06 November 2013

SUMAYE AANIKA MAMBO MAZITO

  • AZUNGUMZIA TUHUMA DHIDI YAKE NDANI YA CCM
  • ATOA MSIMAMO URAIS 2015, AMUUNGA MKONO JK
 Na Goodluck Hongo

Vita ya kuwania urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inazidi kupamba moto baada ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu wa Tatu, Bw. Frederick Sumaye, kuanika hujuma zinazofanyika dhidi yake kupitia mialiko, usambazaji taarifa katika vyombo vya habari na propaganda chafu za kisiasa.

  Bw. Sumaye alianika hujuma hizo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hujuma anazodai kufanyiwa pamoja na kutoa msimamo wake wa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kwa kukemea rushwa ndani ya chama hicho.
  Alisema zipo hujuma zinazofanywa katika shughuli za jamii kwa masilahi kisiasa ambapo kuna mialiko inayotolewa na taasisi, vikundi vya jamii au madhehebu ya dini kwa viongozi mbalimbali ili waweze kuwasaidia katika shughuli zao kama kuhamasisha, kutoa ujumbe, kuzindua jengo, mradi pamoja na kuchangia fedha.
 Aliongeza kuwa, mwaliko uliopangwa unaweza kuvurugwa kwa sababu yoyote ambayo haistahili kuwepo na kusababisha wahusika kucheleweshewa maendeleo na manufaa ambayo wangeyapata kutokana na shughuli  inayohusiana na mwaliko huo.
Alitoa mifano miwili iliyohusu kujuma dhidi yake na kudai Oktoba 27 mwaka huu, alialikwa na kikundi cha Joggers cha Dar es Salaam, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja."Dakika za mwisho, nilipewa taarifa kuwa shughuli imeshindikana kwa sababu imeingiliwa na kikundi chenye kulinda masilahi yake au ya mtu wao lakini baadaye niliambiwa ilifanyika na mgeni rasmi alikuwa mtu mwingine," alisema Bw. Sumaye.
Alisema hiyo ilikuwa mbinu ya kuzuia ujumbe aliokusudia kuutoa siku hiyo ambapo hujuma ya pili, ilihusu mwaliko wa kuzindua SACCOS ya Nshamba Muleba, mkoani Kagera, ambapo alipata mwaliko wa kufanya shughuli hiyo Oktoba 28 mwaka huu.
  "Mwaliko huu sikuuomba bali viongozi wa chama walinipendekeza kwa sababu zao wenyewe sasa wakati najiandaa kwenda Kagera, nikaambiwa shughuli zimeingiliwa na watu fulani ambao walitoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa SACCOS ili isifanyike na kuambiwa haiwezekani Sumaye afike Kagera kabla ya mtu wao," alisema Bw. Sumaye na kuongeza;
"Hata matangazo yaliyolipiwa fedha kutangaza mkutano huo, ilibidi yasitishwe na fedha kurudishwa...nataka kuwaambia hao wanaohangaika na mialiko yangu wajue kuwa, mialiko ninayo mingi hadi mingine nakosa muda wa kwenda, siitwi kwa sababu ya fedha maana wanajua sina fedha za aina hiyo," alisema.
Bw. Sumaye alisema, jinsi wanavyojitahidi kumzima kwa rushwa ili asiendelee kukemea vitendo hivyo, ufisadi na dawa za kulevya ndivyo wanavyompa nguvu na mifano hai ya jinsi rushwa na ufisadi ni kirusi hatari katika Taifa.
Alisema mafisadi ni watu hatari katika jamii kwani lengo ni kuvuruga mipango ya nchi.
Aliongeza kuwa, kipindi hiki cha kuelekea 2015 kuna propaganda na mbinu mbalimbali zinazotumika na wanasiasa wanaotafuta nafasi mbalimbali kufanikisha malengo yao.
Alisema kuna mbinu nzuri za kistaarabu pia kuna mbinu chafu kama za kupakazana matope.Bw. Sumaye alisema mbinu ya kistaarabu ni pale mhusika anapowashawishi wanaomsikiliza kuwa yeye ni mtu safi atakayemudu nafasi hiyo bila kumwathiri mtu mwingine ambaye anadhaniwa kuwania nafasi husika.
"Mtu wa aina ya kwanza, tungeweza kusema anajisafishia njia yake kwa kufyeka miiba na kuondoa magogo njiani ili wakati ukiwadia mbio zake zisikwazwe na vigingi vyovyote."Aina ya pili ni mbinu chafu ambapo mhusika anatengeneza mbinu za kuwamaliza wengine wanaodhaniwa kuwa washindani wake au kuwawekea vikwazo wasijisafishie njia," alisema.
Alisema mtu wa aina hiyo anawachafua wenzake kwa kuwapakaza matope ya uongo au kuwajengea mazingira yeye kupendwa kwa kutumia migongo ya wengine.Tukirudi kwenye mfano wetu wa kufyeka barabara, atakuwa anachimba mitaro kwenye barabara wanazofyeka wenzake au anatupia miba na magogo yanayotoka kwake na kuyatupia kwa wenzake ili mradi wenzake wakwame wakati ukiwadia.
  "Mimi mtu akihangaika kujisafishia njia bila kuathiri wengine au kuathiri mambo fulani ya msingi huwa hainisumbui sana, lakini ikiwa inaathiri mtu mwingine itabidi tuiambie jamii ukweli na hivi ndivyo nitakavyofanya leo (jana), hata wakati mwingine jambo kama hilo likijitokeza," alisema Bw. Sumaye.
Alitolea mfano habari moja iliyoandikwa na gazeti moja (si Majira) kuwa Siri ya mradi wa kuvuta maji Ziwa Victoria yafichuliwa.
Aliongeza kuwa, katika maelezo yake mtoa habari alisema ni Mawaziri wawili tu waliounga mkono mradi huo na wengine waliupinga."Najua mhusika ameutumia mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua sana ili la mradi ametukanyaga vidole wengine na kutupia miba na magogo kwenye njia yetu.
"Amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa Waziri Mkuu na mradi umetekelezwa chini ya uangalizi wangu kama kiongozi na Msimamizi Mkuu wa utekelezaji wa shughuli zote za Serikali.
"Kama unachumbia msichana mzuri mweleze jinsi utakavyomjengea nyumba, lakini usianze kuwachafua wengine wanaotaka kumchumbia msichana huyo," alisema.Bw.Sumaye alisema lililoelezwa kuhusu mradi huo ni uongo, mhusika kama Waziri Mwandamizi wakati huo na sasa anadaiwa kuwinda nafasi kubwa katika nchi, hakutegemewa kutoa siri za Baraza la Mawaziri labda amediriki kufanya hivyo kwa sababu anajua anayoyasema siyo ya kweli vinginevyo ni kosa la jinai na akishtakiwa anafungwa jela.
Aliongeza kuwa, mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ni mradi wa Serikali si wa mtu. "Mradi huu ulikuwa wa Mheshimiwa (jina tunalihifadhi), wakati huo alikuwa Waziri wa Maji na aliusimamia hadi ukakamilika kama ambavyo angeusimamia Waziri mwingine wa Maji.
 "Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna Waziri mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza la Mawaziri likiukataa, alisisitiza na kuongeza kuwa, hapendi kuingilia mambo ya watu wengine lakini yanapomgusa hatanyamaza hivyo ni wajibu wake kueleza ukweli hasa pale unapopotoshwa kwa makusudi.
Kumuunga mkono JK
  Bw. Sumaye alisema anamuunga mkono Rais Kikwete kwa kuonesha nia ya kupambana na rushwa ndani ya chama hicho kwani yeye ataendelea kuwa mstari wa mbele katika vita hivyo. Alipoulizwa atafanya nini kama watu wanaotoa rushwa watapitishwa na CCM kuwania uongozi, alisema; "Kama CCM itapitisha majina bila kuangalia waliotoa rushwa chama kitaanguka.
"Lakini siamini kuwa watapitisha watu wanaonunua watu wengine, wakipitisha hatutaweza kukaa pamoja na watoa rushwa, sitahama, lakini sitakaa nao," alisema.
Kuwania Urais
   Alipoulizwa kama ana mipango ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu 2015, Bw.Sumaye alisema;
 "Mimi ni mwana CCM, chama kimesema atakayejitangaza atakiona cha moto, sasa mnataka nikione cha moto...kama ni kugombea nina haki zote, uwezo na nina imani Watanzania wana imani na mimi," alisema.
  Alisema amekuwa akisikia watu wakimtaja lakini wakati ukifika atatangaza kama anawania nafasi hiyo au hapana.
Fedha UswisiAlipoulizwa kama yeye ni miongoni mwa watu waliohifadhi fedha nje ya nchi hususan Uswisi, alikataa na kuishangaa Serikali kwanini inashindwa kuwataja watu hao.
 "Sijawahi kuwa na akaunti nje hata ambayo haina hela lakini nashangaa kwanini Serikali haifanyi utaratibu kwa ajili ya kuwataja majina walioficha fedha huko," alisema Bw. Sumaye.
Jumuiya ya Afrika Mashariki
  Bw. Sumaye alisema ni kosa kubwa kwa Tanzania kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwani suala hilo ni la wananchi si la viongozi.Alisema katika ulimwengu wa sasa, nchi nyingi zinaungana hivyo suala la kujitoa ni la wananchi kuamua wenyewe kwani wakati wa kuanzishwa tena jumuiya hiyo walikaa vikao vingi na wananchi ndipo waliporidhia.
 Aliongeza kuwa, nguvu kubwa ilitumika wakati wa kuanzishwa jumuiya hiyo ambayo awali ilivunjika lakini anashangaa kuona kuna watu wanataka kujitoa kitu ambachoki namu umiza sana."Dunia nikotenchim balimbali zinaungana, hakuna uchumi unaoendeshwa kwa malori ila kuimarika kwa reli na bandari kutaifanya Tanzania kuwa na uchumi mkubwa kwa haraka.
 "Huwezi kutegemea uchumi unaotokana na jembe la mkono bila kuimarisha banda rina reli, usafiri wa rel I ndio muhimu katika usafirishaji,"alisema Bw. Sumaye. Aliongeza kuwa, kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi ku wa Tanzania ina eneo kubwa na wengine kudai watatoa talaka zinamshangaza kwani katika maeneo mengi h ususan mkoani Arusha,ardhi kubwa imechukuliwa na wageni wakiwemo Wachina.
 "Kwa maoni yangu, napingana na Tanzania kujitoa Afrika Mashariki kwa sababu nchinyin gi duniani zina unganalak iniwenginewanasema sisi ndiyo tutatoa talaka," alisema.Alisema njia pekee ni kukaa katika mazungu mzo ili kutatua changamoto zilizopo kwani kama nchi ina bandari ni kitu muhimu sana hivyo kusema waende kujiun gana C ongo(DRC) ni kitukisichokubalikaNo comments:

Post a Comment