekuwa naye muda wote.

“Tumeshirikiana vizuri katika jambo hili hadi tukafika mahakamani, vyombo vyote vinajua mgogoro uliopo upo katika hatua gani, kidogo inanipa tabu kama tukio hili litahusishwa na Serikali ili iweje! njia rahisi tusubiri uchunguzi wa kina,” alisema Bw. Pinda

Akijibu swali la Bw. Mbowe la kumtaka aeleze hatua ambazo Serikali itazichukua kuokoa maisha ya wananchi katika hospitali za rufaa ambako madaktari wamegoma, zikiwemo za Bugando, Mbeya, KCMC na Muhimbili, Bw. Pinda alisema Serikali imeomba Hospitali ya Jeshi Lugalo itumike ili kuhakikisha wagonjwa hawakosi huduma na hospitali ndogo zitumike kupunguza madhara.

Aliongeza kuwa, Serikali imechukua uamuzi wa kuwarudisha madaktari waliostaafu ili kukabiliana na hali hiyo pamoja na wale waliopo wizarani warudi hospitalini kutoa huduma.

Lissu ataka Pinda ajiuzulu

Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu, alisema madaktari walipogoma Februari mwaka huu, suala hilo alilishughulikia Mwenyewe na Taifa likatangaziwa mgomo hautajirdia tena.

Alisema kabla miezi mitatu haijapita, madaktari wamegoma tena hivyo kwanini Bw. Pinda asijiuzulu kwa kushindwa kutatua matatizo ya madaktari

Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema; “Mheshimiwa Spika, yako mazingira unayoweza kuwajibika lakini si lazima yakawa yote, mimi sioni kama hili ni moja ya maeneo hayo, nakiri kuwa tatizo hili ni la muda mrefu lakini nimefanya jitihada kubwa kulimaliza na lina changamoto nyingi kwa sababu mambo yameingiliana.

Mgomo wahusishwa na ufadhili

Akiuliza swali kwa Bw. Pinda, Mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Matha Mlata, alitaka kujua kama mgomo huo unachochewa na vikundi vya watu ambavyo vinawatumia baadhi ya madaktari kwa kuwapa fedha ili wahamasishe mgomo ili nchi isitawalike.

Aliitaka Serikali ichunguze uvumi huo ili kuokoa maisha ya
Watanzania wanaokufa.

Ajibu swali hili, Bw. Pinda alisema, mgogoro huo una maneno mengi kwani hata yeye amesikia maneno hayo lakini wameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia ili kujua kama yana ukweli.

Hali ya Dkt. Ulimboka

Hali ya Dkt. Ulimboka anayeendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inaendelea vizuri ambapo hivi sasa amehamishiwa katika Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), chini ya jopo la madaktari ambalo linaongozwa na Daktari Bingwa, Profesa Joseph Kihamba.

Ulinzi kwa ajili ya usalama wa Dkt. Ulimboka, imeimarishwa na madaktari wenyewe kwa kupeana zamu hali inayodhihirisha kuwa, bado wana mashaka na mazingira ya tukio lililomkuta mwenzao.

Kwa mujibu wa Profesa Kihamba, hali ya Dkt. Ulimboka imeimarika tofauti na juzi baada ya kuanza kuanza kutambua watu.

“Tuna matumaini makubwa kuwa atanyanyuka na kuendelea na shughuli zake kama kawaida, hali yake inatupa matumaini,” alisema Profesa Kihamba.

Uongozi wa MOI wanena

Ofisa Uhusiano wa Taasisi ya Mifupa (MOI), Bw. Almas Jumaa, alisema Dkt.Ulimboka amelazwa katika taasisi hiyo ingawa huduma zingine zote zimesitishwa isipokuwa zile za dharura.

Alisema hakuna huduma za kliniki isipokuwa za dharura kwa sababu madaktari haawapo.

Tume ya Serikali

Jumuiya ya Madaktari Tanzania, imesema haina imani na tume iliyoundwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,  Suleiman Kova, kuchunguza mazingira yaliyosababisha Dkt. Ulimboka kujeruhiwa kwa madai hawana imani nayo.

Katibu wa jumuiya hiyo, Bw. Edwin Chitage, alisema wanahitaji tume huru ambayo itafanya uchunguzi huo lakini si tume iliyoundwa na polisi kwani tangu kutokea tukio hilo, baadhi ya madaktari hasa wa Mkoa wa Dodoma wameanza kupata ujumbe wa vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.

“Tunawaomba madaktari wote nchi nzima kuendelea kushikamana hadi Serikali itakapotutimizia madai yetu bila kuogopa vitisho vinavyotolewa na baadhi ya watu,”  alisema

Kutokana na hali hiyo, jumuiya hiyo imesisitiza hakuna njia nyingine ya kumaliza mgogoro huo zaidi ya kukaa meza moja na kufanya mazungumzo na Serikali.

Alisema katika kipindi hiki kigumu, kimewafanya madaktari nchi nzima kuungana pamoja bila ya kuvuruga amani ya nchi na kuwaomba madaktari kuwa watulivu ili wapate haki yao.

Tume ya Haki za Binadamu

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imetoa taarifa ya kusikitishwa na kitendo cha kinyama cha kupigwa Dkt. Ulimboka na kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, kwani kitendo hicho kimekiuka haki ya msingi ya binadamu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji mstaafu, Bw. Amiri  Manento, ambaye ni Mwenyekiti wa THBUB, ilisema kwa mujibu wa sheria ni kumteka na kumtendea mtu vitendo vya kinyama na  udhalilishaji wa utu wake.

Alisema THBUB inalaani vikali kitendo hicho ambacho kimemnyima Dkt. Ulimboka haki yake ya kikatiba ya kuheshimiwa utu wake na kutofanyiwa vitendo vya kinyama na kudhalilisha.

Aliongeza kuwa, tume hiyo inatoa mwito kwa wananchi na vyombo vya dola kuheshimu sheria, utawala wa sheria, haki za binadamu, utawala bora na kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliofanya kitendo hicho cha kinyama.

TUCTA yang'aka

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limeitaka Serikali kuwajibika ipasavyo na kutoa tamko thabiti juu ya tukio, lililompata Dkt. Ulimboka.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa TUCTA, Bw. Nicholas Mgaya, alilaani kauli iliyotolewa na Bw. Pinda, bungeni juzi kuwa Serikali itatoa msimamo wake na liwalo na liwe.

“Serikali lazima ichunguze vyombo vyake vya usalama, msitu wa Mabwepande unajulikana kwa mabaya hivyo lazima itoe tamko,” alisema Bw. Mgaya.

CUF yadai kukosa imani na tume

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema hakina imani na tume iliyoundwa kuchunguza kipigo cha Dkt. Ulimboka, badala yake kimeshauri kazi hiyo ifanywe na vyombo vingine vilivyo huru kwa kushirikisha wanaharakati na asasi za kiraia.

Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi wa CUF Taifa, Bw. Abdul Kambaya, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Majira,

Alisema CUF haina imani na chombo hicho kutokana na mazingira  ya kutatanisha kuhusu gari lililotumika kumteka Dkt. Ulimboka ambalo linadaiwa halikuwa na namba.

Aliongeza kuwa, chama hicho kimesikitishwa na tukio la kutekwa kiongozi huyo, huku Serikali ikiwa na mgogoro na wanataaluma hao ambao wanadai haki zao.

“CUF hatuna imani na tume hii kwani gari lililohusika kufanya utekaji huu ina maana polisi waliokuwa doria hawakuliona barabarani hadi lifike Mabwepande,” alisema Bw. Kambaya.

CHADEMA yahoji intelejensia ya IGP

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimehoji ilikuwaje intelejensia ambayo Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Said Mwema, ambayo amekuwa akiitumia kudhibiti maandamano ya chama hicho kwa madai ya kuashiria uvunjifu wa amani isitumike kuwajua watu waliomteka Dkt. Ulimboka.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mafunzo na Organization wa chama hicho, Bw. Benson Kigaila, alisema mipaka ya intelejensia hiyo inaishia katika maandamano ya CHADEMA badala ya tukio hilo.

Alisema hilo sio tukio la kwanza kutokea nchini kwa watu wanaodai haki zao kufanyiwa vitendo kama hivyo na kuundwa tume ambazo hazina majibu kwa wananchi.

Imendika na Stella Aron, Rehema Maigala, Mariam Mziwanda, Goodluck Hongo, Grace Ndossa.

19 comments:

  1. Mungu amekulipa kwa adhabu unayoipata,mgomo wa daktari unawatesa wagonjwa wengi nchini na kufa. imekuwa vizuri Ulimboka hukufa ili aone adha wanayopata wengine. Mungu akuzidishie maumivu ili afahamu mateso ya wengine sio kwa kusikia tu. hiyo ni faida ya kutumiwa na wanasiasa kwa faida zao za kisiasa. watu wanateseka mahospitalini wewe unakata kinywaji leaders club kweli huu ni utu. hao wanaopiga kelele kwa maumivu yako mtu mmoja hawaoni maelfu wanaoteseka? nina wasiwasi na chama kimoja kilichojaa jamaa wa mikoa ya kaskazini ndio wamekuingiza katika janga hili bila ya wewe mwenyewe kujua. kwanza wamekutumia wewe kusdhupalia mgomo na ipli wamekuteka na kukutesa ili kuzidisha petroli kwenye moto unaowaka bila ya wewe kujielewa.hawa jamaa ni wakatili sana kwenye pesa wanawezafanya chochote tu kwa ajili ya pesa, nakuombea uendelee kuumwa na nimefurahi kusikia hukufa ili uwone mateso yetu. ndugu yangu mmoja alikatwa mguu kutokana na mgomo wenu uliopita sasa amekuwa ni mtu tegemezi basi namuomba Mungu akutese hivyohivyo kama wanavyoteseka wengine na familia zao na wewe familia yako ipate mateso hayohayo. najua wengine watajibu kuniona mkatili lakini ukatili aliofanyiwa ndugu yangu hadi akakatwa mguu si mdogo. Hawa CUF na Chadema ni wehu nilitegemea mtaishupalia serikali ipumguze mishahara na marupurupu ya wabunge na watendaji serikalini ili ziende kwa madaktari mnatoa kauli za kipuuzi kwa madhara ya mtu mmoja wakati maelfu wanateketea na kufa. ndio maana nasema wanasiasa mmwewapata watanzania mandondocha hawana wanalolijua,ndugu yake anakufa hospitali kutokana na mgomo anasapoti madktari,kwani mara ya kwanza walipoongezwa mishahara walibadili mwendo wao hadi sasa wakiongezwa wabadili? ATESEKE SANA HUYO BARADHULI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtanzania mwenzangu kwanza Mungu akurehemu nakukusamehe ww hujui unachosema na huna uhakika na unayoyasema,kama hunachakuandika unyamaze kimya,unavyomwombea maumivu na mateso mwenzako yatakurudia ww Mungu ndiye anahukumu na wala si mwanadamu,je unajua kwa siku dr anatibu wagonjwa wangapi?unajua kuna siku wagonjwa hawana fedha zakununua dawa hao madaktari wanaingia mifukoni mwao wanawanunulia?Je ww unajua mazingira ya kazi za madaktari?unajua madaktari hawagomo kwa ajili ya mishahara nikwa ajili ya watanzania kuhusu vifaaa vya utendeaji wa kazi yao?unajua hospitali kunaukosefu wa vifaa vingapi vinavyowafanya hao hashindwe kufanya kazi kwa ufanisi?unajua wanafanya kazi kwa masaa mangapi? unajua wameshaomba mara ngapi ww ungeweka ktk hiyo nafasi usingejaribu hata kunyanyua mkono au mdomo kushutumu ww huelewi kaa kimya,kwa akili zako timamu kabisa unafanya kazi nyumbani hujaacha fedha,watoto wanasoma kwa shida, halafu uje kazini hakuna vifaa mazingira magumu alafu umsikilize mgonjwa na kumtolea maelezo atibiwe nini ww unafikiri ni kazi rahisi hiyo,HATA SIKU MOJA HAKUNA MTU ATAKUJA PIGANIA HAKI YA MTU MWINGINE WW KAMA WW NDIO UNAJUA MAUMIVI YA KAZI YAKO,na pia hili swala usiliangalie kisiasa .

      Delete
    2. Acha kudanganya watu,daktari gani anatoa pesa mfukoni kumnunulia mgonjwa dawa zaidi ya kutaka rushwa ya kutibu. Nimefiwa na baba yangu ndani ya mikono ya daktari akidai rushwa ya shillingi laki moja,hiyo imetokea kabla ya mgomo. madaktari wa kiafrika ni makatili mno,hawastahili hiyo kazi. na kama wewe ni daktari na wewe pia ulaaniwe kwa kuacha wagonjwa wafe. HIVI KWELI DAKTARI MWENYE AKILI TIMAMU ATAACHA WAGONJWA WAFE KWA SABABU HAKUNA VIFAA,HUYO ULIMBOKA WENU ALIWEKWA KWENYE VIFAA VIPI KUOKOA MAISHA YAKE,NA WENGINE WANATAKA HUDUMA ALIYEPEWA ULIMBOKA KWANI HAKUOMBWA RUSHWA WALA KUDAIWA GHARAMA ZA HOSPITALI. MADAKTARI WA KIAFRIKA MLAANIWE NA WEWE ULIMBOKA MUNGU ASIKUUE HARAKA UTESEKE KAMA WENGINE.NYIE MADAKTARI WA TANZANIA MNAWAADHIBU WATU WALIOWASOMESHA NA KUWALIPIA GHARAMA ZOTE, MLIKUWA MNALALA NA MBUZI VUJIJINI KWETU SASA MMEKUJA MJINI MMEJUA AIR CONDITION NA MAGARI NA WANAWAKE NDIO MAANA MNAUA WATU. ULIMBOKA MMOJA ANATESEKA NCHI INAPIGA KELELE BADALA YA KUPIGA KELELE ZA MATESO YA WENGI. NCHI INA UMOJA WA MADAKTARI,UMOJA WA WANASIASA,UMOJA WA MAWAKILI NA UMOJA WA MAJAJI WOTE HAWA NI WAUWAJI.WEWE BWANA MKUBWA HAPO JUU UGULIWA NA BABA YAKO,MAMAYAKO,MWANAO,MKEO,NDUGU AU RAFIKI UENDE HOSPITALI MADAKTARI WAMUANGALIE TU KWA AJILI YA MGOMO UTAJISIKIAJE? MUULIZE ULIMBOKA NA FAMILIA YAKE KWA SASA WANAJISIKIAJE? JAPO ANAHUDUMIWA NA MAFIA WA NCHI HII. ULIMBOKA KUFA TARATIBU NDUGU YANGU UONE MACHUNGU YA WANAOFIWA NA NDUGU ZAO NA WANAOTESEKA NDIO WALIPA KODI ILIYOKUSOMESHA WEWE SASA UNAWAADHIBU

      Delete
  2. DOLA YOYOTE INA MIHIMILI MITATU SERIKALI,BUNGE NA MAHAKAMA TUHESHIMU MAJUKUMU YA KILA MHIMILI TUSIWE MABINGWA WA KUCHOCHEA UVUNJIFU WA AMANI INAONYESHA DHAHIRI KUWA WAPO WATU WAKIPEWA NCHI HII NI KILIO NA KUSAGA MENO SISI TUNAOMWABU MUNGU ALIYE HAI WALA SIO FREEMASON ASIKIE KILIO CHETU AHAMISHE MAGONJWA YA WAGONJWA WETU WALIOKO MAHOSPITALIN NA NYUMBANI KWA WOTE WANAOTETEA MADAKTARI /WAUAJI WAENDELEE KUUA WANYONGE KUWAWAHISHA KUZIMU KABLA YA MUDA NIWAOMBE WOTE MULIOHAMISHWA KUZIMU MUOMBE HAKI ZENU KWA MUNGU KUPITIA UNYAMA NA UKOSEFU WA UTU WA MADAKTARI NA WAKALA WAO WOTE WANAOWAPA JEURI YA KUUA WATANZANIA WASIONA UWEZO HAINGII AKILINI MADAKTARIWAKITAALUMA,MAWAZIRI,WATU MAARUFU KWENDA SAMUNGE LOLIONDO KWA BABU KUNYWA KIKOMBE HAKUNA ANAYEPANDA KUFA KWANINI LEO WATANZANIA WALEWALE WANASHEREHEKEA WENZAO WAFE SNA UHAKIKA NA MZEE NDESAMBURO NAYE ANAUNGA MKONO LICHA YA KUTUMIA HELIKOPTA YAKE KUPELEKA WAGONJWA SAMUNGE

    ReplyDelete
  3. Jamani tuwe waungwana,tusitoe maoni kwa ushabiki wa upande mmoja.Anaye staili kutoa hukumu ni Mungu peke yake.Hivyo mimi sioni kama Ulimboka kuwa kiongozi wa madaktari amaefanya kosa au anastaili kumpata yaliyo mpata.Tuangalie mazingira wapendwa,leo hii kiongozi akifanya maamuzi magumu kwaajili ya maslahi ya wengi anaonekana yeye kitu ambacho si sahihi.Kama Zitto Kabwe asingi tafuta saini za wabunge ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu,leo hii mawaziri walioenguliwa wasinge enguliwa na mambo yange kuwa kama kawaida.Hoja yangu ni kwamba tutoe maoni kwa kuwa makini na kwa kutafakari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hatutaki siasa hapa kuna watu wanakufa kutokana na mgomo wa madaktari wanaofadhiliwa na mafia wa nchi hii

      Delete
  4. PINDA UKWELI UNAUJUA KUHUSU Dr. ULIMBOKA UNATAKIWA KWANZA WEWE UJIELEZE KUHUSU KAULI YAKO YA KIPUUZI "LIWALO NA LIWE" ULIMANISHA NINI HASWA WEWE WE KIONGOZI GANI USIE NA MAONI YA HEKIMA KWA WATU WAKO? HAKINA SERIKALI INATAMBUA VZR KUTEKWA KWA HUYU MDOGO WETU Dr. ULIMBOKA. ACHENI UPUUZI SISI SIO WATOTO WADOGO, IWEJE ASKARI KANZU AMFUATE HOSPTALI KWENDA KUMFUATILIA Dr. ULIMBOKA NA AKAOKOLEWA NA WENZIE????????????? NINYI WOTE AKINA PINDA NI WAPUMBAVU SANA NA SERIKALI YAKO. LAKINI IPO SIKU YENU YA MWISHO ITAFIKA TU.

    ReplyDelete
  5. KWELI SERIKALI IMEFIKIA PABAYA MAANA KAULI SIYO NZURI KWA WANANCHI WAKE MAANA ALIPOCHAGULIWA ALIABA MIMI PINDA NITAITUMIKIA SERIKALI YANGU KWA HALI NA MALI SASA HIZO KAULI ZINGINGINE SIYO ZA KIONGOZI MAANA, KIONGOZI NI YULE MWENYE HEKIMA WAKATI WOTE NA KUTAFAKARI KABLA YA KUJIBU SWALI HATA KAMA UMETUKANWA MAANA UONGOZI NI JALALA NA NILAZIKA UKUBALI YOTE KAMA ULIVYOKUBALI KUCHANGULIWA NDIYO MAANA KUNA WAKATI WA KULIA NA WAKATI WA KUCHEKA SASA WAKTI WA KULIA UKIFIKA SASA WEWE UNAONA NI MZINGO MBONA WAKATI WA KUCHEKA USIONE NI MZINGO, NA VIONGOZI WA JUU MNAFUNDISHA NINI, NA JE INGEKUWA NDIYO CHAMA CHA UPINZANI KIMESEMA HIVYO LEO ANGAKUWA WAPI, NDIYO MAANA VIONGOZI WA JUU WANACHUKUA MADARAKA MKONONI KUENDESHA KESI NA KUFANYA KAMA HIYO KAULI LIWALO NA LIWE, MFANO NI MBUGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA, ILA MUNGU ANAJUA WATU WAKE MMEMTOA LAKINI SASA NDIYO KAPATA NAFASI NZURI NA MFANO WA KUTEMBEA TANZANIA NZIMA, NA SASA NDIYO MMEWASHA MOTO HAKUNA MWENYE KUITAKA TENA VIONGOZI WA JUU MLIOKO MADARAKANI MAANA HAKUNA HAKI ILA NI UNYANYASAJI WA KINYAMA SANA, NA HIYO SIYO DAWA ILA NDIYO MNATENGENEZA DAWA KALI TENA MUARUBAINI TENA MWITU

    ReplyDelete
    Replies
    1. hatutaki siasa hapa kuna watu wanakufa kutokana na mgomo wa madaktari wanaofadhiliwa na mafia wa nchi hii ndio hao kina unaowataja

      Delete
  6. SERIKALI ZEZETA HUUNGWA MKONO NA WANANCHI MAZEZETA KAMA HAWA WANAOFURAHIA TUKIO HILI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na wewe ni zaidi ya zezeta kwa kufurahia baba yako,mama,watoto na wananchi kufa kwa mgomo wa madaktari,ulimboka haponi huyo laana ya waliokufa na wanaoteseka ndio inamkaanga

      Delete
    2. mashetani si lazima yaonekane kwa macho na mapembe yao utayatambua hata kwa kauli zao tu,huitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu kuwatambua,furaha na maombi yako yako juu ya mateso kwa ulimboka hayamuongezei maumivu bali moyo wa kishujaa kwa wengine.umeyaona mateso ya ndg yako aliyekatwa mkono kuwa ni makali mno kuliko ya ndg zetu wanakufa vijijini kwa kukosa hata panadol?je ni ulimboka aliyeshindwa kupeleka dawa huko?mbona hujawalaani wanaosababisha mateso na dhiki kwa kina mama wajawazito na watoto wanaripotiwa kufa kila siku huko vijijini tena kwa magonjwa yanayotibika tena kirahisi tu kama malaria?takwimu zako za watu wanaoteseka zinaishia kwa ndg yako tu aliyekatwa mkono?mateso na kuteka nyara watu kamwe hazitanyamazisha sauti za wadai haki,damu za watu ktk misitu ya pande na maeneo mengine tusiyoyajua zimeanza kuwaumbua,ni suala la muda tu wako wengine watakiri hadharani yaliyojificha nyuma ya pazia.

      Delete
    3. Mbona wakiambiwa wakafanye kazi huko vijijini kwao wanakataa. Mungu muadhibu tu huyo Ulimboka hana ushujaa wowote zaidi ya ukatili na ushetani. malipo anayapata hapahapa duniani. hata huko vijijini wanakufa sasa hivi zaidi kutokana na mgomo wa madaktari. wewe ni shetani wa miguu saba unayetetea maangamizi. milkuwa mnalala na mbwa,mbuzi na kondoo kwenye vibanda vya udongo sasa mjini kumewafundisha starehe mpaka mnakufuru. KUFA TARATIBU ULIMBOKA UONE MACHUNGU YANAYOWAPATA WENGINE.WANAOFADHILI MGOMO,TANZANIA MAFIA NA WANAOSAPOTI MGOMO HUU NI WAUWAJI KULIKO HATA HIYO SERIKALI YENYEWE

      Delete
  7. WAALIMU WALIPOTANGAZA MGOMO UKAWEKEWA PINGAMIZI MAHAKAMA KUU KITENGO KAZI MWENYEKITI WAO ALILAZIMIKA KUTANGANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUWA MGOMO UMESITISHWA WAALIMU HAWAKURIDHIKA NA UAMUZI HUU LAKINI ILIBIDI WATII SHERIA HALALI HAWA MADAKTARI WAO SIO WATANZANIA NI DHAHIRI SASA WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU,HAKI ZA KIRAIA,WAANDISHI WA HABARI,NA BAADHI YA VIONGOZI WA KIROHO WAMEAMUA KUWA VYAMA VYA SIASA VISIVYO NA USAJIRI WAACHE UNAFIKI KUFANYA SIASA ZA MAJI TAKA

    ReplyDelete
  8. UGOMVI WA PANZI NEEMA YA KUNGURU, NAMAANISHA MVUTANO WA SERIKALI NA MADAKTARI, IZIRAEL ANACHUKUA ROHO ZA NDUGU ZETU, USHABIKI HAUFAI, ACHA TU DR. ULIMBOKA NAYE APATE MAUMIVU KWANI MGOMO WAO UMEUA WANANCHI WANGAPI? SASA HIYO YA KILA MTU KULAANI KITENDO HICHO KWANINI MSIANGALIE WANANCHI WENGI WALIOPOTEZA MAISHA YAO. UTAKAPOPATA MGONJWA ALIYE MAHUTUTI HAPO NDO UTAJUA MGOMO HUU USIVYOFAA;

    ReplyDelete
  9. BAADHI YAVIONGOZI WA KIROHO UTAWASHANGAA KAULI ZAO KAMA WANA SIASA HIVI WATU WANAOKUFA SASA HIVI MUNAWAZIKA KWA SALA IPI KWAMBA BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA KUTOTOA TAMKO MUMEIONEA HAYA INJILI NA YESU ATAWAONEA HAYA SIKU YA MWISHO ACHENI KUFANYA SIASA

    ReplyDelete
  10. Madaktari waoneeni huruma watanzania wenzenu wanakufa.kama swala lenyewe liko mahakamani kwanini hamtaki kuwa na subira? mjue hatima ya madai yenu? Mgomo sio njia ya kutatua matatizo bali jia yakujiongezea matatizo .kama mnauhakika na mnachokifanya kwanin hata mnadhiriki kukiuka amri ya mahakama? hebu kuweni wasaarabu katika hili.
    pia enyi wana siasa mnaochochea issu za migomo ya madakatari hamoni kama mnawapoteza wapigakura wenu? maana kwa uchocheziwenu wapinga kura wenu wanakufa,wanakuwa vilema.mbona mwajikaanga na mafuta yenu wenyewe??????????

    ReplyDelete
  11. KUNA MAFIA TANZANIA INAFADHILI MGOMO WA MADAKTARI. NYERERE ALIKATAA NENO UMOJA WA KINA FULANI,UTALETA MADHARA NCHINI. SASA KUNA UMOJA WA WACHAGA,WAHAYA, NA WENGINEO TENA BILA AIBU WANAPANGA MIPANGO YA KIMAFIA NCHINI NA SI YA MADAKTARI TU HATA KWENYE MAHAKAMA NA SEHEMU ZINGINE. UMOJA TUNAOTAKA NI WA WATANZANIA TU MWINGINE WOWOTE HAYA NDIO MADHARA YAKE. WAPO WANAOFADHILI MGOMO WA MADAKTARI KWA MASLAHI YAO BINAFSI

    ReplyDelete
  12. Naukana utanzania ! kila mmoja kawa mjuaji...nikiwemo mimi..kwa heri ila ntamis jina la Bongo.Byeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete