Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), jana limetangaza kikosi cha wachezaji 32 wanaosafiri kwenda Lagos,
Nigeria wiki hii kushiriki mashindano ya kimataifa kwa vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars.
Ofisa Maendeleo
wa TFF, Salum Madadi amewataja wachezaji wanaounda timu ya wasichana kuwa ni
makipa Najihati Abbasi kutoka Mkoa wa kisoka wa Kinondoni na Niwale Halfan
(Temeke). Wengine ni Stumai Abdallah, Anastazia Anthony, Tatu Iddi (Kinondoni),
Vumilia Maharifa, Donisia Daniel, Maimuna Hamisi na Amina Ally (Ilala).
Aliwataja
wachezaji wengine kuwa ni Shelda Boniphace, Rehema Yahya na Anna Hebron
(Kinondoni), Khadija Hiza (Tanga), Neema Paul, Amina Ramadhani na Latifa Ahmed
(Temeke).
Wanaounda
kikosi cha wavulana ni Arafat Mussa (Ilala), Aziz Hashim (Ilala), Rothan Mkanwa
na Petro Mgaya (Morogoro), Bruno Shayo (Mwanza), Thomas Chideka (Temeke),
George Chota (Morogoro), Luseke Kiggi (Mwanza) na Ramadhani Kondo (Morogoro).
Wengine ni Martin Luseke (Mwanza),
Omary Hussein (Ilala), Joseph Mushi (Ilala), Miraj Kwangaya na Salum Issa
(Temeke), Optanus Lupekenya (Morogoro) na Athanas Mdam (Mwanza).
Mashindano hayo ya vijana ya kimataifa
yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu, baada ya yale ya uzinduzi kufanyika
jijini Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wavulana
pekee, ambayo hata hivyo ilitolewa katika hatua za awali huku timu ya Niger
ikitawazwa kuwa mabingwa.
Airtel imeanzisha mashindano hayo ya
vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia upatikanaji wa vijana wenye vipaji vya
soka, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya taifa.
Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa
vijana kudhihirisha uwezo wao kwa makocha wa taifa na kimataifa na kuweza
kujiendeleza zaidi kisoka.
Hivi sasa Airtel Rising Stars ni moja ya matukio muhimu ya
kisoka kwenye kalenda ya TFF. Huanzia katika hatua ya usajili ikifuatiwa na
mechi za mtoano, ili kupata wachezaji nyota wa kuunda timu za mikoa ambazo
huchuana katika ngazi ya taifa.
No comments:
Post a Comment