03 December 2013

ALL STARS TANZANIA, KENYA UWANJANI DES.12



 Na Mwandishi Wetu
Timu inayoundwa n a wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Tanzania All Stars' na wale wa Kenya 'Wazee wa Kazi' wataoneshana kazi mjini Nairobi, Kenya siku ya fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji Desemba 12, mwaka huu.

Nyota wa zamani wa timu ya Yanga na ya Taifa, Kitwana 'Popat' Manara alisema jana kuwa mechi hiyo ya kihistoria imebarikiwa na Baraza la Vyama la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na wameanza mazoezi makali chini ya usimamizi wake. Timu hiyo inatarajiwa kuondoka jijini Desemba 10.
Mbali ya Manara, mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Talib Hilal anasimamia mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kila siku jioni kwenye viwanja vya Leaders Club jijini.
Manara alisema kuwa wapo katika mazoezi makali kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itachezwa kabla ya fainali ya mashindano hayo.
Alisema wachezaji wote wapo vizuri na malengo yao ni kuonesha ubora na vipaji vilivyotukuka walivyokuwanavyo enzi za ujana wao na kuleta sifa kubwa katika soka la Tanzania.
Mbali ya Manara, wachezaji wengine wanaounda timu hiyo ni Isihaka Hassan, Mohamed Mkweche, Lawrence Mwalusako, David Mwakalebela, John Mwansasu, Ali Yusuph Tigana, Sekilojo Chambua na Rashid Idd Chama.
Wengine ni Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein Mmachinga, Khaleed Abeid, James Kisaka na Omari Gumbo. Kutoka Zanzibar golikipa ni Gopi na Mwinyi Bwanga.
Alisema kuwa wanatarajia kumjumuisha kipa nyota wa zamani, Juma 'Mensah' Pondamali ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Kilimanjaro Stars inayoshiriki mashindano hayo.
Kwa upande wa viongozi ni Hassan Mnyenye na mjumbe wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Jamal Lwambo.
"Lengo letu ni kuwa na wachezaji wengi zaidi, lakini wengi wao wameshindwa kujiunga na sisi kutokana na matatizo mbalimbali, hao ndiyo walioitikia wito huo na wameanza mazoezi, tunaomba wadhamini mbalimbali kutusaidia ili kuweza kufanikisha safari hiyo, ni gharama kubwa sana na lengo letu ni kuhamasisha mchezo wa soka," alisema Manara.
Hu k u t imu y a Ta n z a n i a ikisaka wadhamini, wenzao wa Kenya wanaendelea na mazoezi na wamekwisha taja kikosi kitakachoikabili timu hiyo. Kikosi hicho kipo chini ya kocha George Sunguti kina wachezaji 30 ambao waliwika Harambee Stars enzi zao.
Wachezaji hao ni makipa James Siang'a, Mohammed Abbas, John Busolo huku mabeki ni Josphat Murila, Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo, Thobias Jua Kali Ochola, Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu, Paul Ochieng na John Bobby Ogola.
Viungo ni Allan Thigo, Paul Onyiera, ambapo washambuliaji ni Joe Kadenge , Peter Dawo , Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga , Mike Amwayi, Douglas Matual, Joe Birgen, Abdul Baraza, Ricky Solomon, James Nandwa, Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya, David Ochieng', George Sunguti na Austin Oduor.

No comments:

Post a Comment