Na Rehema Mohamed
MKURUGENZI wa Mashtaka Nchini (DPP) amemfutia mashtaka raia wa
Kenya, Joshua Muhindi (22) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kumteka na kumdhuru
Dkt.Steven Ulimboka na kisha kumfungulia shtaka jipya la kutoa taarifa za uongo
kwa Jeshi la Polisi.Mshtakiwa huyo jana alifikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu
Waliyarwande Lema ili upande wa mashtaka
ueleze mustakabali wa kesi hiyoHata hivyo, Wakili wa Serikali Beata Kitau
aliieleza mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya
mshtakiwa hivyo anaomba kuliondoa chini ya kifungu 91(1) cha Mwenendo wa Makosa
ya jinai (CPA).
Hakimu Lema
alikubaliana na hoja hiyo na kuifuta kesi hiyo ambapo hata hivyo baada ya
kutoka mahakamani mshtakiwa huyo alikamatwa tena na polisi na kisha kupandishwa
kizimbani mbele ya Hakimu Aloyce Katemana.
Akiwa mbele ya
hakimu huyo, wakili wa serikali Tumaini Kweka alimsomea shtaka la kutoa taarifa
za uongo kinyume na kifungu 122 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa, Julai 3, 2012 Kituo cha Polisi Oysterbay mshtakiwa huyo
(Muhindi) alitoa taarifa za uongo kwa ofisa wa Polisi kwamba yeye na wenzake
wasiojulikana walimteka na kumjeruhi Dkt. Ulimboka wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa huyo
alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa
shauri hilo umekamilika na wanaomba tarehe ya kutajwa ili wamsomee maelezo ya
awali.
Baada ya kusema hivyo, Muhindi aliiomba
mahakama impe dhamana na kwamba alikuwa na wadhamini, lakini hata hivyo upande
wa mashtaka ulipinga kwa madai kuwa mshtakiwa ni mgeni na hana makazi maalumu
hivyo itakuwa vigumu kumpata.
Hata hivyo, Mkenya huyo aliibuka na kudai
kuwa amekaa gerezani toka Julai 13, 2012 lakini upande wa mashtaka umeshindwa
kuthibitisha mashtaka dhidi yake hadi jana wanamfungulia mashtaka mengine.
Alidai kuwa jambo la kumrudisha yeye
gerezani linalenga kumpoteza ili kutuliza umma na Bunge na kwamba akirudi
gerezani atagoma na kufanya maandamano.
“Hawa watu wanataka kunipoteza mimi kijana
mdogo wa miaka 22, mashtaka wanayonishtakia si ya kweli naumia sana hakimu,
nikirudi gerezani nitafanya maandamano na kugoma, hakimu utapata taarifa,”
alidai Muhindi.
Kwa upande wake Hakimu Katemana aliutaka
upande wa mashtaka kuwasilisha mahakamani hapo hati ya zuio la dhamana kama
wanataka mshtakiwa huyo asidhaminiwe kwa sababu shtaka analokabiliwa nalo
linadhaminika.
Alimweleza mshtakiwa huyo kuwa atakuwa nje
kwa dhamana ikiwa atatimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili kutoka taasisi
zinazotambulika watakaosaini bondi ya sh. milioni tano na pia awasilishe
mahakamani hapo hati zake za kusafiria.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu
NADHANI SASA POLISI WANALO JINA LA MTU AU WATU WALIOMTEKA ULIMBOKA
ReplyDeletedanganya toto hiyooooooo!!!!!!!!!!!!!.........
ReplyDeleteKwanini hao mapolisi wa Tanzania wanazidi kubobea kusema uwongo! Kwani hawajui mhusika wa unyama aliofanyiwa Dr. Ulimboka? Hebu acheni kuliaibisha taifa na hizi "danganya toto" za kila siku. Au hapo ndo utaalamu wenu umefikia! Hamuwezi kwenda zaidi!!!
ReplyDeleteKESI IKISHAANZA KUZUNGUMZIWA MAGAZETINI NI KUHARIBU MWENENDO WA KESI HAKUNA HAKI TENA KAMA BUNGENI HAWARUHUSIWI KUZUNGUMZIA MASUALA YA MAHAKAMANI MBONA MAGAZETI HAWAZUILIWI KATIBA MPYA IWAFUNGE MIDOMO
ReplyDeleteThis is one of the reasons to, why our Country is now Politically Unstable. Serikali isome alama za nyakati
ReplyDelete