07 November 2013

MISS UNIVERSE TANZANIA ATAMBA MOSCOW Na Namkeshe Ridhiwani
  Miss Universe Tanzania, Betty Omara ametamba katika maonesho ya mavazi kwa warembo 85, wanaowania taji la Miss Universe 2013 yatakayofanyika mjini Moscow, Urusi.

Katika maonesho hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Vegas Mall, vazi la Betty lililobuniwa na mbunifu anayekuja kwa kasi nchini, Mwanakombo Salim lilipendwa na mashabiki wengi na anamatarajio makubwa kushinda taji hilo, wakati wa fainali za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Jumamosi.
Vazi hilo limechorwa na wasanii wa Tingatinga, Said Kambili na Mimus, michoro ambayo ni maarufu nchini iliyoasisiwa na msanii maarufu wa zamani, hayati Edward Tingatinga. Vazi hilo mbali ya kudumisha utamaduni wa Tanzania, pia limechorwa michoro mbalimbali ya kuvitangaza vivutio vya kitalii.
Vazi hilo pia lina nakshi za mkeka na miba ya mnyama ajulikanaye kwa jina la Nungunungu. Vilevile pia umetumika kama njia ya kumuonesha ndege tausi kama inavyoonekana rangi za mkeka kwenye mkia na kilemba kichwani mwake.
  Lengo kuu la nguo na michoro hiyo ni kutangaza kazi za mikono na utalii wa Tanzania na miongoni mwa michoro iliyooneshwa ni duma, tembo na twiga vilevile imeonesha ndege na maliasili zipatikanazo Tanzania kama vile tausi, vipepeo, mimea na Mlima Kilimanjaro.Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa

No comments:

Post a Comment