- CHADEMA KIGOMA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU
- HOFU YA KUTOKEA VURUGU YATANDA MAJIMBONI
Na Mwajabu Kigaza, Kigoma
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), mkoani Kigoma, kimesitisha ziara ya Katibu Mkuu wa chama
hicho Taifa, Dkt. Wilbrod Slaa, ambayo ilipangwa kufanyika mkoani humo kuanzia
Desemba 5 hadi 13 mwaka huu, kutokana na hofu ya usalama miongoni mwa wanachama
wake.
Mwenyekiti
wa chama hicho mkoani humo, Jafari Kasisiko, aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, usalama katika baadhi ya
majimbo mkoani humo ni mdogo sana.
Alisema
kutokana na hali hiyo, wameona ni bora ziara hiyo isitishwe kwanza ili kuepusha
machafuko yaliyoandaliwa na wanachama dhidi ya Dkt. Slaa kama atafika mkoani
humo.
“Uamuzi wa
kusitisha ziara hii umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Uongozi mkoani hapa
kilichofanyika Desemba Mosi, mwaka huu na kushirikisha viongozi wa majimbo
mengine.
“Majimbo
haya ni Kigoma Mjini, Kaskazini na Kusini ambao kwa pamoja walielezea uwepo wa
njama za kuhujumu ziara hii ili kumdhalilisha Dkt. Slaa,” alisema.
Aliyataja
majimbo yaliyodaiwa kuchafuka kisiasa kutokana na maamuzi ya Kamati Kuu ya
CHADEMA kumvua nyadhifa za uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho
Bara, Bw. Zitto Kabwe kuwa ni Kigoma Mjini, Kaskazini na Kusini, wakati ambapo
majimbo ya Buhigwe, Kasulu, Muhambwe na Buyungu pia hali ya usalama imedaiwa
kuwa ya mashaka.
Akizungumzia msimamo wa chama hicho
mkoani humo kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu kumvua uongozi Bw. Kabwe kwa madai ya
kutaka kukisaliti chama, alisema kikao hicho kilikuwa halali.
“Hatua zote za kumvua uongozi Bw.
Kabwe na wenzake Dkt. Kitila Mkumbo na Bw. Samson Mwigamba, zilifuatwa sasa kama anadhani ameonewa, ana haki ya kukata rufaa Baraza
Kuu.
“Ziara ya Dkt. Slaa hapa Kigoma,
haina uhusiano na maamuzi ya Kamati Kuu kwani ilipangwa muda mrefu na
kusitishwa kutokana na vikao vya Kamati Kuu, lengo la ziara hii ni maandalizi
ya uchaguzi ujao ngazi za chini,” alisema.
Aliwataka baadhi ya wanachama
wanaoendesha vitendo vya vurugu na kuhujumu miundombinu ya chama kuacha kufanya
hivyo kwani ni kinyume cha maelekezo ya chama kwani palipo na vurugu hakuna
haki.
Baadhi ya wanachama wa chama hicho
kutoka majimbo yaliyotajwa kuwa na vurugu, walikutana Mjini Kigoma katika moja
ya kumbi za mikutano kupinga ujio wa Dkt. Slaa, Desemba 5 mwaka huu.
Akisoma tamko la wanachama hao,
Fanuel Sindika alisema wameikataa ziara hiyo kwa sababu CHADEMA kimekuwa
kikiwaonea baadhi ya viongozi hasa kutoka mikoa ya Magharibi na wapo tayari
kufanya vurugu ili kumdhalilisha kiongozi huyo.
Alisema hawakubaliani na maamuzi
yaliyotolewa na Kamati Kuu dhidi ya Bw. Kabwe ambayo hayajazingatia haki kwa
mujibu wa katiba.
Aliongeza kuwa, kwa muda mrefu chama
hicho kimekuwa na mgogoro unaotokana na hofu ya madaraka katika nafasi ya
Mwenyekiti wa chama ambayo inadaiwa kuwaniwa na Bw. Kabwe akisaidiwa na rafiki
zake kwenye kampeni ili kuhakikisha anashinda kiti hicho.
Hivi karibuni,
baadhi ya vijana kutoka Tawi la Mwandiga, Jimbo la Kigoma Kaskazini, walifanya
maandamano ya pikipiki na kuburuza bendera barabarani, kuchoma kadi, bendera na
kuvunja bango la Tawi la Msingi katika kijiji hicho
KIGOMA MSIKILIZENI HUYO SLAA LA SIVYO MTAONEKANA WABABAISHAJI AU MNATUMIKA. ADUI UKIMKIMBIA HUTAMJUA KAMA YUKO JUU YAKO HUTAWEZA KUJUA MBINU ZAKE. NI UJUA TU KUZUIA SLAA ASITEMBELEE KIGOMA KITU KINACHOKOMAZA WATU KUSEMA WATU WANATUMIKA ILI TATIZO LIENDELEE KUWEPO.
ReplyDeletekwa wenye uelewa haihitaji darasa ili kuyafahamu haya, na kakuna kinachoweza kueleweka bila maelezo namajadilianona pamoja, poleni sana wana kigoma kwa kukosa haki ya taarifa.
ReplyDeleteJAMAN WATU WA KG KUWENI WAELEWA MSIKILIZENI MWENYEKITI WA CHADEMA NDIPO MTAELEWA UTATA UKO WAPI HAPAITAJI ELIMU YOYOTE NI MASIKIO YENU TU
ReplyDeleteWewe nichizi kama kama slaa wako, mtaishia hapo hapo nachuki zenu wala hamuwezi kushinda na KG mkifika mnaliwa Live
ReplyDeleteendeleni kuvua dagaa na huyo zitto wenu amieni ccm basi kama anataka
ReplyDeletendo maana mnavua dagaa angali wenzenu tunavua samaki
Delete