LONDON, England
CHAMA cha Mpira wa Miguu England (FA), kimfungia kucheza mechi moja na faini ya pauni 20,000, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez kutokana na
kumtia hatiani kwa kuwaonesha ishara mbaya mashabiki wa Fulham, baada ya timu yake ya Liverpool kupoteza mechi ya Ligi Kuu mapema mwezi huu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza Reuters, pia Klabu ya Liverpool imelimwa faini ya pauni 20,000 na huku FA ikiwaonya kuhusu tabia hiyo baada ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi Kevin Friend.
Mwamuzi huyo alimtoa nje kwa kadi nyekundu Jay Spearing, katika kipindi cha pili cha mechi hiyo iliyofanyika Desemba 5 mwaka huu na Fulham, wakaibuka washindi kwa 1-0.
Wiki iliyopita FA ilimfungia Suarez, kucheza mechi nane na kutozwa faini ya pauni 40,000 baada ya kupatikana na hatia ya kumtolea maneno ya kibaguzi beki wa Manchester United, Patrice Evra.
Pamoja na kukata rufani kupinga maamuzi hayo, ili aweze kucheza mechi ya Ligi Kuu kati Liverpool na Newcastle United, itakayofanyika baadaye leo lakini kutokana na adhabu hiyo, atalazimika kukaa nje.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia tovuti ya FA, ilieleza kwamba Liverpool, imepigwa faini na kuonywa kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake.
No comments:
Post a Comment