Na Mwandishi Maalum
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka maofisa mipango miji
nchini kurekebisha utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya
iliyojengeka miongoni mwa jamii dhidi yao.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Kwanza
wa Wataalam wa Mipango miji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa
Mipango miji ulioanza jana jijini Dar
es Salaam.
“Taswira
ya utendaji kazi katika taaluma ya mipango miji na katika sekta ya ardhi kwa
ujumla miongoni mwa wananchi na Serikali sio nzuri sana.
Watafiti
wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji yetu hapa
nchini yamejengwa kiholela.
Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi
hayo na wanaishi kiholela,î alisema.
“Wako wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako
wanaosema ninyi kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila
ninawasihi muwe na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza.
Aliwataka wajadili masuala yanayohusu migogoro ya ardhi
baina ya wafugaji na wakulima, baina ya mipaka ya vijiji, baina ya wilaya,
baina ya wanavijiji na hifadhi za Taifa au maeneo ya uchimbaji madini na
kujadili njia za kutatua migogoro hiyo ili kuwa na mipamgo endelevu.
Aliwataka waangalie suala la ukuaji wa miji iliyokaribu na Jiji la
Dar es Salaam kwa kuangalia dhana ya miji
mikubwa kubeba vijiji vinavyoizunguka na hasa kuangalia uwezekano wa kupunguza
mrundikano wa watu katika jiji hilo.
“Miji ya Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo inatumikaje kusaidia
kupunguza msongamano katika jiji la Dar
es Salaam,” Waziri Mkuu alihoji.
Alisema wataalamu wa mipango miji wanapaswa kuwa na maono makubwa
ya baadaye kama kweli wanataka kupunguza majanga katika siku za usoni.
“Angalieni utafiti wa gesi unaoendelea pale Mtwara na mjipange,
angalieni mpango wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na kuunganisha na reli ya
kati, angalieni Lindi na upatikanaji wa Liquified Naturala Gas (LNG), pangeni
miji kwa siku za baadaye siyo sasa,” alisisitiza.
Aliwataka wanataaluma hao wasimamie vyema taaluma yao kwani katika
miaka 37 ijayo, (mwaka 2050) inakadiriwa kwamba nusu ya watu wote watakuwa
wakiishi mijini. “ Kuweni wakweli, tumieni weledi wenu la sivyo katika miaka 37
ijayo kama wanavyosema watafiti, itakuwa balaa tupu,î alisema.
Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wataalamu hao
kutoka mikoa yote hapa nchini, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Prof.
Anna Tibaijuka, alisema maofisa mipango miji wanakabiliwa na changamoto ya
kufikiri na kubuni aina ya miji ambayo itakidhi mahitaji ya jamii ya baadaye.
Alisema hata hivyo maofisa hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
ya kushindwa kutoa maamuzi au ushauri wa kitaalamu kwa kuhofia kuadhibiwa na
madiwani.
Wizara ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa
akishiriki kuandaa bajeti ya upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya
fedha akiwa waziri kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake
haaminiki tena," alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa
sharti la jina lake kutochapishwa gazetini.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga
mwamba kutokana na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es
Salaam leo linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es
Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana kutokana na
malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mahojiano hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
jijini Dar es Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya
Kileo kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na
mwanasheria wake, lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano
yalitakiwa yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu
ya polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao makuu
ya Polisi.
Kileo, alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani,
alisema hana taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa
aliyejitambulisha kwa jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao
makuu ya Polisi kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto,
ameyafikisha.
"Niliambiwa nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto
amezifikisha Polisi, lakini sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema
Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi,
badala ya vituo vingine kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui
labda wapigie polisi ili muwaulize swali hilo."
Gazeti moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa
Zitto, amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao
ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment