Na
Mwandishi Wetu
BENKI ya Eximim ekabidhi shilingimilion
i10, kwaBenkiKuuyaTanz ania(BoT) zitaka zot um ikakus aidiaMfukowaUdha mini
waBen kiKuumaaruf u k ama'Mwali muJu lius Nyere reMemorial Schol arshipFund'iki
wa ni dhamira yaBenki yaEximku ungam konojit ihadaza ku endele zasekta ya elim
unchin i
.Benk iKuumapem
amwezi uliopitail itanga za kuwaita dhaminiwanaf unzi s itawae limu
yajuuwaliokatikakiw ang ochas hah ada yakwanzana shahada ya uzamiliwa naosome
am asomoyahesabu, sayans i nateknolojia chini ya mfukohuo.
Akizung umzaw
aka tiwah aflaya kukabidhimsaada huoDa r es Salaa mmwishoni mwa wiki ,Kaimu
Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha Dkt. Natu Mwamba,alisema mfuko huo
umejikita katika kudhamini wanafunzi wa kike katika shahada ya kwanza wanaosoma
hesabu, sayansi na teknolojia katika vyuo vikuu nchini mwaka huu.
"Fedha
zitakazopatikana katika mfuko huu zitatumika kudhamini wanafunzi wote wa kike
na kiume wa Tanzania wanaosoma shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi,
tehama, heasabu na fedha pamoja na wanafunzi wanaolenga kusoma shahada ya
uzamili katika maeneo hayo.
"Udhamini
utatolewa kwa kufuata sifa za kitaaluma na kupitia mchakato mkali wa uteuzi wa
wadhaminiwa, alisema na kuongeza kwamba waombaji watakaofanikiwa watapata
udhamini kamili pamoja na kupewa laptop," alisema.
Dkt. Mwamba alisema kuwa udhamini huo
utalenga gharama za moja kwa moja za chuo ikiwa ni ada na usajili na pamoja na
gharama nyingine za mwanafunzi zikiwemo chakula, malazi, vitabu na vifaa vya
kujisomea isipokuwa gharama za mafunzo kwa vitendo, mahitaji maalum ya masomo
na gharama nyingine kama zilivyoorodheshwa na chuo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Exim, Bw. Anthony Grant alisema benki hiyo inatambua umuhimu wa
kusaidia elimu kwa maendeleo ya vijana kwa kuwa wao ndo viongozi wa baadaye wa
Taifa hili.
Naye Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya
Exim, Bi Anita Goshashy, aliongeza kuwa benki yake imekuwa mstari wa mbele
kusaidia jitihada mbalimbali za kusaidia maendeleo ya jamii zikiwemo afya na
elimu.
Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya
Mwalimu Julius Nyerere ulizinduliwa jijini Arusha mwaka jana na Rais Jakaya
Kikwete ukiwa na lengo la kukuza elimu katika masomo ya hesabu, sayansi na
teknolojia kwa wanafunzi wa kike.
Kila mwaka mfuko unalenga
kudhamini takriban wanafunzi 25 wenye vigezo na wanaofaidika na udhamini ni
pamoja na wanafunzi wa kike waliofaulu zaidi katika masomo ya hesabu na
sayansi.
No comments:
Post a Comment