Na
Mosi Mrisho
USAILI wa
waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board), ulitarajia kukamilika jana.Kwa mujibu wa Ofisa Habari
wa shirikisho hilo,
Boniface Wambura, Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu
Mbwezeleni ilianza usaili juzi ambapo matokeo ya usaili yanatarajiwa kutangazwa
kesho.
Alisema kati ya Septemba 4
na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF itawasilisha
kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili, ili kujadiliwa na
kutolewa uamuzi na kamati hiyo."Vilevile kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni
kipindi cha kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo
ya maadili," alisema Wambura.Alisema
kwa watakaokata rufaa wanatakiwa kuambatanisha na ada ya rufaa kwa Katibu Mkuu
wa TFF, kabla ya saa 10 jioni ya Septemba 6 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment