- NDUGAI AWAPA ‘RUNGU’ ASKARI WA BUNGE
- MBOWE AONDOLEWA KWA NGUVU BUNGENI
Na
Waandishi Wetu
HALI si shwari ndani ya U k u m b i w a
B u n g e mjini Dodoma, ndivyo u n a v y owe z a k u s ema kutokana na baadhi
ya wabunge wa upinzani, kutunishiana misuli (kutishiana) na walinzi wa Bunge
ili wasiweze kutekeleza amri ya kumtoa nje ya ukumbi huo Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe.
Askari hao
walipewa amri hiyo na Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai muda mfupi baada ya
wabunge wote kupiga kura ya kukubali au kukataa majadiliano ya Muswada wa
Katiba uliopelekwa bungeni na Serikali, ujadiliwe na Bunge hilo.Idadi kubwa ya
wabunge, waliunga mkono Muswada huo ujadiliwe bungeni. Wabunge 59 walisema
mjadala huo uondolewe ambapo 156 walitaka uendelee kujadiliwa kwa kuwa
ulishapita katika hatua mbalimbali.
Kutokana na
matokeo ya kura hizo, Bw. Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge hivyo
alimsimamisha Mbunge wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro, Bw. Augustino Mrema (TLP),
aweze kuchangia Muswada huo.
Kabla Bw. Mrema hajaanza kuchangia, Bw. Mbowe alisimama na
kuomba mwongozo juu ya uamuzi wa wabunge kuunga mkono majadiliano ya Muswada
huo Bw. Ndugai, alimtaka akae.
Akitumia kiti
chake, Bw. Ndugai aliwataka wabunge kuyakubali na kuyaheshimu matokeo ya kura
zilizopigwa ili Muswada huo uweze kujadiliwa kwa masilahi ya Watanzania na
Taifa.Bw. Mbowe
alikataa kukaa ambapo baadhi ya wabunge kutoka upinzani, nao walimuunga mkono
kwa kusimama. Pamoja na Bw. Ndugai kuwataka wakae na kuheshimu taratibu za
Bunge, bado walikataa hivyo aliwataka askari wa Bunge wajiandae.
Wabunge hao waliendelea kusimama pamoja
na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani ambapo baada ya muda mfupi Bw. Ndugai
alitoa amri kwa askari hao wamtoe Bw. Mbowe.Amri hiyo ilisababisha tafrani kubwa ndani ya ukumbi huo ambapo baadhi
ya wabunge wa
upinzani waliokuwa
wakimuunga mkono Bw. Mbowe, walitoka katika viti vyao na kwenda kuwazuia askari
hao ili wasiweze kumtoa kiongozi huyo.Mabishano makali yaliibuka kati ya
wabunge hao na askari wa Bunge ambao baadhi yao walikuwa nje ya ukumbi huo lakini
walilazimika kuingia ndani ili kutekeleza amri hiyo.
Baada ya mvutano mkali, askari hao
walifanikiwa kumtoa Bw.Mbowe ndipo wabunge wenzake waliokuwa wakimuunga mkono,
nao walilazimika kutoka nje ya kususia kikao hicho.Muda mfupi baada ya Bw. Mbowe
kuondolewa bungeni, Bw. Mrema aliendelea kuchangia Muswada huo na kusema kuwa,
kitendo kilichofanywa na baadhi ya wabunge si cha kiungwa mkono na kinaleta
fedheha kwa jamii na Taifa.
"Kutotoka kwangu nje ya Ukumbi wa
Bunge, haimaanishi mimi ni kibaraka wa CCM...wananchi wangu wa Vunjo
hawajanituma kufanya hivyo, nitakaa ndani ya Bunge hadi kieleweke."Mimi ndiye kiongozi wa vyama
vyote tisa hivyo nastahili kuheshimiwa, ninachopigania ni masilahi ya Taifa
sikutumwa nitoke nje ya Bunge au kususia kikao," alisema Bw. Mrema.
Baada ya kuchangia Muswada huo,
alisimama Mbunge wa Same Mashariki, Bi. Anne Kilango Malecela ambaye aliitaka
Serikali kusimama imara bila kuogopa vitisho vinavyotolewa na watu wasioitakia
mema Tanzania.Alisema kitendo kilichofanywa na
wapinzani bungeni hakina nia njema ili kupata Katiba Mpya ambapo wabunge 156
waliopiga kura, wana vigezo vya kuchangia Muswada huo kujadiliwa.
Wabunge hao walichangia Muswada huo kwa
muda wa nusu saa ambao uliongezwa na baadaye, Bw. Ndugai aliahirisha Bunge hadi
jioni ambapo wabunge waliotoka nje, hawakurudi bungeni wakati Muswada huo
ukiendelea kujadiliwa.
Vurugu ndani ya Bunge hilo, ziliaza muda mrefu ambapo baadhi ya
wabunge, walikuwa wakizingumza bila kufuata utaratibu hivyo Bw. Ndugai,
alilazimika kusimama mara kwa mara ili kujeresha utulivu.Sakata la mjadala huo lilianza juzi
jioni baada ya wabunge wa CHADEMA na CUF, kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge baada
ya Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu kuwasilisha maoni ya kambi hiyo
na kudai wananchi wa Zanzibar,
hawajashirikishwa katika mchakato Rasmi ya Katiba Mpya.
Imeandaliwa na David John, Rehema Maigala na Mariamu Mziwanda
sasa ni wazi hawa chadema hakuna wanachokijua, huyu mbowe alikua anapinga kitu gani jamani? mbona kichwa chake kigumu hivi? huyu ni kiongozi wa upinzani aibu gani nchi hii? kura imepigwa wabunge wanaoptaka muswaada ujadiliwe wameshinda sasa hapo katika akili ya kawaida kuna kupinga tena?, Huyu aende akauze pombe zake, kiti hakiwezi hicho
ReplyDeletechadema ni taasisi binafsi wasitusumbue wanayoyafanya si tu utomvu wa nidhamu bali ni upumbavu ambao hata mtoto hawezi kuufanya, sasa kwa mtindo huo ndio wanataka wapewe nchi hivi kweli tutafika? naomba wananchi tufikirie mara 2 HAWAFAI labda ujumbe wa nyumba kumi kumi.
ReplyDeleteregards
masala jonathan sowa
Unataka wapewe ujumbe wa nyumba kumi? Hujui walivyoingiza ubishi na kutoridhika kwa kila ngazi, hata ndani ya familia sasa ni kwa mbinde kutoa maamuzi!
DeleteMhhu! Tuangalie kwa makini, angalia vizuri hoja za Upinzani walivyochambua kipengle kwa kipengele katika mapendekezo ya marekebisho ya hoja ya sheria ya mabadiliko ya katiba. "We need to think out of Box". Kuhusu Freeman Mbowe, nadhani angepewa nafasi kama alivyo Waziri Mkuu basi yote yale yasingetokea. Ubabe ulitumika zaidi ya Kanuni za bunge.
DeleteKama upeo wako mdogo au unaegemea upande mmoja bila hata reasoning ya mada husika, nashauri tusitoe comment.
ReplyDelete