Na Rashid
Mkwinda, Mbeya
AS ILIMIA 4 0 y a mapato ya Mkoa wa
Mbeya yanatokana n a s h u g h u l i z a kiuchumi katika sekta za
viwanda,biashara na kilimo huku asilimia 80 ya wakazi wake wakijishughulisha na
kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Akizungumza na
timu ya waandishi wa habari waliokuwa katika mafunzo ya habari za Biashara na
Uchumi, Mkoa wa Mbeya, Mchumi wa Mkoa, Rukia Manduta, alisema asilimia 40 ya
mapato hayo yanatokana n a uwe k e z a j i k a t i k a viwanda, madini,
biashara na usafirishaji.
Alisema kuwa
serikali inaendelea kuimarisha miundo mbinu katika barabara ambapo Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Songwe umeongeza chachu kwa wakulima kupata fursa ya
kusafirisha mazao ya kilimo kama vile maua
mboga mboga na matunda.
Alisema uwekezaji
katika sekta ya utalii umeendelea kuimarika kwa Bonde la Ihefu lililopo
wilayani Mbarali kuingizwa katika Hifadhi ya Taifa ilhali Ziwa Rukwa lililopo
wilayani Mbozi na Chunya na Ziwa Nyasa lililopo katika wilaya ya Kyela
yanasaidia pato la mkoa katika sekta ya usafirishaji na uvuvi.
Kwa upande wake
Ofisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya, Joseph Semu alizitaja baadhi ya changamoto
zinazochangia kukosekana kwa wawekezaji wakubwa kuwa ni pamoja na uhaba wa
maeneo na kwamba kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
ameunda timu ya watu sita ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Semu alisema kuwa timu iliyoundwa na
mkuu wa mkoa imechukua wataalamu kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo
mkoa wa Mbeya(SIDO),TCCIA,TIC, Mhadhiri wa chuo kikuu Mzumbe, na wataalamu
wawili kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Awali, akizungumza na Katibu Tawala
msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha, mkufunzi wa mafunzo ya habari za
Biashara na Uchumi kwa waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya, Mnaku Mbani alisema
kuwa lengo la mafunzo hayo kwa wanahabari ni kuwajengea uwezo wanahabari
kuandika habari za biashara na uchumi.
Alisema fursa hiyo kwa wanahabari imelenga kuibua changamoto
za kiuchumi kwa Mkoa wa Mbeya kwa nia ya kupatiwa ufumbuzi na kutangaza fursa
za uwekezaji zilizopo mkoani humo.
No comments:
Post a Comment