26 July 2013

MWEKEZAJI AJIPANGA KUWAUMBUA MAJANGILI



 Na Eliasa Ally, Iringa
KAMPUNI ya Mkwawa Hunting Safari imeahidi kuisaidia Jumuiya ya Matumizi Bora ya Mali Hai ya Tarafa ya Idodi na Pawaga (MBOMIPA) mbinu za kufanikisha kukabiliana na ujangili wa uwindaji haramu wa tembo na wanyamapori wengine.Uwindaji ambao huwa unafanywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika eneo lao la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hamed Huwel aliyasema hayo jana kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya MBOMIPA kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati alipokuwa akijitambulisha katika mkutano wa wajumbe wa halmashauri hiyo.
Pia katika kikao hicho wajumbe wa MBOMIPA walikuwa wanapitia mkataba wa mwekezaji huyo.Huwel alisema kuwa, pamoja na kuwasaidia katika kazi ya kupambana na ujangili pia atavisaidia vijiji vyote 21 ambavyo vinaizunguka Hifadhi ya Ruaha kuchimba visima vya maji, kutengeneza barabara zinazokwenda kwenye vijiji husika pamoja na kuchimba mabwawa makubwa manne.
" Lengo ni ili kuwawezesha kunywa maji wanyamapori ambao wanapata tabu...kupata maji katika kipindi cha kiangazi," alisema.Aliongeza kuwa, Jumuiya hiyo ya MBOMIPA inayoshughulika na Uhifadhi wa Maeneo ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jamii (WMA) nje ya mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, wilayani Iringa, wanyama walioko katika eneo hilo wanatoka ndani ya hifadhi hiyo na Hifadhi ya Mikumi ambapo alisema kuwa Mkoa wa Iringa una utajiri mkubwa na endapo watautumia vizuri wananchi wanaweza kupata maendeleo makubwa zaidi.
"Ninyi mnajua na Watanzania wanajua kwamba wanyama katika eneo lenu wanazidi kupungua sio kwa sababu shughuli za utalii endelevu ndizo zinazosababisha, lakini ni kwa sababu tumeshindwa kukabiliana na majangili, n i n awa omb a wa j umb e wa MBOMIPA na wananchi wote kwa pamoja tuendelee kushikamana ili kulinda rasilimali zetu hizi," alisema Huwel.
Alisema, ili kukabiliana na ujangili katika eneo hilo kunahitajika doria ya hali ya juu na kwamba yeye yupo tayari kushirikiana na wanajumuiya kufikia azma hiyo ya kuwadhibiti majangili ambao wanaendelea kuiba rasilimali za Watanzania.Pia alisema kuwa, atatoa doria katika Hifadhi ya Ruaha ambapo barabara zote zinazoingia hifadhini na zile ambazo zinapita ndani ya hifadhi hiyo amezitengeneza kwa gharama zake.
Akimshukuru kwa misaada hiyo, Mwenyekiti wa MBOMIPA, Phillip Mkumbata alisema wanahitaji ushirikiano huo ili wanyama waliopo katika Hifadhi ya Ruaha waendelee kuongezeka na watalii kuvutiwa.
Alisema, pia wanahitaji kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kambi za Lunda, Isele na ukanda wa Kinyangesi na Mkupule.
Alisema, doria zinazoendelea kufanywa katika maeneo hayo zinaonesha kuwepo kwa alama za nyayo za majangili na kuongeza kuwa wanao mkakati wa kuimarisha ulinzi katika eneo hilo unalenga kuitikia wito uliotolewa na Serikali.Wito ambao unalenga kuusaka na kuufikisha katika vyombo vya dola mtandao wa majangili wa meno ya tembo bila kujali nafasi walizonazo katika jamii.
Aliongeza kuwa, Mwekezaji wa Mkwawa Hunting Safaris pamoja na kutoa msaada wa kudhibiti ujangili pia ametoa misaada mingine ya kuwachimbia wananchi visima vya maji na kuwaondolea kero kubwa ya kutafuta maji."Kujenga nyumba mbili za kuishi wahudumu wa zahanati pamoja na kuchangia katika sekta ya elimu kwa kutoa madawati katika Shule ya Msingi ya Kitisi ikiwemo kujenga madarasa mawili," alisema Mwenyekiti huyo.
Mkumbata alisema kuwa, mwekezaji huyo pia amechimba visima vya maji tisa ya kutumia wa n a n c h i n a k i l a k imo j a kimegharimu sh. milioni 15 hivyo jumla kuu ya fedha ikiwa ni sh. milioni 135.S amb amb a n a k u j e n g a nyumba mbili za walimu ambazo zimegharimu sh. milioni 30, kujenga madarasa mawili yenye thamani ya sh. milioni 15 hatua ambayo inalenga kuziondoa kabisa kero zinazowakabili wakazi wa Iringa.
Akiwa mkoani Iringa hivi karibuni, Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema kuanzia sasa watakaokamatwa au kugundulika kuwepo katika mtandao huo wa majangili watatangazwa majina yao, wanakoishi, nchi wanazotoka na watafunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria za nchi.Aliwataja baadhi ya watu waliopo katika mtandao huo wa ujangili kuwa ni pamoja na majangili, wahifadhi, maofisa wanyamapori, viongozi wa Serikali, wasafirishaji, idara ya uhamiaji na baadhi ya watumishi wa vikosi vya usalama nchini.

1 comment:

  1. Hao akina huwel ni majangili wakubwa nani asiyejua ?? Leo hii mwizi anasema atajikamata ??

    ReplyDelete