04 December 2013

OFISI YA CHADEMA YACHOMWA MOTO



Na Queen Lema, Arusha
Katika hali isiyo ya kawaida, watu wasiofahamika wamevamia ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya kaskazini iliopo mkoani Arusha na kuichoma moto uliosababisha haraka kubwa.

Akizungumza na Majira, Katibu wa kanda hiyo ambaye pia ni Katibu wa CHADEMA mkoani humo, Amani Golugwa, alisema tukio hilo lilitokea jana asubuhi katika ofisi hizo zilizopo eneo la Ngarenaro, mjini humo.
Alisema watu hao waliingia katika ofisi hizo baada ya mlinzi wa zamu kutoka hivyo walivunja kioo kikubwa, kupanda katika dari la ofisi, kutafuta chumba kinachohifadhi nyaraka muhimu na kuwasha moto"Wakati wanawasha moto, ghafla uliweza kulipuka hivyo lengo halisi halikuweza kutimia kwa haraka badala yake walishuka na kuanza kukimbia wakati jengo letu likiwa linateketea moto.
"Baada ya watu hao kuona hawawezi kuchoma chumba hicho, walitengeza shoti kubwa ya umeme iliyosababisha vyumba vya choo na bafu, kuunguwa na hatimaye walishuka wakiwa wanakimbia wakati moto ukiendelea kuwaka."Hatuwezi kusema walikuwa na lengo la kuchoma chumba hiki ambacho kinahifadhi nyaraka muhimu, inavyoonekana lengo lao ni kupoteza ushahidi wa vitu mbalimbali," alisema.
Katika hatua nyingine, Golugwa alisema tukio hilo linaonesha kuna baadhi ya watu ambao wanatumia muda na fikra nyingi kuwawinda viongozi wa CHADEMA.Aliwataja baadhi ya viongozi wanaowindwa ili wajeruhiwe kuwa ni pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Goodbless Lema na Mwenyekiti wa Wilaya, Ephata Nanyaro
"Hadi sasa tunawahisi watu watatu katika sakata hili, tayari tumeripoti polisi ili waanze upelelezi wao lakini jengo letu tumeliwekea ulinzi mkubwa sana... kumbukumbu zote zipo ingawa hadi sasa hatujui hasara tuliyoipata," alisema.

3 comments: