28 November 2013

MBOWE KUPANGUA ‘MAWAZIRI’ WAKE!

  • HATIMA YA NAFASI ZA ZITTO KUJULIKANA KARIBUNI
  • ALIYEMLALAMIKIA KUHOJIWA POLISI MAKAO MAKUU LEO
Na Goodluck Hongo

   Kiongozi wa Kambi Rasmi Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, anatazamiwa kufanya mabadiliko kwa Baraza lake la Mawaziri Kivuli, wakati wowote katika kipindi cha Mkutano ujao wa Bunge ili kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu iliyokutana hivi karibuni na kumvua wadhifa wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.


Zitto amevuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu kutokana na kile kinachodaiwa anahusika kuandaa waraka wa kufanya mapinduzi ya viongozi ndani ya chama hicho.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho vililiambia gazeti hili kuwa Kamati Kuu ambayo ndiyo inasimamia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hivyo mara baada ya kutangaza kumvua Zitto, wadhifa wake (unaibu katibu mkuu) ilielekezwa uanze mchakato wa kumuondoa kwenye nafasi zake.

Bungeni, Zitto ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi akiwa msaidizi wa Mbowe na Waziri Kivuli wa

 Wizara ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena," alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini.

Hata hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana kutokana na malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Mahojiano hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya Kileo kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.

Baada ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na mwanasheria wake, lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano yalitakiwa yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu ya polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao makuu ya Polisi.

Kileo, alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani, alisema hana taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa aliyejitambulisha kwa jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao makuu ya Polisi kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto, ameyafikisha.

"Niliambiwa nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto amezifikisha Polisi, lakini sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi ili muwaulize swali hilo."

Gazeti moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto, amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho

5 comments:

  1. Zito vumilia tuko nyuma yako, endelea kutochukua posho,waliorudia shangingi watatueleza kwenye kampeni.pia wanaochukua posho wakati ipo kwenye maagizo ya chadema .je tuwaelewe vipi?

    ReplyDelete
  2. Zitto ni opportunist the Kafulila or Kigoma type. Kwa mwenendo huo utakwama tu. Fanya SWOT analysis yako vizuri. Acha kutumika, unasema umesoma why not specialize? Wanaotaka mabadiriko wanakuona ni janga. Huwezi kupata kote utakosa kote. Jina lako halilingani na tuhuma zako jirekebishe mapema. Anza 'a' utarudi kwenye chati achana na CCM kumejaa. Nionyeshe waliotumika wako wapi?

    ReplyDelete
  3. Kweli Zito umefanya mengi mazuri na wato wote wanaona. Lakini a) Haiingi akilini kwamba waliopanga mipango ya siri ya kuondoa uongozi halali Chadema madarakani walifanya hivyo wakati wewe hujui.
    b) Kama mahesabu ya vyama hayajakaguliwa, kwa nini unalaumu vyama wakati wewe ndiye mwenyekiti wa kmati ya kusimamia fedha?

    ReplyDelete
  4. CHADEMA angalieni msipoteze matumaini kwa watanzania

    ReplyDelete