30 August 2013

MTIHANI KWA POLISI:MATAPELI STENDI YA MABASI UBUNGO

  • WAJIFANYA USALAM WA TAIFA,POLISI,UHAMIAJI
  • WADAIWA KUTOA VIZA KWA WAGENI SH.20,000
 Baadhi ya matapeli wakiwa wanajipanga kwa ajili ya kumtapeli mwanamke ambaye hakufahamika jina (aliyejifunga ushungi) akitokea mkoani Kigoma na kushuka Dar es Salaam juzi katika basi la Adventure.

 Mmoja wa matapeli ambaye hutumika kama dereva teksi isiyo rasmi
Na Waandishi Wetu
HALI si shwari ndani ya kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT), Dar es Salaam, kutokana na utapeli mkubwa unaowafanywa na watu wanaojifanya waajiriwa wa Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na Uhamiaji.Utapeli huo unafanywa kwa abiria wanaoingia jijini humo, wakitokea mikoa ya mbali kama Kigoma, Bukoba na nchi jirani za Kenya, Uganda, Bunjumbura na Malawi
.Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa kasi ya watu wanaotumia majina ya taasisi hiyo kufanya utapeli, imekuwa ikiongezeka katika maeneo tofauti ya jiji hilo.Majira baada ya kupata taarifa za utapeli huo wiki mbili zilizopita, lilituma kikosi kazi cha waandishi walioshinda katika stendi hiyo ili kubaini mbinu chafu ambazo zimekuwa zikifanywa na watu hao kujipatia pesa.
Katika uchunguzi huo, imebainika mbali ya watu hao kufanya kazi ya ukaguzi wa mabegi ya abiria ili kufanya utapeli, pia wamekuwa wakijifanya mawakala wa baadhi ya mabasi yanayokwenda masafa marefu kwa kuuza tiketi feki.Jambo la kushangaza, baadhi ya wafanyakazi wa mabasi hayo, wamekuwa wakishirikiana na matapeli husika kwa kupeana ishara pale mabasi hayo yanapofika kituoni ili kuwafahamisha abiria waliobeba mizigo mikubwa.
Chanzo chetu cha habari katika stendi hiyo, kilidai matapeli hao wana mtandao mkubwa (ambao ulishuhudiwa na waandishi wetu), ambao baadhi yao, hutoa viza za kusafiria kwa sh. 20,000 ambazo abiria akifika nazo mpakani, hukaguliwa na kuonekana za halali."Biashara hii hufanyika kila siku kwa usiri mkubwa lakini wapo baadhi ya askari polisi hapa Ubungo, wanashirikiana na hawa matapeli kufanikisha uhalifu wao," kilisema chanzo hicho.
Alisema abiria wenye mizigo kutoka mikoani na nje ya nchi, wamegeuzwa mradi wa matapeli hao. Kikosi kazi cha Majira kiliwashuhudia baadhi ya matapeli hao wakiwa wamevaa vizuri hivyo kuonekana watanashati kumbe wahalifu.
 Mazingira ya Utapeli
Baada ya mabasi hayo kuingia stendi, matapeli hao hulisogelea basi husika wengine wakijifanya Maofisa Usalama, Polisi na Uhamiaji ambao huingia ndani ya mabasi hayo na kufanya ukaguzi kabla abiria hawajashuka.Waandishi wetu walishuhudia dada mmoja aliyeshuka katika basi la Kampuni ya Advernture akiwa na mizigo kutoka Kigoma, akitapeliwa na watu hao kwa kulazimishwa kuingia kwenye teksi bubu (namba tunazo) na kuondoka naye.
Uchunguzi umebaini kuwa, matapeli hao wanatumia magari maalumu ambayo hupaki ndani ya stendi hiyo na kufika eneo hilo kuanzia saa moja asubuhi na mabasi hayo yanapoingia, hupeana ishara mbalimbali.Kikosi kazi kilichokuwa kikiwafuatilia matapeli hao, kilibaini mtandao huo pia unahusisha wanawake ambao nao hujifanya maofisa wa taasisi hizo (Usalama, Polisi na Uhamiaji).
Juzi baada ya matapeli hao kubaini kuna watu wanaowafuatilia, walilazimika kupotea kwa muda na kurudi jioni wakiwa makini kuwatafuta waandishi wetu ambao baada ya kubaini hali hiyo, waliondoka eneo hilo bila kushtukiwa.Hitimisho la uchunguzi huo kwa siku ya jana, kikosi kazi cha Majira kiliwashuhudia zaidi ya matapeli 10 wakiwa wamejigawa katika makundi matatu, wakiitana kwa majina na kugawana fedha walizofanikiwa kumwibia abiria.
Mtandao huo unafanywa na watu ambao umri wao ni mkubwa, ambapo waandishi wetu walishuhudia mzungu mmoja raia kutoka nchini Canada, Bi. Hayley Wade, akimwaga chozi baada ya kutapeliwa sh. 150,000 wakati akitaka tiketi ya kwenda Uganda.Kikosi kazi kilizungumza na Bi. Wade muda mfupi baada ya kutapeliwa na kusema baada ya kufika kituoni hapo, alipokelewa na watu waliojifanya wafanyakazi wa Kampuni ya Falcon na kumkatia tiketi kutoka Dar es Salaam hadi Kampala.
Alisema baada ya kupewa tiketi, walimwambia asubiri basi lakini alijikuta akikaa muda mrefu kituoni hapo bila kuliona basi hilo hivyo alitaka kurudishiwa fedha zake.Waandishi wetu waliishuhudia tiketi hiyo ambayo ilikuwa haijaaandikwa kiasi cha pesa alizolipa kwa safari hiyo na kubaini mzungu huyo tayari ametapeliwa mchana kweupe.
"Ni l i p o o n a n a c h e l ewa , niliomba nirudishiwe fedha zangu, niliambiwa mtu niliyempa pesa hayupo hivyo ni vigumu kurudishiwa fedha zangu," alisema Bi. Wade.Wakati waandishi wakizungumza na Bi. Wade, alitokea mfanyakazi mmoja wa kampuni hiyo, kumtaka aoneshe tiketi na kumwambia asubiri baada ya saa moja lakini mzungu huyo alisema hawezi kusubiri kwani muda unaenda na yeye hajui hatima yake hivyo alitaka kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akakate tiketi ya ndege.
"Ninachotaka ni pesa zangu niende Uwanja wa Ndege...sitaki tena kusafiri na basi, naona muda umeenda na safari hakuna," alisema Bi. Wade mbele ya waandishi akimwambia mfanyakazi wa kampunih iyo.Baada yamuda, alitokea mtumwingi ne a liyedai na yenimfa nyakaziwakampunihiy o, kumc hukuaBi. Wade nakwendanayepemben i ambapoa lim rudishia sh.90, 000ambayo haikujul ikana ilito kawap i ndipomzunguhuyoakapandateksi nak uondok a.Wakati Bi. Wad eakiwakwenye teksi,alis ikikaakisemaakiru di nyumb anikwao , atazungu mzanavyombovyahaba rinchin ihumo ili kuwe ka w aziut apeliu liopoTanzania



Mkuu wa Kituo
Ma jiralilimt afutaMkuuwaKituocha PolisiUbung o, amb aye alid ai k utokuwanata arif azozotejuuyamatapel i ha onak uahidi kulifuatilia suala hilo kuanzia jana.
RPC Kinondoni
KamandawaPolisi MkoawaKinondoni, Cam iliusWambu ra, alipo ulizwakuhusian anautapeli huoalikiri kuwepok wa tatizohilonatayaribaadhi ya matapeli wam eka matwa .
"Kunamatapeli wanaoj iita Maofisa Usalama, PolisinaUhamiaji, t umejipan gailikukomeshavit endohi vi, tumewaka matasita nabadotutaendeleakuwa sakawen gine," alisemaKamandaWamb ura.Alion geza kuwa , hivisasakuna mat apeliwengi ambao habari zaozimer ipotiwakatikav yombovyahabarinakuto a witokwaabir ia, was iku balikupeku liwa hovyoba dalayakew aon eshwekielele zokama kwel imtuhusika ni askari ambapo eneo hilo pia kuna Kituo cha Polisi hivyo ukaguzi ukafanyike huko.
TABOA wazungumza
K waupa nde wake,Ka tibuMkuuwaCha machaW amil ikiwa M abasi yaen dayo Miko ani(TA BOA), Bw.EneaMrutualis emakituonihapokuna matap elisug una waowalis hatoataarifaras mikw ab arua wal iyompaaliyeku waKamandawaPolisi Mkoawa Kipolisi Kinondo ni, Cha r lesKeny elalakini hakunahatuazo zoteam bazozilichukuliwa.
"Hivi karibuni tumeandika barua nyinginekwendakw aKamandaWambura kumwele zaha li hii lakini hatuja rudishi wam ajibu. ..hapastendiUbungokun amambomengi yanafany ika."Watuwanajifanya Maofisa wa Po lisi nah atawakikamatwa, baada yadakik a10 wameachiwahivyotunaom bapo lisiwote walio kokatikakitu ohiki kwazaidiya miaka10wahamish wenaku wekwa wapya ili kudhibitihali hii ,"alisemaBw. Mrutu.
Alisemahadi sasa hakuna derevayeyo teal iyek amatwanakuchuku liwa hatua kwa kushirikiana na mtandao wa matapeli,piakunama basi me ngi yanayos afi risha abiria bila leseni na baadhi ya kampuni hazina uanachama wa TABOA hivyo inakuwa ngumu kuyadhibiti mabasi yote

2 comments:

  1. TATIZO NI AJIRA SASA WATU WANABUNI JINSI GANI YA KUJIKIMU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ukosefu wa ajira isiwe kisingizio cha kufanya uhalifu ni tabia tu mbona hata wenye ajira wanawatapeli watu?

      Delete