KINSHASA, DRC
RAIS Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo
(DRC), amesema hayupo tayari kuruhusu mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na
waasi, eneo la Afrika ya Kati.Alisema mapigano hayo yanaweza kuligawa
Taifa hilo
ambapo jeshi la nchi hiyo litaendelea kulinda amani na kuchukua hatua kwa
yeyote anayejaribu kuivuruga.
Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya
Ujerumani (DW), Rais Kabila aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa
mwishoni mwa wiki mjini Kinshasa
wakati akifungua mkutano wa maridhiano ya kitaifa nchini humo.
Hata hivyo, mkutano huo ulisusiwa na
baadhi ya vyama vya siasa kutoka upinzani ambapo mazungumzo ya amani kati ya
Serikali ya Congo
na waasi wa M23 yanatarajiwa kuanza leo.Hali hiyo inatokana na ongezeko la vurugu karibu na eneo la mpaka wa Congo na nchi jirani ya Rwanda ambapo
kundi la M23, lilianzisha uasi Mashariki mwa Kongo na kufanikiwa kuudhibiti Mji
wa Goma kwa muda mfupi
Siri ya waasi imefichuka. Rais Kabila kaza boot. Utashinda!
ReplyDelete