LONDON, Uingereza
ARSENE Wenger juzi alikiri kuwa Arsenal imejiweka mahali pabaya baada ya kufungwa na vinara wa ligi hiyo, Manchester City. Kipigo hicho kimefanya Gunners kupitwa kwa
pointi 12 na City ingawa bado zimebakia mechi 22 kabla ya Ligi Kuu kuisha, wakuu wa Emirates wanajua kuwa kuna tofauti kubwa ya pointi.
Wenger alisema kuwa timu yake ingeweza kukaa kwenye njia nzuri kwa kuifunga timu ya Roberto Mancini.
Lakini badala yake ilipata kipigo kwa kufungwa bao 1-0 kwa lililowekwa kimiani na David Silva na kuwa na mlima wa kupanda.
Wenger alisema: "kwa wakati huu itakuwa ngumu kuwakaribia City.
"Bahati mbaya, ni mchezo ambao hatukutakiwa kuupoteza kwa kuwa ulitufanya tuwe nyuma zaidi ya City.
"Kama tungeshinda ingetufanya tupitwe pointi sita na walinzi wetu pembeni Jack Wilshere na Abou Diaby wanarejea.
"Tutakuwa na kikosi kizuri katika mzunguko wa pili wa msimu."
Wenger amesema kuwa timu yake inakuwa na mabadiliko makubwa baada ya kuanza vibaya msimu wa Agosti, mwaka huu na kuongeza kuwa kwa kufungwa ina maana wanatakiwa kujituma zaidi na pia ana matumaini timu itafikia malengo yake.
Alisema katika mechi ya juzi walinzi Koscielny, Djourou na Vermaelen walicheza vizuri lakini walikuwa tatizo katika sehemu ya ulinzi ya katikati.
No comments:
Post a Comment