06 December 2010

Kanisa Katoliki lafafanua waliotengwa

Na Edmund  Mihale

KANISA Katoliki Jimbo la Sumbawanga limezungumzia sakata la kusimamishwa kwa baadhi ya waumini wa jimbo hilo na kudai kuwa adhabu hiyo ni kawaida kuchukuliwa kwa waumini wanaokwenda kinyume na imani ya kanisa hilo.Hatua hiyo ya kanisa hilo
imekuja baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa limesimamisha waumini 400 ambao ni wanachama wa Chama Cha Mpinduzi (CCM).

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Paroko wa Kanisa Kuu la Sumbawanga, Padri Deogratius Simemba alisema wanachama waliosimamishwa si 400 kama ilivyoripotiwa bali hawazidi na hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu ya kwenda kinyume na maelekezo ya kanisa

Alisema kitendo cha kusimamishwa kwa waumini hao ni cha kawaida katika kanisa hilo katika kusimamia nidhamu kwa waumini wake na si mambo ya kisiasa wala kukichukia chama fulani.

"Kanisa siku zote limekuwa likisisitiza waumini wake kushiriki katika siasa, lakini kwa uadilifu na iwapo litaona muumini anakwenda kinyume na maelekezo ya kanisa humchukulia hatua kwa mujibu wa sheria za kanisa," alisema Padre Simemba.

Alisema wanachama hao wamesimamishwa kutoka na kuvunja sheria za kanisa kwa kuukufuru utatu mtakatifu yaani Mungu Mwana wa Mungu Baba na Roho Mtakatifu .

Gazeti moja la kila siku liliripoti jana akuwa utatu huo mtakatifu ulifananishwa na 'mafiga matatu ya CCM, ambapo mgombea urais, Rais Kikwete alifananishwa na Mungu, Mgombea ubunge alifananishwa na Yesu Kristo na wagombea udiwani wakalinganishwa na Roho Mtakatifu.

Padri alisema kosa lingine la waumini ni kushangilia ushindi wa mbunge wa jimbo kwa kutumia msalaba jambo ambalo ni kosa kutoka na sheria na kanuni za kanisa hilo.

Alisema kuwa kanisa limekuwa likitoa adhabu kwa waumini wake wanaofanya makosa mbalimbali, yakiwemo kushiriki katika imani za kishirikina na wote wanaokwenda kinyume na sheria za kainisa.

Naye msemaji wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Modestus Katonto alisema watu wanataka kulichukulia suala hilo kisiasa, wakati ni la kiimani.Alisema anavyofahamu yeye watu waliotengwa na kanisa hilo hawazidi 10, miongoni mwao wakiwamo wanane waliokufuru msalaba ambao walikuwa wakikimbia na msalaba kushangilia ushindi wa mgombea wa CCM huku wakisema kanisa limezikwa na msalaba.

"Wengine hawajatengwa na kanisa, lakini wamepewa barua kwenda kuomba msamaha katika ngazi ya Jumuiya, wakisamehewa na jumuiya wataendelea kushiriki kama kawaida," alisema.

27 comments:

  1. Ama kwa hakika kitendo walichofanya waumini hao ni kumkufuru Mungu mbaya zaidi kuwashangilia wagombea wa CCM chama kilichofilisika uwezo katika utendaji kutokana na ufisadi. Aheri wangekua wanashabikia chama chochote cha upinzani wangeweza kufikiriwa msamaha. Viva Baba Paroko unajali maslahi ya nchi hii.

    ReplyDelete
  2. HAPA INAJULIKANA WAZI KABISA KTK WARAKA WA KANISA JUU YA UCHAGUZI UMESEMA WAZI NI NANI WA KUMCHAGUWA, ISITAFUTE VISINGIZIO UKWELI NI HUOHUO KUWA WAMEWAFUKUZA KWA KUWA WAMEMCHAGUA ASIE KUWA MWENZAO

    ReplyDelete
  3. Hata wakijaribu kujikomba hao viongozi wa kanisa ni wanafiki. Kwa nini wao walitumia jina la mungu kuleta mambo ya waraka wa kisiasa. Wangetumia msalaba kuwashangilia Chadema kama kanisa lao lilivyotumia msalaba kushangilia chadema kusingekua na tatizo!!

    ReplyDelete
  4. akili ndogo sana....

    dunia ikijua kitendo hiki itatucheka sana, kwanza itawacheka wakristo watz kuwa hawajui kutofautisha misingi ya imani yao (Mungu baba, mwana na roho mtakatifu kiasi cha kuwafananisha na wanasiasa...

    kweli waliofanya hivi ni watu wenye vichwa vidogi sana hata hawastahili kujadiliwa...

    Hilo kanisa linalotenga watu saa hizi kwa mbinu hizi pia limepitwa na wakati..., sasa tunashindwa kutofautisha... waliokufuru wamethibitisha udhaufu mkubwa, wanaowatenga nao hukohuko - wanathibitisha udhaifu mkubwa tena... hakuna wa kuoingoza mwingine...,

    wakati wa "kuadhibu" - "kuchapa" wakristo umekwisha pita na wakati. Ikiwa waliyemkufuru anawahurumia na anawasubiri watubu maana sifa yake ni huruma, ni nani tena anaweza kuwachapa, au sijui kuwaadhibu...

    Mtaji wa maparoko wetu ni ujinga wetu. Kuna siku hawa waliotengwa watagundua kuwa unaweza kutengwa lakini usitengeke.... ngoja wakatoliki wale sangara vizuri wawe na akili "ubabe" wa kanisa utakwisha" - Tunakuwa wababe kwa jina la mungu mwenye huruma hivi jamani??

    Mimi huyo Mungu wa maadhabu hivyo wala sumhitaji...

    Nafikiri huyo Mbunge anahitaji kufundishwa tu na wale wote waliofanya hayo makufuru... wafundishwe.. watunzwe... na kanisa liache vitu vya aibu...

    Ikiwa ni kweli kuwa mheshimiwa mbuge alijifananisha na Yesu na wala hatokei kukanusha matamshi haya... atakua anathibitisha kuwa yeye ni mtu mwenye utashi mdogo sana... maana anaumiza nafsi za wananchi wakristo, hata kama yeye sio muumini, au mkristo.

    Kanisa ondoeni aibu huku jamani....uuuuuuuuwwwwwwiiii!!!

    ReplyDelete
  5. Wakatoliki wanaondelea kuchapwa na kuadhibiwa ni wa afrika na amerika ya kusini tuu... ambako pia biashara utumwa ilitawala wakati ule...

    Huu ni uonevu sana... niaminivyo, hata Rome hakuna mtu utamtisha tena eti tunakutenga, atisheke,

    ReplyDelete
  6. Acheni nyumba ilinde familia yake. wanaosema wameonewa sio solution na haina mantiki. Kutokana na ujumbe uliopo ni wa kukufuru kuingilia imani na siasa. Huu ujumbe kusema kweli haukuwa mzuri. Ina maana mpaka kanisa kuingilia haya mambo, siasa iliingia mpaka kwenye jumuia na jamii haikurizika na jambo hilo.

    ReplyDelete
  7. ACHENI MASUALA YA KIKATOLIKI YAAMULIWE NA WAKATOLIKI WENYEWE, NI KANISA LENYE MSIMAMO NA LISILOYUMBISHWA KWA NAMNA YOYOTE ILE.

    ReplyDelete
  8. Je, ingetokea mkristu akamfananisha JK na Mtume Muhammad tungelala? Si ingekuwa kama Iran na Iraq? Je mnamkumbuka mwandishi wa vitabu ambaye mpaka sasa anatafutwa kuuawa? mambo yote fanyeni lakini tusichokoze imani za watu. hii inakwenda mbali ya Siasa.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu weee achatu yetu macho. Afadhali wakristo ni wavumilivu lakini hao akina nanihiiii......mh. Hiyo ni ngoma zito kwanza uelewa. Ungekuta shingo zao zimeshawikwa juu ya magogo kama mbuzi.

    ReplyDelete
  10. WENYE UWEZO WAKUELEWA MAMBO WATAELEWA, NAWENYE UWEZO FINYU WA KUELEWA MABO WATAENDELE KUANDIKA MAWAZO YASIYO SAHIHI. KAMA KANISA LIMECHUKUA MAAMUZI NIKWAKANISA NASI KWA CCM. MAPADRE NA WAUMINI WAKANISA KATOLIKI MMEFANYA VIZURI NA HINGERENI KUUTETEA UKRISTU WENU BIALAKUJALI KELELE ZA WASIOFAHAMU IMANI YENU, NA MKIONA MTU KATOA MAONI YA KUKASHFU WALA MSITETELEKE HAO NIWALEWASIOJUA HATA ISHARA YA MSALABA NAHIVYO KWAO KUKIMBIANA MSALABA HUKU WAKISHANGILIA USHINDI NIALAMA MOJAWAPOYA KULIFEDHEHESHA KANISA KATOLIKINA KUJIPATIA UMAARUFU WA MAKANISA YAO. NAWAPONGEA SANA KWA KUWA IMARA KIIMANI. NAHAO WAUMINI WAACHENI WANDELEE NA USALITI KAMA WATATUBU SAWA WASIPOYUBU NA WAENDE KWENYE MAHALI AMBAPO MWABUDU MUNGU WAO MLANGO UKO WAZI NENDENI NA MKITOKA MTUFUNGIE MLANGO.

    ReplyDelete
  11. Shetani akikosa wa kumtukana basi humtukana hata mama yake,samahani ndugu zangu wachangiaji sijui kama ntakosea nikisema hao waliowafananisha viongozi wa siasa ,wakafanya kama MIUNGU wao hawatafautiani na MASHETANI,tuwe makini imani si kitu cha kuchezea mkakifananisha na WANASIASA WEZI,ndugu yangu uliyesema wakristu wanauvumilivu,nakuhakikishia uvumilivu unamwisho,kuna siku hiyo nchi tutagawana vipande nyie tulieni tu mtaona siku moja

    ReplyDelete
  12. Eeh walie kina nani? Ngoma ya watu wa imani nyingine hamuiwezi wala hata msijifarague hao imani yao haichezewi. Na waswahili wanasema ukicheza na mbwa atakufuata mpaka msikitini, na hayo ndio matokeo ya kanisa katoliki kujiingiza lenyewe kwenye siasa kwa kuandaa waraka wa uchaguzi. Walitegemea watavuna nini? Hivi mlikwishawahi kusikia wa upande wa pili hata siku moja wanamshirikisha mungu kwenye mambo ya siasa? Mmeyataka wenyewe mara chaguo la Mungu mara sijui Mungu kafanya nini, acheni mvune mlichokipanda sasa, na hao waliosimamishwa wameonewa kwa maana kama kanisa lisingejiingiza kwenye kuamrisha watu kuwachagua watu kwa imani zao na kuandika sijui mawaraka na kuanza kutuma ujumbe wa sms watu wangeliheshimu kanisa na wasingelishirikisha kwenye mambo ya siasa. Haya sasa kaeni kimya mshavuka nguo chutameni chini, hakuna haja ya kusimama wima ilhali hamna nguo maungoni!

    ReplyDelete
  13. Jammaa!!!!!!! na huyu chizi katokea upande gani tena. Hivi ameweka muziki, taarabu au kilevi aina gani? Mbona simwelewi. Samahani rudia tena umeenda mno speed, punguza mwendo kidogo.

    ReplyDelete
  14. watanzania tusome na kufanya utafiti! siyo kuchangia tu kama mbayuwayu changanyeni na zenu! ya wakatoliki tuwaachie wenyewe!

    ReplyDelete
  15. Ni kitu chepesi kabisa, ambae analaumu waraka ni aidha hajausoma na kama kausoma hakuuelewa, na kama hakuulelewa licha ya kueleweshwa ana matatizo ya uelewa.
    Ukisema Mgombea ni sawa na Mungu ama kufananisha na kitu chochote kitakatifu basi ni kufuru ya wazi. Haihitaji uelewa wowote. Mbona Chama Kimoja kimejikita zanzbar na Pwani ambako wenyewe mwaelewa hawaitwi hivyo. Tanzania ni yetu, mafisadi na wachawi wao wako kwenye siasa.
    Kama mmoja alijaribu tu kuchora katuni ya mtume mtakatifu dunia nzima ilisimama, pia jamaa mmoja alitaka kuchoka kitabu kitakatifu dunia ilitetemeka. Je anayefananisha Mungu na Mwanadamu? na Vyeo vya kibinadamu? Tanzania ilitakiwa kusimama na kutetemeka kwa hofu kabisa

    ReplyDelete
  16. Kama sheria ya kanisa imeamua hivyo kutokana wa kanuni na taratibu waacheni wenye mamlaka ya kanisa watimize wajibu wao. wao waliofungiwa ndio wakalalamike acheni kusemea mambo ya watu . usilo lijua ni kama usiku wa giza

    ReplyDelete
  17. Kwanza tuambieni kanisa lilitoa mwongozo gani maana kuna waraka wa kanisa tumeuona unasema Wkristo wamchague Slaa,mimi ninayo moja,kisha tujadili mada. Mimi nadhani wa kuadhibiwa kwanza alikuwa Dr Slaa kutokana na kuzini na mke wa mtu,na baadaye kukiri kuwa hakufahamu lakini hata baada ya kufahamu aliendelea kuzini na kutembea naye,sasa mnaidhalilisha dini kwa kukemea baadhi ya maovu yanayoendana kinyume na maslahi yenu binafsi badala ya dini, na maovu yale ambayo yanafanywa na mtu mumtakaye hamuyakemei,hatushangai kwa sababu tumeshuhudia mapadri wakiozesha wasenge,wakishiriki katika mauaji ya halaiki Ruanda,sasa hakuna cha kushangaa hapa. Wapo mapadri ambao ni mashetani wamevaa majoho ya upadri kama hao niliowataja hapo juu. iweje usimuadhibu mzinifu umuadhibu aliyekataa kuchaguliwa kiongozi na kanisa?

    ReplyDelete
  18. TATIZO HALIKO WAZI HALITAKI KUSEMA LILITOA AGIZO GANI KWA WAKRISTO,SASA WACHENI WATU WASEME YAO. NYIE MNAOSEMA KANISA LINA SHERIA ZAKE,HEBU TUAMBIENI SHERIA INAYOMHUSU SLAA (1) KUACHA MKE, NA SHERIA YA KIKRISTO INASEMAJE KUHUSU HILO (2) UZINZI NA MKE WA MTU SHERIA INASEMAJE? MSIKURUPUKIE WAISLAM,DINI YA KIISLAM INAONGOZWA NA SHERIA ISIYOBADILIKA WALA HAINA CCM,CHADEMA WALA CUF,HAKUNA SHERIA KATIKA DINI YA KIISLAMU INAYOENDANA NA MATUKIO.UCHAGUZI NI TUKIO SASA KAMA KANISA LILIAGIZA WAUMIMNI WAMPIGIE MZINIFU NA WAAMINI HAWAKUKUBALIANA NA HILO,KOSA LIKO WAPI? IPO KITU KANISA LINAFICHA LAKINI SASA WANASEMA WALIKIMBIZA GENEZA LIKIWA NA MSALABA,HAYO YAMEFANYWA SUMBAWANGA TU. UKANDAMIZAJI WA AINA YOYOTE UNAONDOKA DUNIA HII KUTOKANA NA WATU KUWA NA UELEWA MKUBWA NA KUHOJI MAMBO MBALIMBALI

    ReplyDelete
  19. KAMA SUALA NI LA KIKANISA NINYI VIONGOZI WA KIDINI KWA NINI MNAINGIA MJADALA YA KISIASA. NADHANI HAMNA HATA HAJA YA KUJADILIANA NA WANA SIASA HAO WALA WAANDISHI WA HABARI. KAMA NI WATU KUFUNGIWA HUDUMA ZA KANISA HAWA SI WA KWANZA. ENDELEENI NA UTARATIBU WENU BILA KUINGILIWA. TAFSIRI KILA MTU ATOE YA KWAKE, UKWELI UNABAKI PALEPALE. PILI KAMA HAO WALIOFUNGIWA WANAONA KANISA NIMEWANYIMA HAKI BASI WAINGIE KATIKA DINI NYINGINE. NA KAMA VYAMA VYA SIASA VINAKUWA DINI BASI WAENDE HUKO WASILETE FUJO KANISANI. TENGENISHENI MISINGI NA MAAMUZI YA KIDINI NA SIASA. PUNTO.

    ReplyDelete
  20. HAWAWEZI KUTENGA KAMA UNAVYOSEMA KWA SABABU WAPO KWENYE SIASA SIKU NYINGI HAYA NI MAENDELEZO TU? WEWE UNAYESEMA UKO ROME TUAMBIE KANISA LINARUHUSU MZINIFU KUPATA SAPOTI YA KANISA AWE KIONGOZI? KWA NINI KANISA HALIKUWA MSTARI WA MBELE KUMKEMEA HUYO WALIOKUWA WANAMTAKA AACHANE NA HUYO MWANAMKE NA ATUBU BADALA YAKE WAMEKUWA WAKIMPA SAPOTI YA HALI YA JUU. KANISA LA KATOLIKI LIMEKUMBWA NA KASHFA NYINGI AMBAZO ZINGEKEMEWA MAPEMA HALI ISINGEFIKA HAPO ILIPO. SASA HATA HUKO SUMBAWANGA HAKUNA MASUALA YA DINI HUKO KUNA SIASA KWENYE MGONGO WA DINI,HATA UKIWAFUKUZA HAITASAIDIA. HUYO PADRI NI SHETANI NA HUKO ROME KAMA MNASAPOTI MASHETANI MTASHUHUDIA MAPADRI WAKIENDELEA KULAWITI WATOTO WADOGO,KUOZESHA WASENGE NA MENGINEYO MENGI. MSITUHARIBIE NCHI YETU. SISI HAPA TULIKUWA TUNACHAGUA RAIS WA TANZANIA NA NYIE HUKO ROME HUWA MNACHAGUA POPE AMBAYE SHARTI LAZIMA AWE MKRISTO NA MKATOLIKI

    ReplyDelete
  21. suala si ukatoliki wala nini ila ni kuangalia hali halisi. na unapokimbilia katika uzinzi nani ambaye unamfahamu wewe kati alisiye na dosari... Pili mbona uzinzi huo mmeuona baada tu ya uchaguzi na sassa kimyaaa. kama mnataka kujenga hiyo mnayoita nchi yenu hamnabudi kuwa na mipango endelevu kiuchumi, kimaadili na kisiasa. vinginevyo ulevi wenu huo wa udini utawafikisha pabaya ilhali mkilazimisha kutafuta mchawi mahali asipokuwepo. NINYI "WATANZANIA" WAKATI UMEFIKA WA KUFUNGUA MACHO NA KUSHUGHULIKIA MAMBO YA MUHIMU KULIKO KUNG'ANG'ANIA VIJIMAMBO TU.

    ReplyDelete
  22. WEWE WA ROME UNASIKITISHA SANA KWA SABABU HUTUELEZI KWA NINI MZINZI ASICHUKULIWE HATUA NA KANISA ILHALI ANAYESHABIKIA SIASA NDIO ANAYECHUKULIWA HATUA? MTU ANAKIRI MWENYEWE KAMA HAKUWA ANAJUA KUWA HUYO NI MKE WA MTU NA BAADA YAKUJUA BADO ANAENDELEA NAYE,KWA NINI KANISA HALIKEMEI HILI? NDIO MAANA HATA WALE MAPADRI WALIOKUWA WANALAWITI WATOTO WADOGO WALIKUWA WANAFAHAMIKA NA HAWAKUKEMEWA MPAKA PALE AIBU ILIPOTOKA NJE NDIO KANISA LINAOMBA MSAMAHA KWA WALIOATHIRIKA. HOJA YETU NI KWAMBA KWA NINI KANISA LINACHAGUA MAOVU YA KUKEMEA? NA HATA WEWE NI MMOJA WAPO MLIOKUWA MMETAYARISHA WARAKA WA KANISA WA KUMCHAGUA PADRI MWENZENU,SISI HUKU HATUTAKI MAMBO HAYO YA UDINI,NDIO TUFUMBUE MACHO NI SAWA KABISA LAKINI PIA TUANGALIE MASLAHI YA NCHI YETU NA VIZAZI VYETU VIJAVYO NA TUKIANZA KUKAA MAKANISANI NA MISIKITINI KUWAAMBIA WAUMINI TUMCHAGUE FULANI KWA SABABU YA DINI YAKE,HILO NI DHAMBI NA USHETANI MKUBWA AMBAO HAUSAMEHEKI. HATA KELELE ZA UFISADI ZINATIA SHAKA SANA MAANA UFISADI ULIOMALIZA NCHI YETU HAUKUWA WAKATI WA KIKWETE, UMELELEWA NA KUKUZWA NA AWAMU NYINGINE ILIYOPITA. MACHO TUNAYOFUNGUA NI KWA HIYO VIJIMAMBO UNAVYOVISEMA KWETU SISI SI VIJIMAMBO NI MAMBO MAKUBWA SANA NA YANAANGAMIZA TAIFA. KWA HIYO NDUGU YANGU TANZANIA HAINA ULEVI WA UDINI ILA WANASIASA WALITAKA KUWATUMIA VIONGOZI WA DINI KUFIKIA MALENGO YAO NA IMESHINDIKANA KUTOKANA NA MALEZI BORA YA BABA WA TAIFA MAREHEMU NYERERE SASA HASIRA ZAO WANAZIPELEKA KWA WAFUASI WA CHAMA FULANI TU. NI AIBU SANA. BADO NASEMA HUYO PADRI NI SHETANI NA KAMA KATUMWA KUTOKA ROME SIAMINI HILO

    ReplyDelete
  23. Huyu jamaa anayempinga wa Roma inaonekana sio serious na ni mshabiki tu wa siasa na hasa ccm.
    Sina tatizo na ukerekekwa wake wa ccm, tatizo ni kwamba hana hoja, kelele, uwongo na umbeya. Eti Kanisa Katoliki lilitoa waraka kuamrisha waamini wamchague Dr. Slaa. Ni ujinga tu kwani hajausoma na amesikia MAFISADI wanalopoka hivyo naye anafuat mkumbo. Jamani tutakuwa lini huru kiakili?????? Atoe waraka huo anaosema ni wa kanisa. Lakini namshauri huyu jamaa achukue muda kuisoma katiba ya nchi yetu,na aende wizara ya mambo ya ndani apate nakala ya vyama visivo vya kiserikali na dini. Halafu asome vizuri sheria za Kanisa Katoliki.
    Najua hawezi kusoma hata moja ya hizo document kwani ni mvivu na UJINGA hauta mwacha kamwe kwani ataendelea kuropoka tu na kufuata mkumbo.
    MMMMHHHHH ujinga gharama!!!!!!!!Ka kimya usijiaibishe na umri huo, watoto wakijua kuwa hayo ni maoni yako, maujiko yako yote garasha!!

    ReplyDelete
  24. Mnaosema kanisa katoliki lilitoa waraka kumchagua Dr. Slaa ni WAONGO WA MCHANA KWEPEEE. Mi c muumini wa katoliki wala na sipendi ukatoliki lakini ninachokijua wakatoliki walitoa waraka kuwaelimisha aina ya kiongozi bora anayetakiwa kuchaguliwa ili nchi ipate uongozi bora na maendeleo bila kujali huyo kiongozi atatoka CCM, CHADEMA, TLP nk. Pia bila kujali ni mkristo, muislamu au mpagani.

    Tatizo lilikuja pale ambapo sifa hizo zote nzuri za kiongozi bora zilikuwa zinamwangukia Dr Slaa na hapo ndo wanasiasa wakaanza kuwadanganya wenzetu waislamu ambao kwa kawaida wakitajiwa swala lolote la dini hawana uwezo wa kufikiria ipasavyo zaidi ya kuegemea dini yao kuwa Dr. Slaa ni wa wakristo. Ni waislamu wachache sana ambao huwezi kuwanasa kwa mtego wa dini tofauti na imani zingine za dini. Kundi la pili walionaswa na huo uzushi ni makasuku au mashabiki wa CCM ambao hawatafakari kujua ukweli ila wanaendelea kuimba wimbo wowote utakaoonekana unawaumiza wapinzani wao.
    Waraka waliotoa wakatoliki ni elimu nzuri sana kwa wapiga kura ila ukazuiwa na watu wasiotakia mema nchi yetu hasa viongozi wa CCM na CUF walioona sifa hizo zinamwangukia mpizani wao Dr. Slaa.
    Waliojinufanisha kidini uchaguzi wa mwaka huu ni CCM na CUF waliotumia udini kuwazuia waislamu wasimchague Dr. Slaa ili wapate kura na kwa vile wote ni waislamu wakawashawishi viongozi wa kiislamu ambao ni rahisi sana kuwashawishi kumkampenia mgombea muislamu kuwapigia kampeni misikitini.

    ReplyDelete
  25. Hamna jipya nyie wawili mliotoa maoni,naomba majibu ya Kanisa kutomfukuza au kumkemea mzinifu badala yake wanafukuza wanaoshabikia chama cha siasa. Ninachosema kanisa halina haki ya kuchagua ovu lipi likemewe na lipi likemewe,inatakiwa ikemee maovu yote siyo kuchagua. mimi ninao waraka na sijataja ni wa kanisa gani,wala sina ujinga wa kujadili habari ya uchaguzi sasa hivi kwani umeshapita na mshindi kishapatikana. Mliolificha sasa linaonekana. Usinizungumzie wimbo wa mafisadi nimeishachoka nao na walioliachia mpaka likaimaliza nchi wako nje ya utawala huku wakipewa heshima kubwa na makanisa. Na nimeisha eleza msimamo wangu Tanzania tunakuwa na uchaguzi wa Rais wa nchi yetu na Vatican wanakuwa na uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa dini na pale lazima awe Mkatoliki na Mkristo,hili sina haja ya kulirudia na kama kuna Mtanzania alikaa msikitini ama kanisani na akaamuru waumini wake wamchague mtu kutokana na dini yake huyo ni shetani kama alivyo Padri wa Sumbawanga,sasa wewe uliyeniita mimi mjinga nakuomba utafakari kati ya mimi na wewe nani mjinga,mimi ni mzalendo kwa nchi yangu na nimelelewa kuchukia udini na ukabila na ninawaambie hamnigeuzi kwa hilo.

    ReplyDelete
  26. we koma kuwatukana Waislam kwa kuwaambia hawana uwezo wa kufikiri.ujinga huo ndio mgando wa mawazo mlio nao,hayo yameisha pitwa na wakati, tunasoma vyuoni pamoja na tukibanwa huku tunakwenda vyuo vya binfsi,kila kitu kinakwenda kwa msukumo na msukumo wa nyinyi kusoma unaeleweka na hicho ndicho kinachowafanya kuwa na hofu pale Muislam anaposhika madaraka makubwa kwenye nchi. hamna domination tena na huko mbele tuendako hali itawawia ngumu zaidi hamna atakayekubali kukandamizwa

    ReplyDelete
  27. Ukurasa huu usiwe na lengo la kuwagawa watu kwa misingi ya kidini. Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuchangia kwenye mada ambayo kuchangia kwake kutawafanya Watanzania wagawanyike kwa misingi ya kidini. Ukurasa huu usije ukaonekana kama ukumbi wa walevi na ndivyo unavyoweza kuonekana sasa. Jengeni hoja badala ya matusi.

    ReplyDelete