05 September 2013

MNIGERIA ABAMBWA NA DAWA ZA KULEVYA DAR



Ester Maongezi na Zourha Malisa
RAIA wa Nigeria, Anthonia Ojo (25), amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam akiwa na kete 99 za dawa za kulevya. Tukio hilo lilitokea jana saa 7.40 wakati raia huyo akijiandaa kusafi ri na Ndege ya Shirika la Ethiopia kupitia Addis Ababa, kwenda Paris, nchini Ufaransa, Italia na kasha arudi nchini kwake, Nigeria.
 Kutokea kwa tukio hilo kulithibitishwa na Mkuu wa Upelelezi katika Viwanja vya Ndege, jijini Dar es Salaam Hamadi Hamis, wakati akizungumza na gazeti hili. Alisema mtu huyo alikuwa amehifadhi dawa hizo kwenye makopo ya poda za watoto na kwenye shampuu na kasha kuhifadhiwa kwenye begi zake adhaa za safari. 
Alisema wakati wa ukaguzi ndipo askari polisi na Maofi sa wa Usalama waliokuwepo uwanjani hapo waliweza kumbaini na kasha kuanza kumfanyia upekuzi wa kina na kugundua ana dawa hizo. Aliongeza kuwa baada ya ukaguzi, walibaini makopo hayo yametobolewa kitaalam na kisha ndani yake kuingizwa kete hizo za dawa za kulevya 99. 
Hamis alisema bado wanaendelea kumshikiliamwanamke huyo na baada ya uchunguzi kukamilika atafi kishwa kwenye vyombo vya kisheria. Mmoja wa wafanyakazi katika uwanja huo wa ndege (jina tunalo) alisema sio mara ya kwanza raia huyo wa Nigeria kupita uwanjani hapo.

2 comments:

  1. Tungekua na utaratibu wa kuwapa motisha maafisa wanaokamata wahalifu pale uwanjani, hasa wa madawa , pembe au madini, tudhibiti aibu hii

    ReplyDelete
  2. Kwamba huyo Mwana mama amekuwa ni mteja wa kusafiri na kupita hapo Mara kwa Mara?hilo ni jibu tosha kwamba kumbe hao maofisa wanawafahamu wote maharamia wanaoshuhulika na kadhia hii ya madawa hivyo walisubiri huyu BABA mkwe acharuke hatakutimua baadhi ya maofisa ndo waanze kuchemka? Hao maofisa wanawajua wote wahusika na njia zote wanazozitumia,mzee wangu mwakyembe em wape kiminyio zaidi wanao na wajukuu zako huenda wakapona kwa maathiriko ya unga.

    ReplyDelete