03 December 2010

Wabunge CHADEMA wamshtaki Zitto

*Waitaka Kamati Kuu imuhoji kwa kukiuka maamuzi
*Wamo pia wengine 9 waliokacha ufunguzi bunge


Na Edmund Mihale

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameiandikia barua Kamati Kuu ya chama hicho kuiomba imuite Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe na wabunge wengine tisa ili wajieleze kwa nini walikiuka maamuzi halali ya
vikao.

Hatua hiyo imetokana na kitendo cha Bw. Kabwe na wenzake kutoingia bungeni Novemba 18, mwaka huu ambapo wabunge hao walikuwa wameafikiana kwa kura, kuwa watoke nje ya ukumbi wa bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akizindua bunge.Pamoja na makubaliano hayo, Bw. Zitto ambaye ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni na wabunge hao hawakuingia bungeni.

Wengine ambao hawakuonekana siku hiyo ni Bw. Said Arfi (Mpanda Mjini) ambaye ni Makamu Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Mhonga Luhwanya (Viti Maalum), Bw. John Shibuda (Maswa Magharibi), Bi. Maulida Komu (Viti Maalum), Profesa Kulikoyele Kahingi,(Bukombe), Bi. Rachel Mashishanga (Viti Maalum), Bi. Raya Ibrahimu (Viti Maalum), Bi. Lucy Owenya (Viti Maalum) na Bi. Suzan Lyimo(Viti Maalum).

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Mnadhimu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani bungeni, Bw Tundu Lisu alisema kuwa Bw. Zitto amendikiwa barua mbili tofauti na wabunge wengine kutokana na kitendo hicho.

"Zitto kama Zitto ameandikiwa barua mbili, moja ikiwa ya kitendo cha kushindwa kuingia bungeni jambo ambalo tuliamua katika kikao ambacho hata yeye alikuwepo."Barua hiyo iko tayari lakini ninachojua kuwa yuko Ughaibuni na sijui kama amerudi kwa kuwa alinitumia ujumbe mfupi wa simu kuwa anakwenda Malaysia lakini hajaniambia kuwa amerudi. Kusema kuwa yuko hapa nchini ndiyo sasa unaniambia," alisema Bw. Lissu.

Alisema kuwa barua ya pili imeandikwa kwenda Kamati Kuu na wataitwa na kutoa maelezo mbele ya kamati hiyo. "Kwa kanuni za Katiba ya CHADEMA, Kamati Kuu ndiyo yenye uamuzi wa mwisho ama kumpuuza kama itaona jambo hilo halina uzito, au kama lina uzito itaunda tume kuchunguza tuhuma hizo na iwapo itabainika itachukua hatua," alisema Bw. Lissu.

Alisema kosa lingine la Bw. Zitto ni kitendo cha kuwapigia simu baadhi ya wabunge kuwataka kutoka nje ya kikao kilichoitishwa na chama hicho baada ya kutoka bungeni, akiwataka kutoka katika kikao hicho na kumfuata aliko, jambo lililokera wabunge hao, hivyo kutoa taarifa katika kikao.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw Zitto alisema hadi sasa hajapata barua yoyote, na kuwa hizo ni habari za mitaani kwa kuwa hakukuwa na kikao chochote klichoketi ili kujadili suala hilo.

Alisema yeye ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Naibu Katibu Mkuu na pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, hivyo alipaswa kujua hayo yote."Hizi ni habari za mitaani, mimi sijapata barua yoyotem niliyoandikiwa na CHADEMA," alisema Bw. Zitto. 

40 comments:

  1. Endeleeni kuvurugana wenyewe kwa wenyewe tu. Hii haihitaji kwenda shule, kwamba mmeshaonekana threat kwa upande fulani sasa principle ya devide and rule inatumika bila nyie wenyewe kujua.

    ReplyDelete
  2. kutokuingia bungeni kabisa ni jambo moja na kuingia na kutoka wakati rais anahutubia bunge ni jambo jingine. lazima maswala hayo mawili yatofautishwe. hoja ingekua vinginevyo kama mbunge aliingia bungeni na baadae akagoma kutoka nje kama walivyokubaliana katika kikao. si mara ya kwanza kwa wabunge wa chadema kutokuhudhuria vikao vya bunge kwa sababu mbalimbali na bado uongozi wa chama haujawahi kuwachukulia hatua za kutaka kujieleza. naona hapo mmepotoka katika hoja.

    ReplyDelete
  3. Aliyepotoka ni wewe kwani inaonekana haujaelewa dhima nzima ya wao kutoka nje ya bunge wakati Jk anahutubia,pale kulikua bna meseji nzito kwa JK na dunia yote.Sasa tatizo liko kwa wale wabunge wahuni/Mamluki kama zito na Shibuda kutokuingia mjengoni siku hiyo kwa kuwaogopa kuonekana na mafisadi wanyimwe pumzi.

    hivi mtu kama Owenya aliyezawadiwa ubunge na Ndesamburo naye anapata wapi jeuri ya kukaidi uamuzi wa Chama?

    Kwa mtu kama Zito,sisi tunajua wazi kwamba yeye ni mamluki wa Chama kingine na yuklo CHADEMA ili kuibomoa na si kuijenga.

    ReplyDelete
  4. hivi nyie wanasiasa mnayo kweli nia ya dhati ya kutumikia wananchi.mbona siwaelewi kabisa na mambo yenu

    ReplyDelete
  5. MH zitto tunakomba sana tena sana kama unahisi huna umuhim wa kuendelea na CHADEMA ni vyema tu ukaacha chama na kufanya uonalo ni jema.sijaona sababu ya wewe kwenda kwenye baadhi ya magazeti na kusema ndani ya CHADEMA kuna udini.UKiambiwa uthibitishe hilo utaweza? Tabia hiyo si nzuri hasa kwa mtu uliekomaa kisiasa kama wewe. Plz we kama unaona CHADEMA haikufai nenda huko kwema.
    KINGINE:Huu ni mfano katika kukusaidia wewe inaonekana ushajiona star,THIERY HENRY alipokua Arsenal ilikua ikitokea hachezi basi ni masikitiko kwa club lakin alipoenda barcelona hadi bench alikua anasugua.TAFAKARI CHUKUA HATUA.

    ReplyDelete
  6. Mwenyekiti wa chama cha chadema waite wabunge wako wote mkae mjadili na mpate hatima kwanini hawa wabunge wengune hawakufika kabisa bungenni? wakati mlikubaliana kwa kauli moja ya kutoka nje wakt wa Jk akihutubia na kama ilivyo kawaida katika upigaji kura wanasema wengine wape? Kwa hoyo haikiwa na haja zitto kutoka kufika kabisa mjengoni.

    Basi huo zito angefika bungeni na wabunge wenzake wenzke wanavyotoka yeye angebaki humohumo ionekana wazi kuwa yeye ni kibaraka wa CCM.

    Mbowe fanya kweli Mkuu la sivyo mtabki mkilumbnana na kuleta mgogoro ndani ya chama. Msituangushe tunawapenda sanaaaaa chadema

    ReplyDelete
  7. Mimi naona Mh. Zito toka alipozibwa mdomo wakati wa Buzwagi amekuwa kibalaka wa CCM kwani toka kipindi hicho hajaleta lamaana kwenye chama chake, sana sana nikuleta malumbano kila siku kwenye chama ma Chadema.

    ReplyDelete
  8. HAYA NDIO MAMBO YANAYOFANYA SIE WENGINE KUTOHANGAIKA KWENDA KUPIGA KURA. WANASIASA WOTE WANAFANANA, BILA KUJALI NI WAPINZANI AU CHAMA TAWALA.

    INASIKITISHA MAMBO YA NCCR 1995 YANAANZA KUJITOKEZA CHADEMA HATA KABLA HAWAJAKAA KIKAO CHA KWANZA CHA BUNGE. ZITTO NA TUNDU LISSU INAONEKANA WANA AJENDA YAO, KWANI WANAONEKANA KUTUMIA NGUVU NYINGI KUPELEKA MAMBO YA CHAMA KWENYE VYOMBO VYA HABARI BADALA YA KUTAFUTA SULUHU NDANI YA CHAMA.

    ReplyDelete
  9. Nionavyo mimi watu wanashindwa kufahamu maana ya kutoka mjengoni na kusikiliza hutuba ya JK kwenye Runinga.Kama KIZITO aliheshimu maoni ya waliomchagua kuwa haina maana ya kuapa kuwa utailinda, utaihifadhi na kuitetea katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, KATIBA hiyohiyo ndiyo iliyompa madaraka JK. Bora kutoingia kabisa kuliko kuingia na kukataa kutoka. Sisi watu wa kigoma tuliompa KURA Mh. Kizito tunasema kuwa msimamo aliouonyesha ametupa heshima yetu kulingana na maelekezo tuliyompa. Kama mwataka kumfukuza CHADEMA mfukuzeni lakini UBUNGE ataendelea kuwa nao mpaka mwaka 2030 kupitia chama chochote atakachokwenda, MHESHIMIWA ZITO USIBABAIKE NA VIBARAKA WA MB.... SISI TUKO NAWE DAIMA!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. CHADEMA ALIYEWALOGA NAONA AMEKUFA, KWANINI MNAANZA KULUMBANA. TAFUTENI UFUMBUZI WA NINI CHA KUFANYA WAKATI BUNGE LITAKAPO ANZA MWEZI FEBRUARI, BADALA YA KUANZA KUSHIKANA UCHAWI WA KWANINI HAWAKUINGIA BUNGENI WAKATI MH. JK ALIPOKUWA AKIZINDUA BUNGE. MBONA NYOTE MLIKWENDA KUAPA BUNGENI KAMA MLIKUWA HAMKUBALIANI NA MATOKEO SI MNGEKIMBILIA MAHAKAMA KUZUIA MATOKEO KUTANGAZWA.

    ReplyDelete
  11. Dr. Slaa nadhani uwe na busara kataika jambo hili. Inaonekana umeshabweteka na idadi ya wabunge mliopata. Pili, wapo wabunge waliopata kura kwakutumia nguvu zao wenyewe kwao hiyo hawaoni msaada wowote wa chama. Sasa nadhani chama tawala kimeshatumia huo mwanya kimeshagawanya makundi hamtaelewana tena. Acheni jambo hilo shughulikieni kwanza maswala ya kuiimarisha chama.

    ReplyDelete
  12. pETRO eUSEBIUS mSELEWADecember 3, 2010 at 2:04 PM

    Ndugu yangu Zitto,pamoja na usomi wako wote hauzijui shria za nchi.Chama kina nguvu kubwa mno..chaweza kukupora kila kitu.ukupokwa uanachama,kila kitu kinapotea.chunga sana kaka!

    ReplyDelete
  13. KITENDO CHA KUTOKA NJE YA BUNGE HAKIKUWAINUA CHADEMA BALI KIMEWADHALILISHA . PIA ZITTO HAJAIFA KIDEMOKRASIA AU SI MWANACHAMA WA CHADEMA HALISI ILA ANPITIA CHADEMA KUPA AJIRA NA MLANGO WA UBUNGE KUPITIA CHADEMA LAKINI SA KWA MOYO.MAANA HOJA NDANI YA CHAMA ZINAAMURIWA KWA KUPIGIWA KURA NA UPANDE UNAOPATA KURA NYINGI NDIYO UNAKUWA UAMZI WA CHAMA AU KIKUNDI. NA KWAMBA KWENDA KINYUME NA MAAMUZI YA WENGI NDANI YA UMOJA AU CHAMA NI KUKIUKA NA NI DHAHILI NI UKOSEFU WA HEKIMA , VINGINEVYO NJIA PEKEE AMBAYO MH: ZITTO ANGEICHUKUA NI KUTOKA KATIKA CHAMA. LAKINI KWENDA KINYUME NA MAKUBARIANO YA CHAMA NI UKOSEFU WA NIDHAMU. ZITTO SIO MWANADEMOKRASIA MAANA DEMOKRASI NI WENGI WAPE. MTU KAMA ZITTO AKIPATA URAIS NA BAADAE AKASHINDWA ANAWEZA KUAMURU APEWE MAADAMU FIKIRA ZAKE ZINATAKA KINYUME NA WENGI.KWANINI USIJE KWETU MOJA KWA MOJA UNANGOJEA NINI NA KWETU UKILETA MAMBO YA NJE YA UMOJA. TUTAKUTIMUA MAANA MAMBO YETU NI YA UMOJA NA YANAAMURIWA KUPITIA VIKAO KWA KUPIGIWA KURA.MIMI NI MWANACHAMA WA CHAMA TAWALA LAKINI TUNAPENDA TUWE NA TIMU PINZANI NZURI INAYOCHEZA VIZURI NA TUNAPO IFUNGA TUJUE TUMEIFUNGA TIMU NZURI LAKINI WACHEZAJI KAMA ZITTO, NI WAUZA TIMU,NI MWOGA. KWETU USIJE HUNA JIPYA, HUFAI UNAWEZA KUTUSALITI HATA SISI. NA MWAKA 2015 NITAKUJA KUGOMBEA HUKO KIGOMA. JAMANI HATA AKIJA KWETU

    ReplyDelete
  14. HABARI iliyoihusisha familia ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, imeibua utata mkubwa baada ya kuibuka kwa vitisho vilivyosababisha kuzuiwa kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema toleo lililopita Namba 161 katika mazingira ya kutatanisha; huku habari hiyo ikikanushwa kwenye gazeti jingine hata kabla haijatoka. “Baadaye niliitwa kwa bosi wao na kuambiwa natakiwa kwenda kwa Meneja Mkuu, aitwaye Shaber, ambako nilijulishwa kwamba ni lazima habari kuu (inayomhusu Lowassa) iondolewe vinginevyo gazeti halitochapwa kabisa,” anasema Mwendapole. Hata hivyo kwa upande mwingine, gazeti hili limebaini kuwa, maelezo ya awali ambayo yalitakiwa kutoka Tanzania na makachero hao wa Uingereza, ni pamoja na kutaka kufahamu kama kweli Frederick Edward Lowassa amezaliwa Agosti 26, 1977, Mwanza Tanzania na anamiliki hati ya kusafiria yenye namba AB 109402 iliyotolewa Tanzania na kwamba anwani yake nchini Uingereza ni 71 Hendrix Drive, Milton Keynes, MK8 0DY. Pia makachero hao waliitaka Serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi wakitaka kujua kama Frederick Lowassa ni mbia katika kampuni za Alphatel Partnership (Tanzania) Barare Ltd na Intergrated Tanzania Limited, kampuni ambazo zimefahamika kumilikiwa na familia ya Lowassa. Asasi hiyo ya Uingereza pia imeomba kujua kama FIU wana taarifa zozote za uhalifu dhidi ya Frederick Lowassa na kama baba yake Edward Lowassa anachunguzwa kwa tuhuma yoyote ya rushwa na mamlaka za uchunguzi wa rushwa nchini Tanzania kuhusu fedha haramu. Uchunguzi wa awali uliofanywa na vyombo vya dola, ulielezwa na taarifa hizo kwamba Frederick Lowassa si mbia katika kampuni hizo na kwamba Barare Ltd wenye hisa ni Edward Ngoyai Lowassa mwenye hisa 500 na Regina Mumba Lowassa mwenye hisa 500 huku wakurugenzi wakiwa ni hao hao. Ofisa wa Uingereza anayesimamia uchunguzi huo, George Simpson, ameliambia Raia Mwema kupitia barua pepe kwamba kanuni za uchunguzi kuhusiana na kesi zenye mguso wa kisiasa huwazuia kukanusha au kuthibitisha kuhusu uchunguzi unaoendelea hadi pale wanapofikia hatua ya kukamata mtuhumiwa ama anapofikishwa mahakamani. Taarifa ambazo gazeti hili limezipata mwanzoni mwa wiki hii kutoka vyanzo vyake zinasema kwamba uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, na kwamba watendaji wamepewa maelekezo ya kuendelea nao.

    ReplyDelete
  15. Mimi nahisi Zitto ni kibaraka wa CCM, kilichomfanya amkomalie Karamagi ilikuwa ni njaa yake, baada ya kuwekwa kwenye kamati ya madini Njaa ikamwisha. Mfukuzeni aende CCM

    ReplyDelete
  16. mtavurugana sana kwa ukabila na udini wenu. Werevu tushatambua

    ReplyDelete
  17. KWa wanaomjua Zitto hana tofauti na TAmbwe hiza ni matapeli wa kawaida wanaotafuta ulaji na umaarufu. Yapaswa zitto atimuliwe na anajulikana anvyoanza vurugu akijidanganya atagombea 2015.

    ReplyDelete
  18. Huo upumbavu si angeufanya huko nyuma kabla ya uchaguzi?aone wa tz walivyo na hasira

    ReplyDelete
  19. Zito hafai tena. Ni bomu linalosubiri kuteguka.

    ReplyDelete
  20. Hapo hakuna mtu wakusaidia Watanzania kila mtu anapigania tumbo lake na familia yake tu

    ReplyDelete
  21. Jamanı chadema demokrasıa nı pamoja na uhuru wa mtu mmoja mmoja kutoa maamuzı yake kama wengı walıshında kwa kupıga kura kwenye uamuzı wa ajabu sılazıma watu wote watekeleze.ebu achane mıpango ya kuwapa baadhı ya wabunge umaarufu usıo kuwa natıja kwa chama na taıfa.

    ReplyDelete
  22. Mimi nashangaa kwanini hawamfukuzi huyu Zitto. Na nyinyi mnaosema demokrasia nani ni mwanademokrasia kati ya zito na CHADEMA? Walipiga kura kukubaliana watoke wakati wa hotuba ya mkwere na waliokubali walishinda hata Zitto mwenyewe kakiri BBC. Sasa kama alilijua hilo kwanini bado alikuwa mpinzani? Ni demokrasia gani anayoongelea? Wapuuzi wengine wanakimbilia udini katika mambo ya msingi. Zito ni mpuuzi anatakiwa kupigwa chini mara moja. Acha mkwere ampe ubunge wa viti maalumu kama walivyopanga lakini hakuna haja ya kuwa na mtu muhuni ndani ya CHADEma. Wahuni wapo CCm aende kujiunga nao kama NCCR, TLP na CUF walivyofanya. Tanzania ndio maana kila kitu sifuri, eti udini. Yaani mtu ajiharishie upenuni tumuache kwasababu ni muisilamu? Wajinga kweli ndio waliwao.

    ReplyDelete
  23. Sana kaka 2po pamoja, chadema mtimueni huyo haramia na kijakazi wa ccm Zitto.

    ReplyDelete
  24. Kweli CHADEMA kazi imeisha maana mimi nilijua tu Mabere alipotua CHADEMA mwisho wake ni kufa kabisa.Hiyo ndo kazi ya Mabere Marondo(MATEMBERE).Kwani Zitto kupewa na CHADEMA barua ya kutoingia bungeni ni ya CHADEMA au Bunge?Naona sasa Lissu unafanya kazi za Dr.Kashilira..Kazi unayoooooooo..Lissu tatizo lako unajifanya KIPANGA SANA KUMBE KILAZA TU.

    ReplyDelete
  25. Watanzania..! maoni yetu yalenge kujenga taifa. Tupo kwenye kipindi kigumu cha mageuzi. CCM ni chama hatari sana kwa KUWAGAWA WATANZANIA KIFKIRA. Nasi kwa akili zetu zinazonuka umaskini.... tumenasa...!Zito ni kweli ana makosa.... acha chama kitowe maamuzi yake, nasi wananchi wapenda mabadiliko,tutowe baraka zetu kwa haki..! (Kwa sababu kuna baraka bandia..hasa waheshimiwa wanapoapa kwa kutumia misaafu au biblia wakati wanajua wamechakachua matokeo.. Ni DHAMBI KUBWA!!!) Mfano hai ni Uchaguzi wa Ivory cost. Chama tawala daima ndio huvuruga amani ya nchi. Watanzania umefika wakati sasa tujitambuwe. CHADEMA ndio chama makini Tanzania. Kina dira ya kumkombowa mtanzania. Zito hana sifa tena ndani ya CHADEMA...ni tayali anajuwa kumeingia vichwa.....ni haki yake kuhangaika. Kwasababu siku zake za umaarufu kisiasa zinaporomoka kwa kasi.

    ReplyDelete
  26. Kila kitu mtasema lakini mageuzi hayaji kwa kuiondoa ccm tu,ni upepo kila chama kitaikumba kwani demokrasia inachukua mkondo wake. hizo habari za kamati kuu ya chama kuamua fikra za Mtei,Ndesa,Slaa na Mbowe ndio mwongozo wa chama ni udikteta ambao Mungu ameunusuru katika nchi yetu kama hawa jamaa wangechukua madaraka.hawana uvumilivu wala ustahamilivu,hawafai. Wakati wa sasa kama mnavyosema wananchi wameamka vilevile mjue na mlio nao kwenye uongozi wameamka,hamtajifanyia mnavyotaka na hao wabunge walioingia kwa fadhila ole wenu

    ReplyDelete
  27. Mhh yaleyale ya CCM zidumu fikra za wenye chama,nyie vibaraka mlioandika hiyo barua kwa Zitto hamna lolote la kuwasaidia Watz,kwanza waoga kisha hamjiamini,mnatumwa kasemeni hivi kwa niaba ya chama halafu chama kinachukua hatua. Hao ndio wanafiki wakubwa. Mtalamba vidole vya wenye chama

    ReplyDelete
  28. Mh kaazi kweli kweli ,tatizo hapo ni mbowe kung'ang'ania madaraka.zitto alitaka kugombea uenyekiti wa chadema wazee wa kichaga wakaja juu wakamkataza, juzi tena wamemnyima kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kajichagua tena mbowe mbona cuf alikuwa hamadi rashid na sio mwenyekiti wa chama tatizo hapo ni kina edwin mtei kugeuza chama mali ya familia kumpa mkwewe uenyekiti wakati siasa haiwezi wamwache akauze ulevi bills

    ReplyDelete
  29. Zito naona amefika mwisho kisiasa kwani hata ngoma ikilia sana mwisho inapasuka.Msipoangalia zito atakididimiza chama. Aliwapigia simu ya nini wabunge wenzake watoke kwenye kikao halali cha chama wamfuate yeye?yeye ni nani chadema?

    ReplyDelete
  30. CHADEMA, CHADEMA...MSITUKATISHE TAMAA SISI VJANA!!
    ZITO ... ANGALIA BABA .... NYUMA YENU TUKO MAMILIONI YA WATANZANIA WAPENDA MABADILIKO. TUMEWAUNGA MKONO, TUKO NANYI CHADEMA...SASA MAMBO YA UPUUZI MANYOYAFANYA YANATUKATA MATUMAINI YA MABADILIKO. MSITUKATISHE MATUMAINI. SHIKAMANENI, REKEBISHENI KASORO HIZI AMBAZO HAZINA TIJA KWA CHADEMA NA KWA MAMILIONI YA WANANCHI WANAOIPENDA CHADEMA.

    WAKEREKETWA WA CHADEMA, ROME, ITALY.

    ReplyDelete
  31. DEMOKRASIA HUANZIA CHAMANI,KAMA HAMTAKI ITAKUJA TU KWA NGUVU YA WALIOKO. HATA AKIONDOKA ZITTO,HAO WAOGA WATABADILIKA NA KUANZA KUWAKATALIA MABWANYENYE.MSIMTUKANE ZITTO MKAFIKIRI NDIO MWISHO,MABADILIKO HAYAZUILIKI NA HAO WANAOTOA ODA WAKAE TAYARI ODA ZAO KUKATALIWA,MMEISAKAMA CCM KUMBE NYIE PIA HAMNA JIPYA
    HONGERA MAJIRA KWA KUACHIA MAONI YAANDIKWE BILA KUCHAKACHUA MAANA KUNA LINGINE HATA KURA WANAZOANDAA UKIPIGA KWA WASILOLITAKA IDADI HAIBADILIKI,WANAJIFANYA WANAELIMISHA WATU KUMBE NDIO WANAWAFANYA MAZUZU. "MAJIRA KEEP IT OPEN FOR ALL VIEWS AND NOT SELECTED"

    ReplyDelete
  32. CHADEMA ni chama makini, kama zito kajinyea atabaki na kinyesi chake, chama kitaendelea kubaki imara. Kwa mwenye akili ataweza kuona kuwa sasa CHADEMA inakuwa kama mtoto mwenye lishe bora, cha kufanya sasa ni kumkinga asipate maradhi ili afikie umri unaotakiwa kwa muda wake ili kuchukua nchi ifikapo 2015.

    Tunajua CCM wanalijua hili, na ninawashauri wa kiache maana wakiendelea kukizonga watapata aibu itakayowaua kabisa. Bora wajiandae kuwa chama pinzani kama KANU kule Kenya badala ya kuipoteza kabisa CCM. Big up CHADEMA, wasomi tupo nyuma yako, sisi ni walimu, tutawafundisha polepole hawa wenye akili nzito!

    ReplyDelete
  33. Mungu Baba, isaidie Chadema...waondoe mamluki wote ndani ya Chama na wale waliotekwa kifikra pasipo kujijua wape moyo wa kujirudi na kijishusha ili wawatumikie Watanzania waliowapa kura kwa matumaini mapya.
    Mungu ibariki Tanzani.

    ReplyDelete
  34. Tatizo la kuna watu wanapenda sana umaarufu, hebu jiulizeni Mwenyekiti wa LEAT yu wapi? Hata hasikiki kabisa wakati ndiye aliyekuwa kinara na shujaa wa kufanya vitu vingi lakini jamaa kwa kuwa hodari wa kukimbilia kwenye vyombo vya habari akaonekana kuwa yeye ndiye yeye na wenziwe wote hawakusikika tena. Kumbe alikuwa na malengo yake ya muda mrefu, tena nakwambia sasa hivi akishamaliza kugombana na Zitto basi ataingia kutaka kuovateki nafasi ya Mwenyekiti na hapo ndipo utakapokuwa mwisho wake kwenye chama. Heri Zitto anajua jinsi ya kuwacontrol hao wenye chama lakini huyu kwa style aliyotoka nayo leat akileta chadema ili awe maarufu zaidi ya wenye chama basi ataondoka mapema, hawajui hao wacha wamtumie kisha atakiona cha moto. Afadhali mwenzie Zitto hata leo akiondoka Chadema akaanzisha chama kingine kwao bado watamchagua kuwa mbunge wao. Sasa yeye mwenzangu na mie aliyeanza ubunge leo hata moja hajafanya bado jimboni kwake wakimtema hana pa kwenda, NCCR kawatukana, CUF ndio usiseme, na CCM ni matusi ya nguoni si ataenda wapi.

    Siasa si uhasama, na huyu bwana hajui kuwa wenziwe wamejaribu mara kadhaa kumfukuza Zitto wameshindwa wametumia kila mbinu na hila wameshindwa kwa hiyo safari hii wameamua kumuweka yeye mbele ndio awe kinara wa kumuondoa, nakuhakikishia ukimaliza hiyo kazi tu inakuja zamu yako maana hao wenzio wako hapo kwa maslahi ya biashara zao. Wewe pia ni kikwazo kwao ila wanakutumia kwa ajili ya umaarufu na mshawasha ulio nao.

    Kama ishu ni kutoka na watu hawakutaka kufika kabisa kwenye jengo tabu iko wapi? Bifu nyingine kama za BONGO FLEVAAAA!

    ReplyDelete
  35. nimekata tamaa na upinzani.inaonekana ni wababaishaji.nilipigia kura chadema nikiamini kuwa ni chama mbadala but now i dought if i was right.Watz tutakufa na tai zetu shingoni bila mtetezi wa kweli wa maslahi ya Taifa.wote wapo kimaslahi zaidi!Tell us the truth......KUNA MDUDU GANI CHADEMA?

    ReplyDelete
  36. Masanja,Tabora
    Zitto ni kibaraka wa CCM,hata huku jimboni mwake anasaidiwa na CCM ,lengo ni kuivuruga chadema.Aluta Continua Chadema.

    ReplyDelete
  37. Mwanaidi.Tabata
    Zitto wewe ni mtoto wa kike acha tamaa za kike,kuwa mwanaume na endeleza upinzani..Viva Chadema.

    ReplyDelete
  38. Hao wabunge ni wanachama wa CCM. Waliingia CHADEMA kutafuta ubunge baada ya kuonekana vilaza CCM. Sasa CHADEMA lazima mjifunze kuwa kuna wanaharakati wa kweli wa kisiasa na wataka vyeo, hao ndiyo watakaowachanganya kisawasawa. Mjijenge kisiasa kwanza, mjiimarishe acheni kudai mpewe nchi wakati hamna watu makini, bali mnasubiri makapi ya CCM.

    ReplyDelete
  39. Ufumbuzi wa masuala ya siasa unahitaji HEKIMA KUBWA. Kama unataka kuondoa funza kwenye kidole lazima utoe chumba chake chote. La sivyo mayai yataendelea kuzalisha wengine. NINAMAANISHA kuwa UONGOZI MZIMA wa CHADEMA ujiangalie, ujichekeche halafu ufikie mahali pa sawazishana. Kufukuzana si jibu BALI NI KUWAKATISHA TAMAA WALIOWACHAGUA. Pia kumfukuza Zitto siyo jibu WANA-KIGOMA wanampenda anagalieni yaliyowapata kupoteza viongozi wenu sasa ni NCCR-M. Mtaji huo huo wa kufukuzana hautawafikisha popote. Mjifunze toka kwa CCM inapokuwa na jambo zito hujimbia chumbani na kusawazisha mambo ndani kwa ndani HAWAFAIDISHI VYOMO VYA HABARI. CHUNGENI SANA NA BUSARA ZENU VIONGOZI ZITAWAFANYA KUHESHIMIKA NA CHAMA KUENDELEA KUHESHIKIMA..

    ReplyDelete
  40. CHADEMA kuitana MAMLUKI wacheni. Mbona wabunge muliowapata wanatoka VYAMA vingine...huko huko wakiitwa mamluki? Hivi bila interest zenu kuto-zingatiwa ndipo mnaitana mamluki? Chungeni sana UHURU WA KUSEMA NA KUTOA MAONI. Pia VIONGOZI WA CHADEMA hasa wabunge manapaswa mkomae ...solidarity inayong'anganiwa na Viongozi wakuu wa CHADEMA inapingana na ACTIONS ZENU including Chairman Mbowe na Mnadhimu-mwanasheria....You take oath and you go against it!!Chungeni ACTIONS zetu....Mungu hadanganyiki..You held up Bibles and Qu'ran..Angels and people were witnessing.

    ReplyDelete