Na Grace Ndossa
WAZIRI wa Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo, F e n e l l a Mu k a n g a r a , amewataka waandishi wa habari
kujiendeleza kielimu ili sheria itakapopitishwa waweze kuwa na vigezo
vinavyotakiwa.Hayo alibainisha mwishoni mwa wiki
mjini Dodoma alipokuwa anazungumza na kikundi
cha waandishi wa habari (Habari Group) na kueleza kuwa sheria itakuwa inawabana
kama watakuwa hawajafikia vigezo.
A l i s e m a k u w a n i vyema
waandishi wa habari wakaongeza elimu waliyonayo kwani walio wengi hawajafikia
kiwango kitakachowekwa katika sheria ya habari."Nasisitiza mjiendeleze kielimu
ili kufikia vigezo vitavyopitishwa na sheria ya habari kwani elimu ni muhimu na
mjitahidi kuandika habari kwa umakini na usahihi," alisema Mukangara.
Pia alisema katika Wizara ya Habari
yangu ina fursa nyingi za vijana,hivyo mnatakiwa kujitokeza na kutumia fursa
zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.Alisema vijana wanaweza kujiunga kwenye
vikundi na kufika katika wizara hiyo kuelezea kitu wanachotaka k u f a n y a i
l i wawe z e kusaidiwa na mikopo, kwani ipo ambayo mtu atarudisha kwa riba
nafuu.Hata hivyo, alisema kuwa vijana wengi wana fursa nyingi hivyo ni muhimu
wajiunge kwenye vikundi kwani fursa za kilimo kwanza zipo.
No comments:
Post a Comment