06 September 2013

JK, KAGAME KICHEKO



Na Waandishi Wetu
HALI si shwari ndani ya U k u m b i w a B u n g e mjini Dodoma, ndivyo u n a v y owe z a k u s ema kutokana na baadhi ya wabunge wa upinzani, kutunishiana misuli (kutishiana) na walinzi wa Bunge ili wasiweze kutekeleza amri ya kumtoa nje ya ukumbi huo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe.

Askari hao walipewa amri hiyo na Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai muda mfupi baada ya wabunge wote kupiga kura ya kukubali au kukataa majadiliano ya Muswada wa Katiba uliopelekwa bungeni na Serikali, ujadiliwe na Bunge hilo.Idadi kubwa ya wabunge, waliunga mkono Muswada huo ujadiliwe bungeni. Wabunge 59 walisema mjadala huo uondolewe ambapo 156 walitaka uendelee kujadiliwa kwa kuwa ulishapita katika hatua mbalimbali.
Kutokana na matokeo ya kura hizo, Bw. Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge hivyo alimsimamisha Mbunge wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro, Bw. Augustino Mrema (TLP), aweze kuchangia Muswada huo.Kabla Bw. Mrema hajaanza kuchangia, Bw. Mbowe alisimama na kuomba mwongozo juu ya uamuzi wa wabunge kuunga mkono majadiliano ya Muswada huo Bw. Ndugai, alimtaka akae.
Akitumia kiti chake, Bw. Ndugai aliwataka wabunge kuyakubali na kuyaheshimu matokeo ya kura zilizopigwa ili Muswada huo uweze kujadiliwa kwa masilahi ya Watanzania na Taifa.Bw. Mbowe alikataa kukaa ambapo baadhi ya wabunge kutoka upinzani, nao walimuunga mkono kwa kusimama. Pamoja na Bw. Ndugai kuwataka wakae na kuheshimu taratibu za Bunge, bado walikataa hivyo aliwataka askari wa Bunge wajiandae.
Wabunge hao waliendelea kusimama pamoja na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani ambapo baada ya muda mfupi Bw. Ndugai alitoa amri kwa askari hao wamtoe Bw. Mbowe.Amri hiyo ilisababisha tafrani kubwa ndani ya ukumbi huo ambapo baadhi ya wabunge wa upinzani waliokuwa wakimuunga mkono Bw. Mbowe, walitoka katika viti vyao na kwenda kuwazuia askari hao ili wasiweze kumtoa kiongozi huyo.
Mabishano makali yaliibuka kati ya wabunge hao na askari wa Bunge ambao baadhi yao walikuwa nje ya ukumbi huo lakini walilazimika kuingia ndani ili kutekeleza amri hiyo.Baada ya mvutano mkali, askari hao walifanikiwa kumtoa Bw.Mbowe ndipo wabunge wenzake waliokuwa wakimuunga mkono, nao walilazimika kutoka nje ya kususia kikao hicho.
Muda mfupi baada ya Bw. Mbowe kuondolewa bungeni, Bw. Mrema aliendelea kuchangia Muswada huo na kusema kuwa, kitendo kilichofanywa na baadhi ya wabunge si cha kiungwa mkono na kinaleta fedheha kwa jamii na Taifa."Kutotoka kwangu nje ya Ukumbi wa Bunge, haimaanishi mimi ni kibaraka wa CCM...wananchi wangu wa Vunjo hawajanituma kufanya hivyo, nitakaa ndani ya Bunge hadi kieleweke.
"Mimi ndiye kiongozi wa vyama vyote tisa hivyo nastahili kuheshimiwa, ninachopigania ni masilahi ya Taifa sikutumwa nitoke nje ya Bunge au kususia kikao," alisema Bw. Mrema.Baada ya kuchangia Muswada huo, alisimama Mbunge wa Same Mashariki, Bi. Anne Kilango Malecela ambaye aliitaka Serikali kusimama imara bila kuogopa vitisho vinavyotolewa na watu wasioitakia mema Tanzania.
Alisema kitendo kilichofanywa na wapinzani bungeni hakina nia njema ili kupata Katiba Mpya ambapo wabunge 156 waliopiga kura, wana vigezo vya kuchangia Muswada huo kujadiliwa.Wabunge hao walichangia Muswada huo kwa muda wa nusu saa ambao uliongezwa na baadaye, Bw. Ndugai aliahirisha Bunge hadi jioni ambapo wabunge waliotoka nje, hawakurudi bungeni wakati Muswada huo ukiendelea kujadiliwa.
Vurugu ndani ya Bunge hilo, ziliaza muda mrefu ambapo baadhi ya wabunge, walikuwa wakizingumza bila kufuata utaratibu hivyo Bw. Ndugai, alilazimika kusimama mara kwa mara ili kujeresha utulivu.
Sakata la mjadala huo lilianza juzi jioni baada ya wabunge wa CHADEMA na CUF, kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu kuwasilisha maoni ya kambi hiyo na kudai wananchi wa Zanzibar, hawajashirikishwa katika mchakato Rasmi ya Katiba Mpya.
Imeandaliwa na David John, Rehema Maigala na Mariamu Mziwanda

3 comments:

  1. Young parliamentarians are being childish, please mr speaker bear with them.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Who is Childish Young MPs or Depute speaker. you guy you must be specific.
      Is the speaker for ccm mp or all MPs.

      Delete
  2. Kwa kweli mhariri wa habari hii amachemka sana yaani kichwa cha habari hakifanani na maelezo yake please rekiebisheni hii post JK na Kagame wapi na Mbowe na Bunge

    ReplyDelete