09 September 2013

INATISHA

  • OPERESHENI YA JK YAIBUA MAKUBWA
  • MWANAMKE ASALIMISHA SMG POLISI


Na Mwandishi Wetu
OPERESHENI y a kuwaondoa wahamiaji haramu, kuwakamata watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, imeanza kuzaa matunda ambapo bastola 38 na bunduki za kivita zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uhalifu, zimerejeshwa polisi.

Kurejeshwa kwa silaha hizo kumetokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa hivi karibuni akiwataka wahamiaji haramu kurejea katika nchi zao ndani ya wiki mbili na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe

 Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu kuhusu operesheni iliyoanza Agosti mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, Bw. Venance Mwamotto, alisema operesheni hiyo ambayo ni endelevu, imelenga kukomesha vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha mkoani humo.
Alisema operesheni ya salimisha silaha kwa hiari na utoaji siri za watu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi mkoani humo, wananchi na viongozi wa mkoa huo.
“ H a d i s a s a b a s t o l a zilizosalimishwa ni 38 na bunduki za kivita SMG ni mbili, moja ilipelekwa katika Kituo cha Polisi Kibondo na mwanamke, Bi. Erica Josamu (35), mkazi wa Kibondo (picha yake ipo ukurasa wa mbele).“Kati ya watu waliorejesha silaha hizo zinazoweza kutumika kwenye vita ni mmoja ambaye ameonesha ujasiri, nasi hatukusita kumzawadia kwa hiari,” alisema.
Al i o n g e z a k uwa , k a t i k a mahojiano ya awali na mwanamke huyo, alisema silaha hiyo aliiokota njiani na kuamua kuifikisha kituoni hapo, lakini baadaye alikiri kuimiliki na kuitumia kinyume cha sheria na hakuchukuliwa hatua zozote.
“Hatukumchukulia hatua kwa sababu tulitangaza watu warejeshe silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kwa hiari yao, hakukuwa na adhabu yoyote kwa watu walioziwasilisha polisi,” alisema.
Bw. Mwamo t t o a l i s ema wamefanikiwa kuokota silaha nyingi zilizotupwa na wananchi hasa maeneo ya Kambi ya Nduta, ambayo walikuwa wakiishi wakimbizi ambapo eneo hilo lilikuwa maficho ya majambazi sugu.Alisema maeneo mengine yaliyookotwa silaha ni Kamuhasha, Kumbanga na Kanembwa ambapo kulikuwa na matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha.
“Majambazi sugu kutoka Burundi kwa kushirikiana na wakimbizi, walikuwa wakifanya uhalifu na kukimbilia katika Kambi ya Nduta hivyo maficho yao tumeyasambaratisha na kuongeza ulinzi.
“ P i a k a t i k a k amb i h i i tumefanikiwa kugundua shamba la bangi ambayo baada ya kuvunwa ilipatikana kilo 1,500...yote tumeichoma moto, ilikuwa vigumu kubaini kama eneo husika kulikuwa na kilimo cha bangi kutokana na mazingira yalivyokuwa,” alisema.
Aliongeza kuwa, Kambi ya Nduta ni eneo ambalo lina sifa kubwa ya uuzaji dawa za kulevya, bangi na maficho ya majambazi sugu ambapo uhalifu huo ulikuwa ukifanyika bila woga.Alisema operesheni hiyo haina mwisho hadi mtandao huo utakapomalizika ambapo asilimia kubwa ya wakimbizi waliokuwa wakijihusisha na matukio hayo, tayari wameondolewa nchin

4 comments:

  1. xenophobia,hao wakimbizi waliondoka Kambi ya Nduta zaidi ya miaka 4 iliyopita,kambi hiyo wakawagawia wananchi mashamba walime mazao,eneo lote la former Nduta linamilikiwa na Watanzania for the last foru years,leo Shamba la Bangi limegunduliwa wanasema ni la wakimbizi,silaha wamesalimisha wanasema ni za wakimbizi,ni ajabu mkimbizi aliyeondoka miaka minne iliyopita leo arudi tena Nduta kwa ajili ya kusalimisha au kutupa silaha shambani.lets stop this xenophobia,ni aibu.

    ReplyDelete
  2. Hakuna mtu aliyezaliwa na jina/alama ya ukimbizi.Sote tusome historia na alama za nyakati unaweza ukakuta watu wanamjadili mkimbizi kama mnyama fulani hivi au mtu aliyejitakia matatizo.Ninacho amini ni kwamba Burundi amani imesharejea,DRC nako amani itarejea nao wakimbizi kwa jina mlilowabatiza watarudi kwao.Tanzania haijapewa CHETI na mungu kubakia nchi salama milele bali ni kwa neema tu,tukumbuke siku chache tu upepo mbaya umepita nchi za uarabuni kama vile Libya,Misri n.k hakuna aliyejua kama yote haya yangetokea nchi za wenzetu.WAKIMBIZI NAO NI WATU WAPEWE HESHIMA YAO.Tumepewa amani bure Tanzania,tuilinde na kuidumisha maana tukiichezea nasi tutafukuzwa kama wenzetu wanavyofukuzwa.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  3. Maoni mazuri dunia ni kigeugeu,unamfanyia mwenzako ukatili leo,usije uukalaumu kama utageuziwa kibao,ni vizuri jambo hili lifanyike kwa busara zaidi.tusije tukaombewa dua mbaya amani yetu ikavunjika.kisha nasi tukafanyiwa yale yale tuliyowafanyia .

    ReplyDelete
  4. Nawashangaa Ndg zangu nyie wawili mlionitangulia. Hivi kuna ubaya gani Ndg zetu wamefanyiwa??? kuambiwa warudi kwao?? Hivi hata wewe leo uambiwe urudi kwenu kwa usalama km huu utachukizwa na nini??Au na Nyie ni wamojawapo?? Watanzania tuna kila sababu ya kujivunia Utanzania wetu, Wanyarwanda/ Warundi/ Wakenya/ Waganda nk. Nao hawana budi kujivunia uhalisia wa nchi zao. Waende wajenge nakuimalisha uchumi wa kwao, na watambue hata ipite miaka mingapi wao sio Watanzania, labda wakikamilisha utaratibu wa kuishi nchini. Anayewahurumia, awasaidie kwa huo utaratibu. WAENDEEEEEEEE.

    ReplyDelete