Na Eliasa
Ally, Iringa
KAMPUNI ya Mkwawa Hunting Safari
imeahidi kuisaidia Jumuiya ya Matumizi Bora ya Mali Hai ya Tarafa ya Idodi na
Pawaga (MBOMIPA) mbinu za kufanikisha kukabiliana na ujangili wa uwindaji
haramu wa tembo na wanyamapori wengine.Uwindaji
ambao huwa unafanywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika
eneo lao la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa.
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo, Hamed Huwel aliyasema hayo jana kwenye kikao cha Halmashauri
Kuu ya MBOMIPA kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati alipokuwa
akijitambulisha katika mkutano wa wajumbe wa halmashauri hiyo.
Pia
katika kikao hicho wajumbe wa MBOMIPA walikuwa wanapitia mkataba wa mwekezaji
huyo.Huwel
alisema kuwa, pamoja na kuwasaidia katika kazi ya kupambana na ujangili pia
atavisaidia vijiji vyote 21 ambavyo vinaizunguka Hifadhi ya Ruaha kuchimba
visima vya maji, kutengeneza barabara zinazokwenda kwenye vijiji husika pamoja
na kuchimba mabwawa makubwa manne.
"
Lengo ni ili kuwawezesha kunywa maji wanyamapori ambao wanapata tabu...kupata
maji katika kipindi cha kiangazi," alisema.Aliongeza
kuwa, Jumuiya hiyo ya MBOMIPA inayoshughulika na Uhifadhi wa Maeneo ya Hifadhi
ya Wanyamapori ya Jamii (WMA) nje ya mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha,
wilayani Iringa, wanyama walioko katika eneo hilo wanatoka ndani ya hifadhi
hiyo na Hifadhi ya Mikumi ambapo alisema kuwa Mkoa wa Iringa una utajiri mkubwa
na endapo watautumia vizuri wananchi wanaweza kupata maendeleo makubwa zaidi.
"Ninyi
mnajua na Watanzania wanajua kwamba wanyama katika eneo lenu wanazidi kupungua
sio kwa sababu shughuli za utalii endelevu ndizo zinazosababisha, lakini ni kwa
sababu tumeshindwa kukabiliana na majangili, n i n awa omb a wa j umb e wa
MBOMIPA na wananchi wote kwa pamoja tuendelee kushikamana ili kulinda
rasilimali zetu hizi," alisema Huwel.
Alisema, ili
kukabiliana na ujangili katika eneo hilo kunahitajika doria ya hali ya juu na
kwamba yeye yupo tayari kushirikiana na wanajumuiya kufikia azma hiyo ya
kuwadhibiti majangili ambao wanaendelea kuiba rasilimali za Watanzania.Pia alisema kuwa,
atatoa doria katika Hifadhi ya Ruaha ambapo barabara zote zinazoingia hifadhini
na zile ambazo zinapita ndani ya hifadhi hiyo amezitengeneza kwa gharama zake.
Akimshukuru kwa
misaada hiyo, Mwenyekiti wa MBOMIPA, Phillip Mkumbata alisema wanahitaji
ushirikiano huo ili wanyama waliopo katika Hifadhi ya Ruaha waendelee
kuongezeka na watalii kuvutiwa.
Alisema, pia
wanahitaji kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja
na kambi za Lunda, Isele na ukanda wa Kinyangesi na Mkupule.
Alisema, doria
zinazoendelea kufanywa katika maeneo hayo zinaonesha kuwepo kwa alama za nyayo
za majangili na kuongeza kuwa wanao mkakati wa kuimarisha ulinzi katika eneo
hilo unalenga kuitikia wito uliotolewa na Serikali.Wito ambao unalenga
kuusaka na kuufikisha katika vyombo vya dola mtandao wa majangili wa meno ya
tembo bila kujali nafasi walizonazo katika jamii.
Aliongeza kuwa,
Mwekezaji wa Mkwawa Hunting Safaris pamoja na kutoa msaada wa kudhibiti
ujangili pia ametoa misaada mingine ya kuwachimbia wananchi visima vya maji na
kuwaondolea kero kubwa ya kutafuta maji."Kujenga nyumba
mbili za kuishi wahudumu wa zahanati pamoja na kuchangia katika sekta ya elimu
kwa kutoa madawati katika Shule ya Msingi ya Kitisi ikiwemo kujenga madarasa
mawili," alisema Mwenyekiti huyo.
Mkumbata alisema
kuwa, mwekezaji huyo pia amechimba visima vya maji tisa ya kutumia wa n a n c h
i n a k i l a k imo j a kimegharimu sh. milioni 15 hivyo jumla kuu ya fedha
ikiwa ni sh. milioni 135.S amb amb a n a k u j
e n g a nyumba mbili za walimu ambazo zimegharimu sh. milioni 30, kujenga
madarasa mawili yenye thamani ya sh. milioni 15 hatua ambayo inalenga kuziondoa
kabisa kero zinazowakabili wakazi wa Iringa.
Akiwa mkoani Iringa
hivi karibuni, Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
alisema kuanzia sasa watakaokamatwa au kugundulika kuwepo katika mtandao huo wa
majangili watatangazwa majina yao, wanakoishi, nchi wanazotoka na watafunguliwa
mashtaka kwa mujibu wa sheria za nchi.Aliwataja baadhi ya watu waliopo katika mtandao huo wa
ujangili kuwa ni pamoja na majangili, wahifadhi, maofisa wanyamapori, viongozi
wa Serikali, wasafirishaji, idara ya uhamiaji na baadhi ya watumishi wa vikosi
vya usalama nchini.
Hao akina huwel ni majangili wakubwa nani asiyejua ?? Leo hii mwizi anasema atajikamata ??
ReplyDelete