Na Daud
Magesa, Mwanza
RAIS Jakaya Kikwete
jana amewa o n g o z a mami a y a waombolezaji katika mazishi ya Askofu Mkuu wa
Kanisa la The Evangelical Assemblies Of God Tanzania (EAGT ) Moses Kulola.Mbali
na Rais Kikwete mazishi hayo ambayo yalifanyika jana katika kanisa la Kalvary
EAGT Bu g a n d o J i j i n i Mwa n z a , yalihudhuriwa na Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa, Mke wa Rais, Salma Kikwete,Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt.
Wilbroad Slaa na mkewe Josephine Mshumbusi, Katibu Mkuu wa ADC, Lucas Kadawi
Limbu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, Wakuu wa wilaya mbalimbali,Wabunge
wa CCM na Chadema wakiwemo, Maaskofu na wachungaji wa kanisa hilo.Akitoa
salamu za rambirambi kwa wafiwa na waombolezaji waliohudhuria katika mazishi hayo,
Rais alisema alipokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Marehemu
Askofu Kulola.
Alisema
marehemu alikuwa mtu mwema, muungwana ambaye alithamini sana watu na kuwapenda
na hakuwa mtu wa kujikweza kama wanasiasa, bali alitumia muda mwingi kutumikia
watu na hakuwa mbaguzi.
Rais
alimwelezea Marehemu Askofu Kulola kuwa mahubiri yake yalihimiza upendo na
kuhimiza watu kuishi bila kujali mahali walikotoka, rangi zao, makabila yao
wala dini zao.
“Angekuwa hana sifa
hizo asingekuwa rafiki yangu. Mimi si Msukuma, si Mkristo, wakati niko Ikulu
alikuja kwangu na mama akaniambia amekuja kukuombea pamoja na nchi yetu kupitia
kwako. Mungu atakuwezesha, kweli alikuwa mtu shupavu na mkweli,”alisema Rais
Kikwete na kuongeza;
“Alikuwa mchungaji
mwema wa kondoo wa Bwana na ni vigumu kuamini. Katangulia mbele ya haki nasi
tutafuata kwa njia hiyo hiyo. Tumshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kuishi naye
duniani kazi yake haina makosa.”
Aliwataka
waombolezaji na waumini kuyaendeleza mazuri aliyoyasimamia na kuyadumisha mema
a l i y o y a h u b i r i n a kuyaendeleza, tukiyafanya hayo hata machozi yetu
yatakuwa na maana mbele za Mungu.
Awali katika Ibada ya
mazishi iliyoendeshwa na Askofu Mkuu Msaidizi wa EAGT, Asumwisye Mwaisabila,
alisema marehemu alikuwa mcha Mungu aliyejitolea kuwaleta watu kwa Yesu.Alisema
na kuhoji atapatikana kijana gani wa kumuiga marehemu huyo kutokana na
alivyojitoa kufanya kazi ya Mungu.
No comments:
Post a Comment