14 June 2012
Polisi Dar wamnasa mfuasi wa Al-Qaeda
Na Salim Nyomolelo
JESHI la Polisi nchini, linamshikiria raia wa Ujerumani aliyefahamika kwa jina la Bw. Emrah Erdogan, ambaye aliyekamatwa jijini Dar es Salaam, Juni 10 mwaka huu.
Bw. Erdogan ambaye kwa jina lingine anaitwa 'Abdulrahaman Othman', inadaiwa ni mfuasi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Kamishna wa jeshi hilo, Bw. Isaya Mngulu, alisema kijana huyo ana umri wa miaka 24.
Alisema Bw. Erdogan anadaiwa kushiriki mapambano mbalimbali nchini Afghanistan na hivi karibuni alishirikiana na Kikundi cha Al-Shabab kufanya ugaidi.
Aliongeza kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kumuhoji wakishirikiana na mataifa mengine.
“Tunashirikiana na nchi za Uganda, Kenya na Ujerumani kumhoji ili kubaini taarida zake, baada ya hapo tutatoa taarifa kwa Watanzania,” alisema Bw. Mngulu.
Hata hivyo, Bw. Mngulu alisema jeshi hilo linatambua mchango wa wananchi ambao ndio uliosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa na kuongeza kuwa, hiyo ndio dhana halisi ya ulinzi shirikishi.
“Jeshi la Polisi linawahakikishia wananchi kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara kukabiliana na vitisho vyote vya uhalifu na ugaidi, natoa wito kwa wananchi waendelee kutupa ushirikiano katika vyombo vyetu ili kuimarisha amani na utulivu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
NIWE WA KWANZA KUWAPONGEZA ASKARI HAO NA WAZAWADIWE KWANI HUYU ASKARI ANGESABABISHA MILIPUKO JESHI LA POLISI LINGELAUMIWA KWA UZEMBE NA NDIO UTAMADUNI WETU .HUYU GAIDI HAWEZI KUJA TU TANZANIA ANA WENYEJI WAKE ABANWE AWATAJE WOTE KWANI MAWAKALA WA UKOLONI MAMBOLEO WAPO
ReplyDelete