09 September 2013

CHADEMA: NDUGAI ALITUMWA

 •  LIPUMBA ASEMA MBOWE AMEDHALILISHWA BUNGENI 

Rachel Balama na Darlin Said
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), tukio la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuondolewa bungeni mjini Dodoma kwa agizo la Naibu Spika, Bw. Job Ndugai, lilipangwa na Serikali ili kuhakikisha Muswada wa sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013, unapitishwa bungeni ili kulinda masilahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CHADEMA, Bw. John Mnyika, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema Serikali ilipanga kupitisha muswada huo bungeni ndio maana hata Bw. Mbowe kama Kiongozi wa Upinzani bungeni, aliposimama kutaka kuzungumza, hakupewa nafasi hiyo badala yake alitakiwa akae na alipokataa Bw. Ndugai aliagiza atolewa nje jambo ambalo hawakuliunga mkono.
Aliongeza kuwa, Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wabunge wa CCM wanakuwa wengi katika Bunge la Katiba ili kupitisha mambo wanayoyataka."Kilichopitishwa bungeni na wabunge wa CCM ni kibaya kuliko ilivyokuwa awali...wameharibu zaidi, CHADEMA imepinga kwa masilahi ya makundi mengine ya kijamii ili yaweze kupata uwakilishi katika bunge hilo," alisema.
Bw. Mnyika alisema CHADEMA walipendekeza Bunge la Katiba lipunguze uwakilishi wa chama kimoja ambapo katika kipengele cha wajumbe 166 wanaoteuliwa na rais, iongozwe na kufikia wajumbe 359 lakini Serikali imekataa."Lengo letu ni kutoa nafasi kwa makundi mengine ya kijamii kama wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi na taasisi nyinginezo kutoa wawakilishi wao kwenye bunge hili," alisema.
Alisema upande wa Zanzibar, hakukuwa na wawakilishi waliotoa maoni yao juu ya nafasi ya Zanzibar katika bunge hilo na kilichosemwa na Serikali ni uongo."Serikali baada ya kushindwa kuchakachua Mabaraza ya Katiba, sasa imeona njia pekee ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kwenye Bunge la Katiba wabunge wa CCM wanakuwa wengi," alisema.
Akizungumzia uamuzi wa Bw. Ndugai kumtoa nje Bw. Mbowe, alisema Naibu Spika amevunja kanuni ya 76 ya Bunge kwani hana nguvu ya kuita askari ambapo kwa mujibu wa kanuni ya 20, alitakiwa kuhairisha shughuli za Bunge."Ndugai amefanya kosa la kuwaingiza watu wasiohusika bungeni na kuruhusu vitendo vya uhalifu vitokee ili kupitisha muswada walioutaka na kulinda masilahi ya chama kimoja.
"Sekretarieti ya CHADEMA itakutana kesho (leo) ili kujadili kwa undani suala hili na kulishughulikia, pia tutatumia nguvu ya umma (wananchi) kuhakikisha katiba haivurugwi, tutakutana na vyama vingine vya upinzani," alisema.Alisema chama hicho hakioni sababu ya kuharakisha katiba badala yake kama wanataka katiba hiyo itumike katika Uchaguzi Mkuu 2015 ni vyema ikaandaliwa ya mpito.
Aliongeza kuwea, katika Bunge lijalo Sheria ya Kura za Maoniambayo itajadiliwa ni ya hatari zaidi kuliko Bunge la Katiba na isipofanyiwa marekebisho, itazusha mgogoro mkubwa zaidi.Katika hatua nyingine, Chama cha Wananchi (CUF), kimepinga kitendo cha askari wa Bunge, kumtoa nje Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe, baada ya kuzuiwa kuzungumza.
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema kitendo cha Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, kuwaagiza askari wa Bunge wamtoe nje Bw. Mbowe, hakiwezi kukubalika, bali ni unyanyasaji na udhalilishaji mkubwa.
"Ni kitendo cha aibu na hakikupaswa kufanywa na Naibu Spika (Ndugai), CUF tunajiuliza angesimama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kutaka kuzungumza angemnyima?" alihoji.Alisema Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013, ulikuwa na utata mkubwa kwani Serikali imeubadili kwa kuondoa maoni muhimu ya wadau ambapo Wazanzibari hawakushirikishwa ipasavyo.
"CUF tunataka muswada huu urejeshwe kwa wananchi ili ujadiliwe upya, mbali ya Mbunge wa Singida Mashariki (Tundu Lissu- (CHADEMA) na Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Zanzibar (Hamadi Masoud), kuthibitisha kuwa Zanzibar haikushirikishwa, wabunge wetu hawana taarifa kama wananchi wao walishirikishwa.
"Kuupitisha muswada huu ni njama za wazi za Serikali na kiti cha Spika kutelekeza maoni ya wananchi na kuyapatia kipaumbele ya CCM, hivyo kuondoa uhalali wa Bunge na kiti cha Spika katika kusimamia mchakato wa kutafuta Katiba Mpya," alisema.Katika hatua nyingine, Prof. Lipumba muswada huo unampa Rais Jakaya Kikwete, mamlaka ya kuteua watu anaowataka kuwa wajumbe wa Bunge la kutunga sheria.
Aliongeza kuwa, hivi sasa kila taasisi itapaswa kuteua majina tisa na kumpa Rais ambaye atateua jina moja au asiteue kabisa,CCM na Serikali wanajua hujuma wanazofanya katika mchakato huu ili kupata katiba wanayoitaka wao si wananchi," alisema.Alisema upo umuhimu wa wananchi kuunga mkono msimamo wa wabunge wa upinzani na kudai kuwa, watendaji wa Serikali wakiwemo Mawaziri na Naibu Spika, wanamhujumu Rais Kikwete asifanikishe mchakatato wakupata Katiba Mpya.
Alisema muswada wa kwanza wa Mabadiliko ya Katiba ulikuwa mbovu ambapo Rais Kikwete alilazimika kuzungumza na wapinzani ili kuurekebishaWakati huo huo, CUF imedai kusikitishwa na kitendo cha kupigwa na kutupwa nje ya lango la Bunge Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi (CHADEMA), na kuvuliwa hijab kwa Mbunge wa Viti Maalum, Bi. Mozza Abeid (CUF) na kudai huo ni udhalilisha usiokubalika.

13 comments:

 1. Hoja yenu chadema ni ya kitoto haina uzito, nyinyi ni mabondia zaidi kuliko wanasiasa

  ReplyDelete
  Replies
  1. Tunashabikia uhuni wa chadema leo. Tutawapigia kura. Wakiingia madarakani tutajuta. Wanavunja na kukanyaga taratibu zote rasmi za kuongoza mijala. Mwisho wanalalamika kuonewa. Wanaugwa sana mkono na magazeti yao yasiyoweka bayana lipi ni uhuni na lipi ni jema

   Delete
  2. kijana soma vzuri uwelewe kisha uchangie hoja zenye manufaa kwa taifa letu
   Delete
 2. La msingi tujifunze kufuata kanuni na sheria. Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani bungeni ndio pekee wanaruhusiwa kusimama bungeni wakati wowote na kusema. Aliposimama Mbowe, Ndugai alitakiwa amruhusu kuongea,sio kumfukuza. Amevunja kanuni na ndio kiini cha matatizo.

  Lakini wa Tanzania pia lazima tujifunze kuwa waadilifu. Sheria ya Sim Card imelalamikiwa kupitishwa kinyemela, sasa marekebisho ya sheria hii ya katiba nayo yamebadilishwa last minute na kutaka kupitishwa kinyemela. Tochi imemulika ikaona ukiukwaji huu, ndio maana Mbowe akasimama. Angeruhusiwa kuongea,bunge ingebidi liahirishwe,badala yake amefukuzwa na wakalazimisha kupitisha.

  Walichotaka Chadema na yule mbunge wa CUF ni ushirikishwaji ZAIDI wa makundi maalum kule Zanzibar, kwanini Ndugai na CCM hawataki makundi haya yashirikishwe zaidi?. Kwanini hawataki wigo wa Bunge la katiba upanuliwe?.Hii katiba mpya si ni ya wote kwa manufaa ya wote?. Au wanataka kutengeneza katiba ya nani?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kwahiyo hayo makundi yana tija gani kwa mwananchi wa kawaida. Hilo tu mfanye bunge kuwa uwanja wa masumbwi.

   Delete
  2. Haya makundi yanawakilisha wananchi wa kawaida,kwa hiyo tija yake ni kupata katiba ya wananchi wenyewe.Walifanya fujo,lakini itatusidia zaidi tukijua kwanini walifanya fujo,si kushughulika na fujo yenyewe tu alafu basi.

   Delete
 3. katiba kamwe haitaiokoa ccm na anguko lake 2015,mnapoteza muda wenu kumbukeni hata odinga Kenya alifanya kila hila kwenye katiba ya Kenya akidhani itampa ushindi mwisho wa siku akaangukia pua Kenyatta ameunda serikali ccm hila zenu kwenye katiba hazitawabakisha madarakani 2015.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wewe mfuasi wa chadema unafikiri mtawalipa nini wananchi mnaowadanganya? Kwanza wananchi wengi wako bize wakilima, wakijenga nyumba, wakipelelka watoto shule na kuingiza magari mapya. Mitaani sisikii watu wakiongelea kuhusu katiba. Nasema kweli kwa jila la mwenyezi Mungu, mitaani hakuna mijala ya katiba watu wanapambana na maisha kama kawa. Nyie muongee mpaka mkaukwe makoo, hakuna nayejali. Chadema ikipata ridhaa ya kuongoza serikali bado haitawapatia kazi wafuasi wake wote. Lazima wakulima watakuwepo, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo na watumishi wa umma pia. Sifa ya serikali palepale! Toa hoja lakini uwe na uelewa mpana kesho yasije yakakufika ukajuta!

   Delete
  2. Sio ufuasi wa Chadema, si unaona sasa na vyama vingine vipo?. Ukiacha ushabiki unao uendekeza,utaona mwanga. Shida yako kubwa umeshindwa kuhusisha katiba, mfumo wa utawala wa nchi na maisha ya kila siku ya hao unaosema wanaendelea na maisha yao.Yaani wewe bora liende tuu!

   Delete
 4. Kwahiyo waingereza na wamarekani ambao madola yao yamedumu kwa miongo mingi ni bora liende? Ushabiki na uelewa ni vitu viwili tofauti. Kwanza wenzako wana malengo mahususi ya kuongoza dola. Wewe una malengo gani? Kwavile ridhaa ya kushika dola iko mikoni mwa wananchi sio kwa makundi ya wasomi wachache. Kwa mawazo yako unatakaa kushawishi umma wa watanzania kua Wazambia, Wamalawi, Wamisri, watunisia nk sasa wako peponi na mifumo ya maisha yao imebadilika.

  ReplyDelete
  Replies
  1. We Tanzanians,it is not a time of arguing on the political matters because whatever we are going to argue there are special people who are there to step down those important things for the minority beneficial. Let us strictly deal with our business that makes us to survive.Whatever we are going to cry and complain on the existence government nothing will change rather we are wasting our times.For our protection and to be in safe side let us be critical thinkers in making our decisions for the benefit of all Tanzanians.

   Delete
  2. Labda hii itakufungua macho kwa mbaaali

   Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

   Tunaongelea mapungufu hapa,sio ushabiki.

   Delete
  3. Tatizo sio mabadiliko au mijadala mikali bungeni. Hakuna hata Mtanzania mmoja ambaye kwa sasa hajaamka na kutaka maisha bora zaidi na yenye haki na uhuru zaidi.
   Tatizo ni mwenendo mzima wa mabadiliko. Huwezi kuwa na uhakika kwamba watu ambao wamefanya kampeni nyingi za kutaka nchi isitawalike na wakashindwa na pia kutakia hoja mbalimbali wakijijengea umaarufu hawatakua maditeta wabaya sana mara wakabidhiwapo madaraka.

   Jaji Warioba alihoji mwenendo huo ambao mnajaribu kukwepa kusisitiza na kussisitiza kile tu kinachopelekana na maslahi yenu. Hata Kabwe pamoja na kuunga mkono hoja ya rais kutosaini mswada bado umehoji uhalali wa kumshinikiza rais.

   Je hizo kampeni zinazofanyika hazigharimiwi na walipa kodi? Na kama laa hizo pesa za kutembea nchi nzima kwa kasi zaidi hata ya rais wanazipata wapi?
   Kama kuna usiri iacheni serikali nayo itatunze siri zake!
   Serikali kamwe haitetewi bali inakosolewa. Tunachoangalia ni nini kitatokea kama ukiitisha mapinduzi zidi ya demokrasia.

   Delete