04 December 2013

HOFU YA VYETI FEKI SERIKALINI  • WATUMISHI WOTE SASA KUHAKIKIWA VYETI VYAO
  • ASKARI WALIOVITUMIA KUPANDA VYEO KUKIONA

 Na Heri Shaaban
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake wote  kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa uhakiki ili kubaini kama kuna vyeti feki.

MPASUKO ZAIDI CHADEMA

  • M/KITI SINGIDA AJIUZULU, ASEMA HAKUNA DEMOKRASIA


Damiano Mkumbo na Darlin Said

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Singida, Wilfred Kitundu, amejiuzulu rasmi nafasi hiyo akipinga mambuzi ya Kamati Kuu kuwavua nyadhifa za uongozi viongozi wake watatu.

OFISI YA CHADEMA YACHOMWA MOTONa Queen Lema, Arusha
Katika hali isiyo ya kawaida, watu wasiofahamika wamevamia ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya kaskazini iliopo mkoani Arusha na kuichoma moto uliosababisha haraka kubwa.

JK AMTEUA DKT. MIGIRO BUNGENa Mwandishi Wetu

Rais Jakaya Kikwete, amemutea Dkt. Asha-Rose Migiro, kuwa mbunge wa kuteuliwa.Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka, ilisema uteuzi huo umeanza jana.
Kwa sasa Dkt. Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pia amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), baada ya kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja uo, Bw. Ban Ki-Moon, Januari 2007 hadi 2012.

KILI STARS 'MTOTO HATUMWI SOKONI LEO' Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), leo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Burundi katika mechi ya michuano ya Chalenji inayofanyika jijini hapa, ikiwa inawania pointi tatu muhimu ili kujiweka vizuri kucheza robo fainali ya mashindano hayo.

...ZANZIBAR HEROES YAAGA MASHINDANO Na Mwandishi Wetu, Nairobi

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya ya Zanzibar Heroes, jana imetolewa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuzabwa na Kenya 'Harambee Stars' mabao 2-0 kwenye mechi iliyochezwa jana mjini Nakuru.

03 December 2013

ZITTO AKATISHA ZIARA YA SLAA


  • CHADEMA KIGOMA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU

  • HOFU YA KUTOKEA VURUGU YATANDA MAJIMBONI 
Na Mwajabu Kigaza, Kigoma
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Kigoma, kimesitisha ziara ya Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa, Dkt. Wilbrod Slaa, ambayo ilipangwa kufanyika mkoani humo kuanzia Desemba 5 hadi 13 mwaka huu, kutokana na hofu ya usalama miongoni mwa wanachama wake.

LOWASSA ‘AFUNGUKA’ KWA WAUMINIWaziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa (mwenye suti),akiwaaga waumini wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mtandi,Wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,baada ya kuendesha harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo ya Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKU),mwishoni mwa wiki ambapo sh.milioni 103 zilichangwa katika harambee hiyo. Kulia kwake ni Askofu wa Kanisa hilo,Dayosisi ya Newala,Oscar Mnung'a.

  •   ACHANGISHA MILIONI 103/-,AMMWAGIA  SIFA MKAPA

Na Mwandishi Wetu, Masasi
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, amesema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote katika mapambano ya kuondoa umaskini kwenye jamii.

MAGUFULI: SINA HURUMA KWA MATAJIRI WA MAGARIWaziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, amesema ataendelea kusimamia sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973 hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara, anaripoti Goodluck Hongo.

WALIOKUTWA NA MENO YA TEMBO JELA MIAKA 20Watu wawili akiwemo mlinzi wa nyumba moja mkoani Tanga, wamehukumumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kupakua na kuhifadhi meno ya tembo 114 yenye thamani ya sh. milioni 44,044 kinyume cha sheria, anaripoti Mashaka Mhando, Tanga.