Na Mwandishi Wetu
KAMATI Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajia kukutana kuanzia Agosti 20 hadi 25, mwaka
huu kwa ajili ya kutoa mapendekezo ya mchakato wa Katiba Mpya.Kwa mu j i b u
wa t a a r i f a iliyotolewa jana Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema vikao hivyo vya kitaifa
vitapokea maoni na mawazo ya wanachama wa CCM.
" Vi k a o
v i t a y a p i t i a n a k u y a u n g a n i s h a ma o n i y a wa n a c h ama
kwa a j i l i y a kuyawakilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya... CCM
kwa ujumla tunaridhishwa na jinsi mchakato wa mabaraza unavyoendelea, ukiacha kasoro
za hapa na pale zinazoendelea kujitokeza," alisema.
Alisema kuwa,
CCM inapenda kusisitiza kuwa haiwezekani kutengeneza katiba itakayo furahisha
watu wote kwa wakati mmoja, hivyo kuvumiliana na kuheshimiana katika mchakato
huo ni suala la msingi sana.
"Mfano,
CCM ina mawazo tofauti pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza kwenye
suala la Muundo wa Muungano.
"Wakati
rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM tunapendekeza muundo wa
serikali mbili, lakini hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye
mawazo tofauti na yetu," alisema.
Alisema
kuwa, kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazojaribu kuonyesha kama vile kuna
mvutano kati ya tume na CCM na wengine wenye mawazo tofauti na CCM lakini hali
hiyo inajaribu kujengwa kwa nguvu ambayo si ya kweli.
CCM sio baba wala mama wa Tanzania hivyo waache kuyumbisha Taifa na kulefa vurugu. Kama ni vikao wakakae na uongozi wa wizara ya elimu ili kutafakari jinsi ya kuborssha elimu Tanzania. Haya maoni mnayotafuta kwa wanachama ya nini? Wapeleke kwenye uongozi wa tume ya katiba. Kwanza mnawakatisha tamaa wahusika na kupoteza muda na fedha nyingi. Kuna mambo ya muhimu nchini hayafuatiliwi. Hii sio dili jamani. Mungu ilinde TZ.
ReplyDeleteKILA CHAMA KINA FURSA YA KUFANYA HIVYO WALA HAKUNA CHAMA KILICHOFUNGWA MDOMO AU KUWEKWA PINGU KILA CHAMA KITUMIE RASILIMALIWATU ILIYO NAYO KUTETEA YALE WANAYOONA YANA TIJA KWA KIZAZI CHA SASA NA KIJACHO KAMA HUNA MCHANGO WENYE TIJA NYAMAZA KATIBA NI YA KIZAZI CHA KESHO ,KESHO KUTWA NA MTONDO GOO TUACHE UFINYU WA AKILI NA UBINAFSI SI AJABU HIYO KATIBA ISIWE NA MANUFAA YOYOTE KWAKO
ReplyDeleteNdugu yangu Jaji Warioba alishaonya vyama vya siasa visiwahadae wananchi na kuwanywesha matakwa ya wanasiasa badala yake raia watoe maoni wanayoona yanalenga maslahi ya maisha yao na mazingira yao. ACHA JAZBA NA CHUKI ZA KUPANDIKIZWA
DeleteInaonekana hata wewe hauelewi maana ya warioba. taasisi maana yake nini kwani ccm siyo taasisi. lkn kama ni taasisi inapaswa kufanya hivyo hata wewe ukiwa ndani ya taasisi yenu ya cdm pelekeni maoni labda kama ni mpiga debe wa chadema.
DeleteCCM inatapatapa!Hii nchi sio ya kwenu ni ya raia wote na wa itikadi zote.Imewalisha sumu makada katika mabaraza ya katiba kusimamia matakwa ya CCM na kuacha yale yaliopendekezwa na wananchi.
ReplyDeleteWaachwe wananchi waamue serikali wanayoitaka bila kuburuzwa.Kama rasimu imetoa yale yaliopendekezwa na wananchi vipi CCM itokwe mishipa kuyapinga na kuyadharau na kuwakebehi wale waliotoa maoni yao.Hii INAONYESHA CCC WAMEISHIWA SERA na wanataka kutumia nguvu na kila namna kuhakikisha ya kwao wanayoyataka ndio yawe ya wananchi wote.HATUKUBALIII!!!!!
kwani makada siyo wananchi? yaelekea hata shule yako ndogo huelewi maana ya wananchi.
Delete