27 February 2013

TCRA yaifungia Radio Imani miezi sita



Na Jesca Kileo

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA), kupitia kamati yake ya maudhui, imekifungia kituo cha Radio Imani kilichopo mkoani Morogoro na Radio Neema, mkoani Mwanza kwa
kipindi cha miezi sita kuanzia leo.


Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Walter Bugoya, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari.

Alisema kituo kingine cha Radio Clouds, kimetozwa faini ya
sh. milioni tano pamoja na kupewa onyo kwa kukiuka kanuni
na sheria za utangazaji za mwaka 2005.

Alisema wakati nchi ikiwa katika mchakato wa kufanya Sensa
ya Watu na Makazi, Radio Imani ilirusha matangazo ambayo yaliwahimiza waumini wa Kiislamu wasikubali kuhesabiwa.

“Mbali ya kuhamasisha, pia kituo hiki kiliwaalika wanawake
wa Kiislamu katika studio zao kukazia msimamo wa kuwazuia Waislamu wasihesabiwe jambo ambalo lililenga kufanya
uchochezi kwa jamii kinyume na sheria za utangazaji.

“Baada ya miezi sita, uongozi wa kituo hiki utatakiwa kuandika barua ya kukiri kutorudia tena kosa kama hili...kama wataendelea, watafutiwa leseni ya kurusha matangazo yao,” alisema.

Kwa upande wa Radio Neema, Bw. Bugoya alisema Januari 17 mwaka huu, ilirusha kipindi kilichozungumzia mwenye haki
ya kuchinja kati ya Waislamu na Wakristo.

Alisema kipindi hicho kiliitaka Serikali iwapatie Wakristo machinjio yao kwani suala la kuchinja ni sehemu ya ibada na kuwashawishi wasile nyama iliyochinjwa na Waislamu.

Bw. Bugoya alisema kuwa, kushawishi Wakristo wasile nyama iliyochinjwa na Waislamu ni kusababisha uvunjifu wa amani
na uchochezi ambao ni kinyume na kanuni, sheria za utangazaji.

Aliongeza kuwa, TCRA ilipata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa Januari 23 mwaka huu, kipindi cha Power Breakfact kinachorusha na Radio Clouds kilipotosha.

Alisema kipindi hicho kilikuwa kikijadili suala la uhalalishwaji ushoga nchini Marekani na hakikuwa kikiendeshwa kwa mfumo
wa kuelimisha bali kuipotosha jamii.

Aliongeza kuwa, mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa akitoa maneno ya ushabiki ambayo hayakuzingatia maadili, kanuni
na sheria za utangazaji.

“Kutokana na kosa hilo, kamati imewatoza faini, kuagizwa kufutwa kwa kipindi cha Jicho la Ng'ombe na kuutaka uongozi uwaonye watangazaji wake kutoshabikia mambo yanayoipotosha jamii,”
alisema Bw. Bugoya.

18 comments:

  1. naipongeza serikali kupitia TCRA kwa kuwa na msimamo katika kusimamia maadili ya mtanzania...hasa kwa kufuta kipindi cha Jicho la Ng'mbe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hicho kipindi cha Jicho la ng'ombe kilikuwa kinaongelea nini kwa faida ya wengine sisi tusiopenda kusiliza redio

      Delete
  2. watangazaji mjifunze kutokana na makosa yenu

    ReplyDelete
  3. TCRA WAMECHELEWA SANA KWANI KWANI REDIO IMAN INGETAKIWA KUFUNGIWA MUDA MREFU.SIKU ZOTE IMEKUWA IKIKASHIFU WAKRISTO NA UKRISTO.PIA KUNA GAZETI MOJA LINALOTUKANA UKRISTO SIJUI KWANINI HALIJAFUNGIWA.SERIKALI IMEKUWA NA TABIA YA KUOGOPA WAISLAMU KWANI WAMEKUWA WAKIENDESHA MIHADHARA YA KUKASHIFU WAKRISTO BILA HATA KIBALI.VURUGU ZOTE ZINATOKEA NCHINI ZINAANZISHWA NA WAISLAMU,KAMA WANGEFANYIWA WAO NCHI HII INGESHAINGIA KWENYE VITA.SERIKALI IACHE KUPENDELEA

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE WATU WAKIZUNGUMZA UKWELI KWAKO NI ASHFA?WAO WANATUMIA KITABU CHAKO HICHOHICHO AMBACHO WEWE WASOMA SIKU YA JPILI TU! UTAKIJUA LINI?

      Delete
    2. TCRA wamechelewa sana , tena wakristu tu wavumilivu sana , laiti wangekuwa wao ingekuwa balaaa, sasa na sisi tunakaribia mwisho wa uvumilivu na serikali inayowabeba .Sio mbali 2015

      Delete
  4. Saluti!!! TCRA,tena hata hizo adhabu za millioni tano na miezi sita hazitoshi inatakiwa kipindi kifutwe kabisa hizi ni serious issue co za kupuuziwa hata kidogo ndo zinazoleta uchochezi wa kidini pia uvunjifu wa amani nchini.

    ReplyDelete
  5. Wewe kama nani unaesema adhabu haitoshi?Tatizo wewe hujui kinachoendelea,usikurupuka na ushabiki wa dini.

    ReplyDelete
  6. Hapa naona bado haki haijatendeka. Hiyo Redio Neema imeingizwa tu ili kujastify issue kwamba hao "Waislamu" wajione kwamba hawajaonewa bali hukumu ni kwa wote. This is very stupid. Hivi tutaendelea kuwaogopa hao waislamu mpaka lini? 2015? I now know the reason.

    ReplyDelete
  7. Tukiangalia kila kitu kwa jicho la tofauti zetu za dini, hatutakubaliana kwa lolote. Nadhan mwanadamu aliumbwa kabla ya dini, hivyo akafanywa kuwa bora kuliko dini...kwa nini leo hili suala la dini liharibu mahusiano yetu? Tupende amani na umoja wa Taifa letu halafu dini ifuate...

    ReplyDelete
  8. Watanzania wapenda Amani, suala la udini linaleta kero kwa sasa. Kama mtu anasimama na kueleza, akiuawa sheikh, imamu, nk. Ua Askofu, Padre, KARDINALI, mchungaji; hii ni dini au kikundi cha wahuni! Watu hawa wamezungumza kwa hadhara kwenye kumbi kubwa kama vile diamond jubilee, lakini hadi leo ndio tunasikia serikali inasema inawatafuta!

    ReplyDelete
  9. Hawa wanaungwa mkono,tumewachok kabisa

    ReplyDelete
  10. Wote mliotoa hayo maoni bado na nyinyi mnaingia katika kundi la wachochezi. unapoongea kwamba redio imaan ifutwe unamaanisha nini? Unataka tuamshe hisia zetu? Tuchungeni midomo yenu. Sio kila kitu cha kusema. Halafu mbona hamtoi picha zenu ili tuwajue! Mnaogopa eeeeeeee!

    ReplyDelete
  11. Wewe mwenyewe mwandishi ni mchochezi, kwanini uanze na kichwa cha habari kama hiki "TCRA YAIFUNGIA REDIO IMAAN MIEZI SITA". Na vituo vilivyofanya makosa ni vitatu? Mwandishi wewe ni mlei mlei mlei. Acha kutangaza dini katika magazeti. Uislam unaenea kwa kasi duniani wewe si mwandishi basi fanya utafiti huko Marekani na Uingereza kisha waandikie wapendwa wako.

    ReplyDelete
  12. Tumechoshwa hasa naserikali katiba ya Jamhri ya muungano ibara ya 14 "kila mtu anahaki ya kuishi" lakini hawawenzetu waislamu wametoa matamko kibao ya kukusudia kuua tena hadharani DVD,CD tunazo niushahidi tosha je hii nchi inaenda wap?

    ReplyDelete
  13. Nchi hii inakwenda huko huko inapoelekea. Ina maana huioni inapoelekea?

    ReplyDelete
  14. TULIFIKIRI KUWA NA UHURU USIO NA MIPAKA NDIO DEMOKRASIA KUWA NA MAJARIDA ZAIDI YA 763 RADIO 86 NA TELEVISHENI 26 HAKUNA CHOMBO CHA KUTATHIMINI NYENDO ZA KILA CHOMBO CHA HABARI

    ReplyDelete