Atlantic City, Marekani
BONDIA Andre Ward amemtwanga mpiganaji kutoka Nottingham, Carl Froch na kutwaa ubingwa wa mashindano ya Super Six, uzani wa super-middle
mjini City, Atlantic Marekani.
Ward ambaye bondia wa Marekani, alikuwa mwepezi kumshambulia mpinzani wake wa Uingereza, kwa kupiga ngumi kali na kuweza kumaliza nguvu Froch.
Bondia huyo ametwa mkanda wa Froch wa WBC na kuungananisha na wa WBA aliokuwa nao, alishinda kwa pointi ambapo majaji wote watatu walimpatia alama.
"Sikuweza kupata chochote, alikuwa akitereza," alisema Froch.
Nilikuwa na hisia kuwa ningeweza kumtwanga Andre Ward.Ninatakiwa kufanyia kazi baadhi ya mambo ya kiufundi, lakini kuna mapambano mengine yanakuja. "
Kwa upande wa Ward, alisema anahisi kasi yake ilikuwa ni kupata ushindi wake.
"Nilishtushwa kwa jinsi Froch alikuwa akipigana taratibu. Niliweza kumtwanga ngumi," alisema Ward, ambaye alitwaa ubingwa wa Olimpiki 2004.
Froch mwenye miaka 34 kwa sasa rekodi yake imeshuka ameshinda mapambano 29 na kupigwa mawili na mweleekeo wake wa kupigana haujulikani.
Anaweza kuchagua kupigana na Mikkel Kessler wa Denmark, ambaye aliwahi kumtwanga katika hatu za awali za mashindano ya Super Six mwaka 2010, au kupigana na Bute.
Kwa kupigwa Froch, ina maana kuwa wapiganaji wa Uingereza wamepoteza mikanda 10 ya dunia katika mechi
12 kwa mwaka 2011, wakimwacha Cleverly akibakia kuwa bingwa pekee.
No comments:
Post a Comment