- WALIOUWAWA NA AL-SHABAAB KENYA WAFIKA 60
- MWANADIPLOMASIA WA CANADA NAYE AUWAWA
- MAKOMANDOO ISRAEL WATUA NAIROBI KUWASAKA
Mmoja wa majeruhi (kushoto) akiwa na jeraha la risasi mgongoni akikimbia kuondoka eneo la tukio.
Watu wakikimbia kuokoa maisha yao baada ya wavamizi kuanza kumiminia watu risasi.
Majeruhi akiwa amebebwa kuondolewa eneo la tukio baada ya kushambuliwa na risasi.
Na
Goodluck Hongo
Idadi ya watu waliokufa katika shambulio
lililofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi
nchini Kenya
imefikia zaidi ya watu 60 na wengine 162 kujeruhiwa baada ya kundi la watu
wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al-Shabaab kuvamia na kuwamiminia risasi
ovyo.
Kwa
mujibu wa kituo cha televisheni cha The Citizen cha nchini Kenya, kundi hilo
lilivamia jengo hilo saa saba kasoro dakika 10 mchana juzi na kuanza kuwapiga
risasi watu hao. Vikosi
vya usalama vya nchi hiyo vikitumia mbwa na helikopta, vimeendelea kuzingira
jengo hilo ambapo hadi jana mchana kundi hilo la watekaji lilikuwa bado linawashikilia watu ndani
ya jengo hilo
la ghorofa nne.
Jengo
hilo ambalo ni lenye maduka na migahawa mingi
hutumiwa na watu wengi ambapo mara nyingi siku kama
ya Jumamosi hujumuika na familia zao kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Televisheni
hiyo ilionesha jinsi vikosi vya usalama vya nchi hiyo vilivyokuwa vikiokoa watu
ambao walikuwa ndani ya jengo, huku helikopta za kijeshi zikizunguka jengo hiloTelevisheni
hiyo ilisema wanamgambo hao ambao idadi yao
haijafahamika bado wamejificha ndani ya jengo hilo wakiwa wamewateka idadi ya watu
wasiojulikana wakati juhudi za kuwaokoa zikiendelea.
Mitandao
ya kijamii
Katika
baadhi ya mitandao ya kijamii ilimnukuu Rais wa Kenya,
Uhuru Kenyatta, akielezea shambulizi hilo
kuwa ni la kigaidi na kwamba kitendo hicho kamwe hakikubaliki.Alisema waliohusika watakumbana na mkono wa sheria.
Aliongeza
kuwa Wakenya hawatagawanyika kutokana na shambulizi hilo
na jeshi lake litaendelea
kukabiliana na magaidi wa nje na ndani ya taifa hilo. Rais
Kenyatta alisema baadhi ya waliofariki ni jamaa zake na miongoni mwa
waliofariki ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa.
Taarifa kutoka Ikulu
ya Rais wa Kenya
zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.
Mashuhuda
Walioshuhudia
shambulizi hilo wanasema kuwa waliwaona watu
waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakianza kumshambulia kila mtu waliyekutana
naye ndani ya jengo hilo.Inadaiwa kwamba
walikuwa wakiuliza waliyekutana naye maswali na aliyeshindwa kujibu alipigwa
risasi.
Uingereza
yatoa tamko
Waziri wa Mambo ya
Nje wa Uingereza, William Hague, alisema Serikali yake inashirikiana na Kenya
kuhakikisha magaidi na wanamgambo hao wanapatikana.Hili ndilo shambulizi
baya zaidi kuwahi kuikumba Kenya
tangu shambulizi la bomu lililotokea mwaka 1998 lililotekelezwa na Al-Qaeda.
Vikosi vya usalama
vikishirikiana na vikosi maalumu kutoka jeshi la nchi hiyo wameendelea kuweka
ulinzi mkali ili kuwaokoa watu walioshikwa mateka na watekaji hao wenye silaha
nzito kwa majibu wa mashuhuda.
Shirika la Utangazaji
la Uingereza (BBC), lilimnukuu Waziri wa Usalama Joseph Ole Lenku, akisema watu
59 wamefariki katika shambulizi hilo
lililofanywa na wanamgambo wa Al-Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.Waziri Ole Lenku
alisema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo hilo
ni kati ya 10 na haijulikani wamejificha sehemu gani katika jumba hilo la Westgate.
Red
Cross wanena
Shirika la Msalaba
Mwekundu la nchini Kenya
awali katika taarifa yake, lilisema kuwa watu 43 ndiyo waliofariki na zaidi ya
50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa katika shambulizi hilo.
Habari zinaeleza kuwa
hadi jana jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo,
magari ya kijeshi yamepelekwa katika eneo hilo,
huku polisi na wanajeshi wakijaribu kuokoa mateka.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo, zinasema
wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.
Al-Shabaab
watamba kuhusika
Kwa mujibu wa BBC,
ofisa mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab, aliliambia shirika hilo kuwa kundi hilo ndilo
limehusika na shambulio hilo.Kwa mujibu wa ofisa
huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita ndani ya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na
kundi hilo.
Wanamgambo wa Al
Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia
kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake
nchini humo kupambana dhidi yao.
Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari
zitakuwa mbaya mno.Kupitia mtandao wao
wa Twitter, Al-Shabaab limesema kuwa Kenya
haikusikia onyo hilo na kuendelea kuwaua
Waislamu wasio na hatia nchini Somalia.
Taarifa hiyo ya
Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa
yanayowakumba Wasomali nchini Somalia.
Makomando wa
Israel
wajitosa
Katika hatua
nyingine makomandoo wa Israel jana waliwazidi nguvu wanamgambo wa
Somalia na kufanikiwa kuwakomboa mateka waliokuwa wakishikiliwa na manamgambo
hao.Milio ya risasi ya
hapa na pale ilisikika huku maofisa usalama wa Kenya wakisema walikuwa wakijaribu
kuwaua au kuwateka washambuliaji waliobakia na kumaliza umwagaji damu uliodumu
kwa saa 28 katika ukumbi wa soko wa Westgate.
“Makomandoo wa Israel wamekwisha wasili na sasa w a n a w a o k
o a ma t e k a n a waliojeruhiwa,” chanzo cha habari cha usalama cha Kenya
kiliiambia Shirika la Habari la Ufaransa- AFP. Wizara ya Mambo ya
Nje ya Israel
ilikataa kuthibitisha au kukanusha kwamba vikosi vyake vilihusishwa
POLENI WANAKENYA.
ReplyDeleteAm very sorry what happen in Kenya since large number of people lost life due to terrorists.let us pray for them so that our God could rest them in peaceful way.others should remain in tolerant spirit during this hardship and difficult period.Amen.
Delete