Na Rehema Mohamed
UPANDE wa mashtaka
katika kesi ya utakatishaji fedha ambayo inamkabili aliyekuwa Mhasibu wa Chuo
Kikuu Huria nchini (OUT), Engels Mrikarika, umeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jinsi mshtakiwa alivyokuwa akimuingizia fedha mpenzi wake Rose Maungu.
Wakili wa Serikali
Prosper Mwangamila, aliyasema hayo jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu
Augustina Mbando, wakati akiwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao.Alidai katika vipindi
tofauti kati ya Julai mosi 2009 na Aprili 30,2011 jijini Dar es Salaam,
Mrikarika kwa makusudi aliandaa nyaraka za malipo ya mishahara ya wafanyakazi
wa chuo hicho na kuingiza jina la Maungu na wengine watano.
Aliongeza kuwa,
wakati huo Maungu alikuwa akifanya kazi Chuo cha Biashara (CBE), Tawi la Dar es
Salaam kama Katibu Muhtasi lakini Mrikarika aliingiza jina hilo akionesha ni
mfanyakazi wa chuo hicho hivyo anastahili kulipwa wakati si kweli.
I l i d a iwa ms h t
a k iwa Mrikarika alipeleka nyaraka hiyo katika Benki ya NBC, tawi la Cooparate
na kutoa ma e l e k e z o kwa b e n k i hiyo ifanye malipo kutoka akaunti
0111030002560 ya chuo hicho kwenda akaunti 0150205110500, 019201046241 za Benki
ya CRDB Tawi la Kichewe akimuingizia Maungu sh. milioni 68.
Mwangamila alidai
kuwa, Maungu alizitoa fedha hizo, kuzifanyia matumizi binafsi na nyingine
kuziingiza katika biashara ya duka la vifaa vya ofisini liitwalo Judiana
Stationery ambalo wanashirikiana na mpenziwake Mrikarika ili kuficha chanzo cha
fedha hizo ionekane zilipatikana kwa njia ya biashara.
Alisema katika
maelezo ya onyo aliyotoa polisi, Maungu alikiri kutokuwa mtumishi wa chuo hicho
ingawa alikuwa akipokea malipo kutoka akaunti 011103000250 NBC kutoka OUT.
Hakimu Mbando alipowahoji
washtakiwa hao juu ya maelezo hayo, waliyakana pamoja na uhusiano wa kimapenzi.
Mwangamila aliieleza mahakama hiyo kuwa ili kuthibitisha mashtaka dhidi ya
washtakiwa hao, wanaomba wapangiwe tarehe ya usikilizwaji ili walete mashahidi
pamoja na vielelezo mbalimbali.
Hakimu Mbando aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 19 mwaka
huu, kwa ajili ya usikilizwaji.
No comments:
Post a Comment