30 December 2011

EWURA yacharuka

*Bodi yafungia vituo vinne vya mafuta Dar
*Vilikaidi agizo la kujieleza kwa maandishi
*Kingine chapewa kusudio kusitishwa leseni
*DPP aombwa kufungua kesi uhujumu uchumi

Na Salim Nyomolelo

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), jana imeanza kuchukulia hatua ya kuvifungia vituo vinne vya mafuta Jijini Dar es Salaam ambavyo
Maofisa kutoka Manispaa ya Ilala, Bw. Uswege Abel (kulia), ambaye ni Mthamini wa Majengo na Ofisa Ardhi, Bi. Fatuma Rashid, wakisindikizwa na Polisi jana, kuhakiki nyumba za wakazi wa Jangwani Magharibi, walioathiriwa na mafuriko, yaliyotokea Dar es Salaam hivi karibuni.

Baadhi ya waathirika wa mafuriko, wanaoishi kwenye Kambi iliyoko Shule ya Msingi Gilman Rutihinda, Kigogo, Dar es Salaam wakipata matibabu, kutoka kwa wauguzi wa Manispaa ya Ilala jana, Bi. Frola Chilwa. (kushoto) na Teddy Uledi.

CUF: Hamad Rashid tulimbana tuhuma 11

*Kamati yasisitiza zote alizikubali, akazitaka kwa maandishi

Na Rehema  Maigala

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema licha ya Mbunge wa Wawi, Zanzibar, Bw. Hamadi Rashid Mohammed, kukataa kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na
Naibu Katibu Mkuu, Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Julius Mtatilo (kushoto), akikabidhi msaada wa mfuko wa unga wa sembe jana kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigogo, Bw. Emmanuel Riwa, kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es Salaam hivi karibuni.

Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu, Uchumi na huduma za Kijamii, Dkt. Bartholomew Bwire Rufunjo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu hatua ya uendelezaji wa sekta ya miundombinu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Picha na Prona Mumwi)

Wataka Katiba Mpya iondoe kinga kwa rais

Na Yusuph Mussa, Korogwe

BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, wamesema kama Katiba Mpya itaendelea kumlinda rais asishtakiwe akiwa madarakani na baada ya

EAC yaibua miradi 244 sekta ya uchukuzi,nishati

Na Gabriel Moses

JUMUIA ya Afrika Mashariki (EAC) imekamilisha na kupitisha mkakati wa ushirikiano katika sekta ya miundombinu ya kiuchumi hususan miundombinu ya Uchukuzi na

Wanaong'ang'ania madarakani Jumuiya ya Wazazi waonywa

Na Queen Lema, Arumeru

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Bw Anthony Musani, amewataka viongozi wa Jumuiya ya
Kiungo wa timu ya soka ya Kimara Kids, Bosingwa Pankras (kulia), akiondosha hatari langoni mwake, huku mshambuliaji, Juma Mohamed wa New Boys ya Gongolamboto, akitaka kumnyang'anya katika mchezo maalumu ulioandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA) kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.

Bundi bado aranda Yanga SC

Na Mwandishi Wetu

BUNDI bado anaonekana kurandi katika Klabu ya Yanga, baada ya jana baadhi ya wachezaji kuibuka na kudai kwamba, wanashangaa uongozi kushindwa kuwalipa

BD kuteta na klabu leo

Na Amina Athumani

CHAMA cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD,) leo kinatarajia kukutana na klabu zote zinazoshiriki Ligi ya Kikapu ya RBA katika Ukumbi wa

Suarez aingia matatani tena

LONDON, England

CHAMA cha Mpira wa Miguu England (FA), kimfungia kucheza mechi moja na faini ya pauni 20,000, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez kutokana na

29 December 2011

NCCR: Kafulila amejipalia mkaa

*Dkt. Mvungi: Washauri wake wanamdanganya
*Asema Mahakama haijatengua azimio la kikao
*Kafulila: Sina cha kusema, naheshimu uamuzi


Na Peter Mwenda

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimesema mbunge wake wa Kigoma Kusini Bw. David Kafulila, ambaye alivuliwa uanachama kutokana na

Katuni 29-12-2011


Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Arusha, Bi Judith Lubuva (kushoto), akimtwisha ndoo ya maji, mwanafunzi Samwel John wa shule ya Msingi Meru, baada ya kuzindua kisima cha maji, kilichochimbwa kwa msaada wa benki hiyo, Jijini Arusha juzi, Wanaoshuhudia ni wanafunzi wa shule hiyo.

Mgomo wa mafuta sasa wahamia Kilimanjaro

Na Heckton Chuwa, Moshi

SIKU chache baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), iwaadhibu kwa kifungo na
Mkuu wa Vodacom Foundation, Bw. Yessaya Mwakifulefule akisaidia kumtwisha Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mkunguni B, Kata ya Hananasifu Bw. Andrew Mkude, kiloba cha sukari, baada ya Vodacom kutoa msaada wa mchele, sukari, unga wa sembe, mikate na maji ya kunywa kwa waathirika wa mafuriko walioko kwenye kambi ya Hananasifu Dar es salaam juzi.

Kamati kumjadili Hamad Rashid Des. 30

*Tuhuma zake kufikishwa Baraza Kuu kwa uamuzi

Rehema Maigala na Surah Mushi

SIKU moja baada ya Mbunge wa Wawi, Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Hamad Rashid Mohammed kukataa kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na

Polisi kizimbani kwa kudhalilisha watoto 3

Rehema Mohamed na Paulina Lyapa

POLISI mwenye namba D 5882 Koplo Richard Singano (47) wa Kituo Kidogo cha Gongo la Mboto amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa
Siku chache kabla ya mwaka mpya, Januari mosi, 2012, mkazi huyu wa Dar es Salaam, alikutwa na kamera yetu , akipita kwenye Barabara ya Livingstone jana, wakati akitafuta wateja wa kununua kuku kwa ajili ya sikukuu.

Ukata wa soko waikosesha serikali bilioni 19/-

Na Mnaku Mbani

KATIKA hali inayoonyesha kuongezeka kwa ukata katika masoko ya fedha nchini, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeshindwa kukusanya sh. bilioni 20. Kiasi hicho kilitarajia

TRA kurejesha VAT kwa wageni

Na Zena Mohamed

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza utaratibu wa kuanza kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT iliyolipwa na raia wa kigeni punde watakapoondoka na
Mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho akimtoka Roger Johnson wa Wolves katika mechi ya Ligi Kuu England iliyofanyika katika Uwanja wa Emirates, London juzi. Timu hizo zilifungana bao 1-1.

Yanga kwazidi kufukuta

*Wanachama viongozi kung'atuka

Na Mwali Ibrahim

BAADHI ya wanachama wa Yanga, wameutaka uongozi wa klabu hiyo kujiuzulu, kutokana na kushindwa kuiongoza. Hali imekuja kutokana na kauli ya Kocha Mkuu wa

Nelly ashika nafasi ya 5 China

Na Mwali Ibrahim

MREMBO Nelly Kamwelu, ameshika nafasi ya tano katika mashindano ya Dunia 'Miss Tourism Queens Internation' yaliyofanyika juzi nchini China akiwa mshiriki pekee

Rihanna amwigiza Michael Jackson

LONDON, Uingereza

RIHANNA ametayarisha video ya wimbo wake mpya, ambayo anaonekana akiwa amevaa mavazi yanayobana mwili huku akicheza kwa kuigiza mitindo ya

28 December 2011

Hamad Rashid aikataa kamati

*Asema wajumbe wake hawana sifa, akataa kuhojiwa
*Ataka ufafanuzi katiba iliyoruhusu kamati kumuhoji
*Tuhuma zake sasa kufikishwa kwenye Kamati Kuu


Na Agnes Mwaijega

MBUNGE wa Wawi, Zanzibar Bw. Hamad Rashid Mohammed, jana aligoma kuhojiwa na

Waishio mabondeni watakiwa kuondoka

*RC atoa tamko rasmi, huduma za umeme, maji kukatwa

Na Anneth Kagenda

WAKATI Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), ikitoa tahadhari kwa wananchi katika mikoa mbalimbali kuchukua tahadhari juu ya mvua zinazoendelea kunyesha na

Aliyemchoma kisu Diwani ajisalimisha Polisi Turiani

Na Mwandishi Wetu, Mvomero

MKURUGENZI wa Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro Bw. Songa Mgweno, ambaye anayetuhumiwa
Dereva wa gari namba T 641 BTL, akimwangalia Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, wakati akiandika maelezo yake, baada ya kukamatwa kwa kuvunja sheria, eneo la Karume, Dar es Salaam jana.

TMA: Mvua zinazokuja zitaendelea kuleta maafa

Gabriel Moses na Surah Mushi

SIKU chache baada ya mvua kubwa zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo kuleta maafa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hasa waishio mabondeni, Mamlaka ya Hali ya
Mwendesha Pikipiki ya abiria (Bodaboda), akiwa amesimama kwenye foleni ya magari, Barabara ya Tanda Mti, Dar es Salaam juzi, huku akisoma gazeti, bila kujali usalama wake.

Mkazi wa jiji (jina halikufahamika) alikutwa na mpigapicha Wetu akihamisha thamani zake kutoka eneo la Kigogo Bondeni. Hata hivyo haikufahamika alikokuwa akizipeleka.

Yanga sasa wamkumbuka Mosha

*Wapanga kuandama kumrejesha

Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wanachama wa Yanga, wameanza harakati za kumtafuta Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Davis Mosha, arejee na ili kuokoa jahazi
Mchezaji wa kikapu wa Sacramento Kings, Tyreke Evans (katikati) akiambaa na mpira katikati ya wachezaji wa Los Angeles Lakers, Derek Fisher (kushoto) na Kobe Bryant wakati wa robo ya nne ya Ligi Kuu ya mchezo huo Marekani (NBA), iliyochezwa Uwanja wa Sacramento, California juzi.Kings ilishinda kwa pointi 100-91.

Mkwassa ataka tatu za kirafiki

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), ameliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuitafutia timu hiyo mechi tatu za kujipima nguvu kabla

FIFA 'yampa ulaji' Joan Kombe la Dunia

Na Zahoro Mlanzi

KATIBU Mkuu wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Joan Minja, ameteuliwa na Shirikisho la Kimtaifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kuwa

Polisi Iringa 'yaota' kucheza Mapinduzi Cup

Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya Polisi ya Iringa, imepanga kukaa meza moja na waandaji wa mashindano ya Kombe la Mpinduzi, kuomba wapewe nafasi ya mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga ambayo

27 December 2011

Hamad Rashid kikaangoni leo

*Kamati ya nidhamu, maadili kumuhoji na wenzake 12
*Wote watuhumiwa kukiuka utaratibu, katiba ya chama
*Ripoti ya mahojiano kuwasilishwa Kamati ya Utendaji
*Mtatiro: Njia aliyotumia haiwezi kukijenga chama chetu


Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeanza mchakato wa kumaliza mgogoro unaoendelea ndani ya
Mbunge wa Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu' akiongoza mtumbwi kuvuka mto Ruvu uliojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha milima ya Upare na mto huo kujaa,na kusababisha wananchi wa Majengo na Manga-Mtindiro kukosa mawasiliano. wengine ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw Erasto Sima (katikati) na katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga, Bw. Acheni Maulid.

Mganga Mkuu Misungwi atimuliwa kazi

*Adaiwa kuhusika na ubadhirifu mil. 335.5/-

Na Daud Magesa, Mwanza

HALMASHAURI ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, imemfukuza kazi Mganga Mkuu wilayani humo, Dkt.Daniel Nyambega, kwa ubadhirifu wa

DC kumweleza JK ubabaishaji bei ya korosho

Na Steven Augustino, Tunduru

WAKUU wa mikoa inayolima zao la korosho nchini, wameazimia kufikisha kilio chao kwa Rais Jakaya Kikwete juu ya ubabaishaji wa bei ya zao hilo ili aweze kutoa tamko

Diwani CHADEMA apigwa kisu, alazwa

*Mtuhumiwa ni mpenzi wake, kiongozi wa chama

Na Mwandishi Wetu, Mvomero

DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi.Tusekile Mwakyoma (28), amechomwa
Mama akiwa na mtoto wake mchanga mgongoni, wakati akipandaji moja ya miti 4000, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, ulioko Jijini Mbeya, mwishoni mwa wiki, ikiwa ni mikakati ya kuboresha mazingira ya mji huo.

Jairo hana kosa, ni majungutupu-Mchungaji

Na Anneth Kagenda

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Dar es Saama, Mchungaji Antoni Lusekelo, ameibuka na kusema kuwa sakata la Katibu Mkuu wa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova (kushoto), akisikiliza taarifa ya Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi hilo, Pascal Luhuna, alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hivi karibuni.

Waanza kuchangishana kujenga barabara

Na David John

WANANCHI wa Kata ya Ukonga Manispaa ya Ilala Dar es salaam, wameamua kuchangishana fedha ili kukarabati barabara yao iliyosombwa na  mvua kubwa hivyo kutenganisha

Ajifungua chini ya mwembe

Na Bryceson Mathias, Mvomero

MKAZI wa Kitongozi cha Ifumbo wilayani hapa, Bi. Selina Jovini, amejifungua mtoto wa kike chini ya mti wa muembe baada ya kubebwa umbali wa kilomita 10 kufuata zahanati

Papic avunja ukimya Yanga

*Adai uongozi unamtenga
Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic ameamua kuweka wazi kinachoendelea ndani ya klabu hiyo, baada ya kusema kama hazijafanyika jitihada za

Matumla, Oswald hakuna mbabe

Na Mwali Ibrahim

MABONDIA Rashid Matumla na Maneno Osward, wametunishiana misuli na kutoka droo katika pambano lao lisilo la ubingwa lilofanyika katika Ukumbi wa

Ilala marufuku 'Disko Toto kimya

Na Mohamed Kazingumbe

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, imepiga marufuku vibali vya 'Disco Toto' pamoja na maonesho ya 'Khanga Moja' katika kumbi zote.Akizungumza

23 December 2011

JK ajionea athari za mafuriko Dar

*Aagiza waishio mabondeni kuhamishwa haraka
*Atembelea waathirika 4,909 waliopewa hifadhi
*Vifo zaidi vyaongezeka, sasa wafikia watu 20
*Dkt.Shein, CUF watuma salamu za rambirambi


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na waathirika wa mafuriko kwenye kambi iliyotengwa na serikali Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa mkoa Bw. Sadik Meck Sadik na Meya wa Ilala Bw. Jerry Silaa.
Na Waandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amewaagiza viongozi wa Jiji la Dar es Salaam, kuhakikisha wananchi
Daraja kubwa la Kigogo likiwa limekatika kwenye ukingo wa Barabara kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam.

...amteua Lubuva Mwenyekiti NEC

Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amemteua Jaji mstaafu, Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Mbali ya uteuzi huo, Rais Kikwete pia amemteua
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong II, kwenye ubalozi wa nchi hiyo Mikocheni, Dar es Salaam jana.

Hamad Rashid akanusha kuomba radhi

*Asema Maalim Seif anakabiliwa na mashtaka manne
*Akusudia kumshtaki kwa Lipumba achukuliwe hatua


Na Benedict Kaguo, Tanga

MBUNGE wa Wawi, Zanzibar, Bw.Hamad Rashid Mohamed, amesema anakusudia kuwasilisha mashtaka manne dhidi ya Katibu Mkuu wa chama

Msaada kwa walioathirika, Mafuriko

Wafanyakazi wa Taasisi za Islamik (HELP) na Pole sana Bw. Samir Adam Rajab, akitoa msaada wa chakula na maji kwa watanzania walioathiriwa na mafuriko, Dar es Salaam jana.

Wafanyabiashara wa soko dogo la Kigogo, Dar es Salaam, wakisaidia kuinua Baiskeli ya magurudumu matatu (Guta) iliyokuwa imebeba magunia ya viazi na kuanguka karibu na soko hilo jana.

Simba, Yanga kuchangia waathirika

Na Mwali Ibrahim

TIMU za Simba na Yanga, zinatarajia kuchagia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Simba na Yanga

Yanga yahifadhi waathirika 400

Na Zahoro Mlanzi

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na kusababisha mafuriko yaliyoleta maafa makubwa, zimesababisha Klabu ya

Ujerumani yaandaa filamu ya Kitanzania

Na Gabriel Moses

KITUO cha Utamaduni cha Ujerumani kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam, kimeandaa filamu inayoelezea historia ya Mtanzania wa kwanza kuigiza na Wajerumani, kabla na baada ya

22 December 2011

Mkakati wa TBS utainua kipato cha Taifa

Na Daud Magesa,
Mwanza

SERIKALI Mkoani Mwanza imesema mpango wa Shirika la Viwango  (TBS) kuanzisha mkakati wa udhibiti wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora,zinazoingizwa nchini utasaidia kuinua pato la taifa, kulinda ajira na afya za walaji hasa masikini Watanzania.


Eneo la Jangwani jiji Dar ni moja ya maeneo yaliyo athirika na matukio ya mafuriko, hili ni eneo linalojulikana kwa matukio kama haya kila mwaka, na wakazi wake walisha Ombwa kuhama makazi hayo kutokana na Athari kama hizo pindi mvua kubwa inaponyesha. Kwa hali hii Inatufndisha nini sisi Watanzania??

Kampuni ya kilimo kutekeleza Kilimo Kwanza

Na Lilian Justice,
Morogoro
 
KAMPUNI  ya Zana za Kilimo Tawi la Morogoro imeamua
kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete  la ’Kilimo Kwanza‘ katika kutekeleza agizo hilo kwa vitendo zaidi.

Waziri Simba awataka maofisa kubuni miradi

Na Ramadhan Libenanga,
Morogoro

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Sofia Simba amewataka maofisa Maendeleo ya Jamii  ngazi zote kuhakikisha wanatekeleza na kubuni  miradi mbalimbali inayopelekwa katika maeneo yao kwa ajili ya kusaidia jamii hususani makundi maalumu.

Mkuu wa Mkoa - Mbeya

Kandole
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro, akimpa pole mmoja wa waathirika wa upepe ulioezua nyumba 88, za wakazi wa Kata ya Galula, Wilayani Chunya, Bibi Maria kutokana na upepo mkali na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. (Picha
na Esther Macha)

MWENYEKITI -NCCR - akiongelea Mafuriko Dar


Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tahadhari ambayo wananchi wanatakiwa kuchukua kutokana na maafa ya mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam. (Picha na Peter Mwenda).

Serikali Ilijitahidi kwenye Uokoaji


Maafa ya Mvua - Dar es alaam

Maafa ya Mvua - Dar es alaam

Madrid yatinga 16 kwa kishindo

MADRID,Hispania

TIMU ya Real Madrid imesonga mbvle kirahisi kwenye michuano ya Kombe la Mfalme maarufu kama Copa del Rey  baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1  dhidi ya timu inayocheza ligi daraja la tatu Ponferradina, huku timu za  Sevilla, Espanyol na Mallorca nazo zikisonga mbele baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao.

Carlos Bianchi amwagia sifa Messi

BUENOS AIRES,Brazil

KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina, Carlos Bianchi,amesema kwamba hana wasiwasi na kiwango alichonacho nyota wa Barcelona, Lionel Messi,na amesema kwamba kwa sasa mchezaji huyo ameshawapiku wachezaji nyota wa zamani Diego Maradona na Pele.

Korea Kusini yapata kocha mpya

SEOUL,Korea Kusinbi

KOCHA wa mabingwa wa ligi,Jeonbuk Hyundai Motors,Choi Kang-Hee,ametangazwa kuwa ndiye kocha mpya wa timu ya Taifa ya Korea Kusini.

21 December 2011

Maafa Dar

*Mvua kubwa yasababisha mafuriko, upotevu wa mali
*Waishio mabondeni wakosa makazi, vifo vyaripotiwa
*JWTZ, Polisi watumia helikopta zao kuokoa wananchi
*Serikali kutumia polisi kuhamisha wananchi kinguvu

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, jana walikubwa na mafuriko, baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha baadhi ya nyumba kujaa maji na watu kukosa makazi kama inavyoonesha katika picha hizi.
Na Flora Amon

MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana hadi asubuhi katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam, imesababisha vifo, uharibifu wa mali na
Wakosa makazi baada kutokana na mafuriko yaliyotokea.

Athari ya mafuriko, baada ya mvua iliyonyesha jana.

Wamasai waliokiuka mila watembezwa 'utupu'

Na Queen Lema, Arusha 

KATIKA hali isiyo ya kawaida, vijana wa Kimasai 'Morani', juzi waliwatembeza utupu watu watano wa kabila hilo kutoka eneo la Matevesi, mkoani Arusha kwa madai ya

Waandamana, wavaa magunia kupinga posho za wabunge

Na Waandishi Wetu, Arusha

WANAHARAKATI wa Kikundi cha Wazalendo Associate, mkoani Arusha, jana wameandamana kwa miguu umbali wa kilometa saba wakiwa wamevaa magunia mwilini ili
Rais Yoweri Museveni wa Uganda, akizungumza na wakulima kutoka Muleba, mkoani Kagera (hawako pichani), walipomtembea nyumbani kwake, Kijiji cha Rwakitura Nchini humo juzi, wakiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, aliyeketi kushoto.

Nileteeni majina ya wala rushwa CDA-Mkurugenzi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Mhandisi Martin Kitilla, amewataka wananchi kumpelekea kwa siri majina ya watendaji wa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (aliyesimama kulia), akiongea na waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), kuhusu umuhimu wa kuboresha mfuko huo kwa faida kizazi cha sasa na kijacho, wakati wa kongamano la kwanza la waratibu wa mfuko huo, mjini Morogoro juzi.

SUMATRA yakana kupanda nauli mabasi ya mikoani

Na Anneth Kagenda

WAKATI wananchi wakiilalamikia serikali kuhusu kupanda ghafla kwa nauli za mikoani katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi, Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na

Kibanda kizimbani kwa madai ya uchochezi

Na Rehema Mohamed

MHARIRI Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Bw.Absalom Kibanda na mwenzake wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la
Mkurugenzi wa Business Times Limited, Bw. Rashidi Mbuguni akimfariji Bi. Joyce Muyo ambaye ni mke wa marehemu Fredrick Muyo, aliyekuwa mfanyakazi wa Business Times kitengo cha biashara. Alifariki juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Ngassa avunja mwiko Yanga

*Aipiga bao, mashabiki vichwa chini

Na Zahoro Mlanzi

HATIMAYE mshambuliaji machachari wa timu ya Azam FC, Mrisho Ngassa amevunja mwiko baada ya kufunga bao moja kati ya mawili dhidi ya timu yake ya

Wazambia kuichezesha Twiga Stars

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeteua waamuzi kutoka Zambia kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC), kati ya

Mwambungu aipiga jeki Majimaji

Na Mhaiki Andrew, Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu ametoa msaada wa mipira 11 yenye thamani ya sh. 660,000 kwa Klabu ya Majimaji ili iweze kufanya vizuri katika

20 December 2011

Tendwa amlilia Kafulila

*Ataka busara itumike kumaliza mgogoro uliojitokeza
*Asema ipo hatari ya chama hicho kupoteza umaarufu
*Nape: Mimi si mfuasi wa siasa za kufukuza vijana
*Aishukuru NCCR kurudisha jimbo hilo kwa CCM


Agnes Mwaijega na Paulina Lyapa

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa, amesema hajafurahishwa na uamuzi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, kwa tiketi ya

Wauza mafuta wafanya mgomo baridi

*Wasababisha kero kubwa, wananchi walalamika
Msururu mrefu wa magari ukisubiri kununua mafuta kwenye kituo cha TSN, kilichokuwa kikiuza mafuta, kwenye makutano ya Barabara za Shekilango na Bagamoyo, Dar es Salaam jana. Hii ni mara ya pili kwa wakazi wa Jiji kukosa mafuta, baada ya wauzaji kugoma kutoa hiyo wakisubiria bei mpya.
Zena Mohamed na Flora Amon

BAADHI ya wamiliki wa vituo vya mafuta Jijini Dar es Salaam, jana walifanya mgomo baridi wa kutouza mafuta ya petroli katika vituo vyao ili kupinga

JK aapisha mabalozi

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi saba na baadhi ya watendaji wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ikulu Dar es Salaam jana, baada ya kuwaapisha mabalozi hao.

Acheni kuuza ardhi za wanyonge-CUF

Na Peter Mwenda

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Bw.Julius Mtatiro, amewaonya viongozi wa serikali za vijiji na kata wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani kuacha tabia ya

Wizara ya Afya yazindua baraza la tiba asili

Na Salim Nyomolelo

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imezindua baraza linaloshughulikia masuala ya tiba asili nchini kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma hizo na kuondoa
Wakazi wa Mji wa Kibiti, wilaya ya Rufiji, mkoa wa Pwani wakishirikiana kuchinja moja ya Ng'ombe 65, zilizotolewa kwa wananchi wa wilaya hiyo, kujiandaa na sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Diwani CCM aliyevamiwa na majambazi

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Bw. Hamisi Mgeja (katikati), Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Bw. Mwenzetu Msabaha (kushoto) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa, Dkt Fredirck Mlekwa, wakimjulia hali Diwani wa CCM, Kata ya Pandagihiza, BW. Ng'honge Nkwabi, aliyevamiwa na kukatwa mapanga na majambazi juzi.

Kili Stars, Z'bar Heroes kufungua Mapinduzi Cup

Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), inatarajia kufungua pazia la mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup), kwa kuumana na

TBF kumpa tuzo Jaji Ramadhan

Na Amina Athumani

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), linatarajia kutoa tuzo ya heshima kwa viongozi waliouletea mafanikio mchezo huo akiwemo

Manchester City yamkatisha tamaa Wenger

LONDON, Uingereza

ARSENE Wenger juzi alikiri kuwa Arsenal imejiweka mahali pabaya baada ya kufungwa na vinara wa ligi hiyo, Manchester City. Kipigo hicho kimefanya Gunners kupitwa kwa

19 December 2011

Kafulila kaponzwa na ubishi -Mbunge

*Asema amemshauri mara nyingi lakini hakusikia
*Afananisha tukio hilo la kihistoria na 'sikio la kufa'
*NCCR: kumpoteza mbunge gharama, hatuna jinsi
*Kafulila: Nilitokwa machozi kuwakumbuka wananchi

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, NCCR Mageuzi, Bw. David Kafulila, akiingia ndani ya gari lake, kwa ajili ya kuondoka Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana, baada ya kuvuliwa Uanachama.
 Na Rehema Mohamed

SIKU moja baada ya kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya Chama cha NCCR-Mageuzi, kumfukuza uanachama Mbunge wa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislam, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana, wakati akiwahamasisha kuchangia uanzishwaji wa Televisheni ya Kwanza ya Kiislam nchini (TV Iman).

Maliasili yatupiwa lawama ugawaji vitalu

Na Said Njuki

WADAU wa uwindaji wa kitalii wa ndani na nje, wamezidi kuibana Serikali kwa kuituhumu Wizara ya Maliasili na Utalii kumilikisha vitalu vya uwindaji wa
Muuguzi Mkuu wa wa Hospitali ya KCMC Moshi, Bi. Redempta Mamseti, akitoa shukrani kwa Benki ya KCB Tanzania, baada ya kukarabati wodi ya wagonjwa mahututi ‘ICU’. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Moshi Bw Rominyika Saitabau.

Pinda: Tutachukua hatua kulinda viwanda vyetu

*Ahoji iweje juisi itoke nje wakati TZ ina matunda

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema Serikali itachukua hatua za haraka kulinda viwanda vya ndani na kuzalisha bidhaa bora ili kuondoa kasumba ya
Wachezaji wa Barcelona (kutoka kushoto), Lionel Messi (jezi namba 10), Cesc Fabregas na Andre's Iniesta, wakishangilia bao lililofungwa na Fabregas katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyopigwa Uwanja ya Yokohama, Tokyo jana.Barcelona ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Santos mabao 4-0.

Papic 'saluti' kwa Chuji

*Amtaka apunguze uzito

Na Zahoro Mlanzi, aliyekuwa Mlandizi

KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Kostadin Papic ameridhishwa na kiwango cha kiungo wake, Athuman Idd 'Chuji', kwa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Jaffarai akitumbuiza kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya Kampuni ya simu ya
Airtel ijulikanayo kama Airtel Money, mwishoni mwa wiki Uwanja
wa Sokoine, Mbeya.

Manji afungua tawi jipya la Yanga G/Mboto

Na Peter Mwenda

ALIYEKUWA Mfadhili wa Yanga, Yusuph Manji, amefungua tawi jipya la Shumato, Mzambarauni, Gongo la Mboto, Dar es Salaam na kuchangia sh. milioni 5 na kusisitiza yeye ni

Ward amtwanga Fronch kwa pointi

Atlantic City, Marekani

BONDIA Andre Ward amemtwanga mpiganaji kutoka Nottingham, Carl Froch na kutwaa ubingwa wa mashindano ya Super Six, uzani wa super-middle

16 December 2011

Posho zamkera Polycarp Pengo

*Asema Watanzania wataichukia nchini yao, serikali
*Asisitiza kushuka ufaulu kunatokana na elimu duni
*Awataka wananchi kuacha mzaha suala la katiba
*Apongeza uamuzi wa serikali kukataa ushoga


Na Peter Mwenda

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema kitendo cha wabunge kuongezewa posho, kitawafanya

JK Entebe Uganda kuhudhuria mkutano

Rais Jakaya Kikwete (anayepunga mkono), alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Entebe, Nchini Uganda jana, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu, kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia.

MUHAS yatimua wanafunzi

*Wahusishwa na vurugu zilizotokea chuoni

Na Godfrida Jola

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kimewasimamisha masomo wanafunzi 66 kwa muda usiojulikana baada ya kufanya vurugu katika

Mabadiliko ya Tabia ya Nchi

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mhandisi Ladislaus Kyaruzi, akizungumza na waandishi wa habari, (hawako pichani), Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano wa mashirika mawili ya kiraia, TADIP na KAS kuhusu mjadala wa mabadiliko ya tabia Nchi. Kulia ni Mwenyekiti wa Mjadala Bw. Salim Zagar.