30 August 2013

ASKOFU KULOLA AFARIKI DUNIA



 Na Mwandishi Wetu
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God nchini (EAGT), Dkt. Moses Kulola (83), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.Taarifa zilizolifikia gazeti hili, zinasema Askofu Kulola amefariki jana saa sita mchana katika Hospitali ya Army, iliyopo Msasani, Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa.

Akizungumzia na gazeti hili juu ya kifo hicho, Mchungaji wa Kanisa la EAGT City Centre, Florian Katunzi, alisema kifo cha Askofu Kulola, huo ni pigo kubwa si kwa familia na waumini wake pekee bali kwa Watanzania wote.
Alisema mbali ya kuumwa muda mrefu (bila kutaja ugonjwa uliokuwa ukimsumbua), alisema uzee nao umechangia kifo chake na aliwahi kupelekwa nchini India kwa matibabu.Aliongeza kuwa, Askofu Kulola anatarajiwa kuzikwa wiki ijayo nyumbani kwao Bugando, mkoani Mwanza, ambapo msiba upo kwenye Kanisa la EAGT, Temeke.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinasema Askofu Kulola, alikuwa na wanachama wasiopungua milioni tano nchi nzima na kufungua matawi katika nchi za Zambia na Malawi.Askofu Kulola amehubiri neno la Mungu kwa zaidi ya miaka 60 hivyo ataendelea kukumbukwa kwa miujiza aliyokuwa akiionesha kwa waumini wake ikiwa ni harakati zake za kuwakomboa wanadamu.

3 comments:

  1. Tumeondokewa na mtu aliekuwa na wito kbwa sana katika medani ya Injili.ni huzuni kbwa sana lakini kibinadamu.Tulipewa Kulola na sasa amelala kwa hiyo sisi tuliobaki tufuate aliyokuwa akituhubiria mnazi mmoja,kidongo chekundu na temeke hapa dar.dvd zipo za 1996-2001 haziuzwi ni bure.Nnko documentarist wa injili ya Kulola 1996-2001

    ReplyDelete
    Replies
    1. MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEN.

      Delete
  2. Kwa heri Baba kwaheri Mzee uliye muhubiri Yesu pasipo kuonea haya Injili.

    ReplyDelete