Na Eliasa Ally, Iringa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, imemhukumu kifugo cha miaka mitano Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Michael Ngilangwa, baada ya
kupatikana na hatia ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi ili amsaidia masomo.
Mchungaji Ngilangwa alikuwa mwalimu wa sekondari ya Pomerini iliyopo wilaya ya Kilolo.
Akitoa hukumu hiyo mjini hapa jana, Hakimu wa Mkazi wa Mahakama Iringa, Bi, Martha Mpaze, alisema mshitakiwa wakati wote wa kesi hakuwa na shahidi, ambapo alijitetea mwenyewe.
Upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano. Alisema mshitakiwa katika utetezi wake, alisema kesi hiyo ni ya kubambikizwa kosa hilo kutokana na wivu uliokuwepo kati yake na baadhi ya walimu wa sekondari ya Pomerini kumfanyia.
Alidai walimu hao walifanyia fitina baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Mkuu wa Shule Pomerini, hatua iliyomwongezea maadui ambao walikuwawakimfanyia fitina na kuandaa mazingira ya mtego ili ili akamatwe na mwanafunzi.
Alisema katika utetezi wake, Mchungaji Ngilangwa alidai baada ya kushika wadhifa huo wazazi wengi walikuwa wakimpelekea matatizo ya watoto wao, akiwemo mzazi wa mwanafuzni aliyemshitaki kwa madai ya kumuomba rushwa ya ngono.
Alisema siku ya tukio mshtakiwa aliyokamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) alipigiwa simu na mama wa mwanafunzi huyo kuwa wanatoka Dar es Salaam hivyo aliomba awatafutie vyumba katika nyumba za kulala wageni.
Katika utetezi wake alidai kwamba alikwenda nyumba ya wageni na kuchukua vyumba viwili kimoja cha kulala watu wawili.
Alidai kwa kuwa ulikuwa ni usiku, alichukua chumba namba 4 kwa ajili yake.
Bi. Mpaze alisema mshtakiwa anaonekana kuwa na makosa kwa kuwa katika kitabu cha wageni alijaza kuwa anatoka Njombe kwenda Iringa wakati siyo kweli.
Alisema ukweli ni kuwa mshtakiwa alikuwa anatoka Pomerini kwenda Iringa mjini.
Alisema kuwa ushihidi mwingine ambao unamtia hatiani Mchungaji Ngilangwa ni ule wa TAKUKURU kumkuta na vidonge vya kuzuia mimba, ambavyo alimpatia mwanafunzi wake ameze kwa kuwa wangefanya ngono bila kutumia kondomu.
Hakimu huyo alisema ushahidi mwingine ni ule wa ujumbe ambao TAKUKURU ilinasa sauti walipokuwa wakiongea na mwanafunzi wake.
Hakimu huyo alikuwa akimwambia mwanafunzi huyo aende chumba namba nne ndiko wangelala.
"Mshtakiwa anatiwa hatiani kwa ushahidi mwingine ambapo TAKUKURU ilimkuta akiwa na mwanafunzi wake huyo saa 5:00 usiku wakati sheria ya nyumba hiyo ya kulala wageni walipokutwa inakataza watu wasio wanandoa kulala chumba kimoja.
Hakimu huyo alisema kama TAKUKURU wasingewahi mwanafunzi huyo angebakwa na azma yake ya kuomba rushwa ya ngono ingetimia.
Mshtakiwa huyo alipotakiwa kujitetea aliomba mahakama imfikirie kwa kuwa ana watoto wanne wanaomtegemea, wawili wanasoma sekondari na wengine shule ya msingi.
Mchungaji Ngilangwa aliongeza kuwa mzazi wake ni mzee wa miaka 82, hivyo hana mtu wa kumtunza.
Akitoa hukumu Hakimu Bi. Mpaze, alisema mahakama imezingatia kuwa mkosaji wa mara ya kwanza lakini akahukumiwa adhabu wa miaka mitano jela.
Katika kesi ya pili ya kuomba rushwa ya ngono mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya sh. 500,000 au endapo atashindwa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.
Mahakimu mara nyingi hawachunguzi sana kiini cha kosa (Natural causes) huwa hazipo kwenye makosa. Kwa mfano, mfadhaiko wa akili huchukuliwa kama something done deliberately. Hata mtu kubaka, huwa kuna mfadhaiko wake ambao hata wao mahakimu huwa nao na huenda kwa ajili ya kuwa Mheshimiwa yanafichwa lakini wanayo makosa makubwa (deep) na grave kwani wengine hulala na housemaids, ambayo ni kama kubaka, lakini kwa vile ni mheshimiwa, hai-surface. Rushwa ya pesa na ngono ni kitu kiko kwa hawa mnao waita waheshimiwa. Vile vile yabidi Mahakimu wasomee psychology kwa kina kikubwa. Kwa kesi hii husika, this was a trap, and nothing but a delibrate trap ambayo huyu mwalimu kwa kuishi kwake kijijini, hakujua kuwa anategewa. Kuna kitu kikubwa ndani ya hii kesi. Huyu mwalimu inaonekana anao maadaui wamemzingira, msichana alitumwa, wazazi walioomba kutafutiwa vyumba walikuwa na lengo baya na pana toka kwa walio watuma na si hao tu kuna pia wengine ambao wako involved. Lakini mlipaji ni Mungu. Adhabu yao itafuata. Acha mtu wa watu akatumikie kifungo lakini walio sababisha, upanga ni juu yao milele.Na huyu Hakimu hana uelewa mpana, akasome tena kwa kina.
ReplyDeletePambaf! Unasumbuliwa na siasa kali, nani alimtuma aende gesti usiku? nani alimwambia adanganye anakotoka na anakoenda kama alikuwa hana nia mbaya? Mwache akachunge kondoo midume jela! Mzinzi tu huyo hana cha uchungaji! Hivi kweli huyo unaweza kumpa binto yako amlee kiroho? Wee, utaambulia mjukuu!
ReplyDelete