09 September 2013

FUSE ODG AITEKA DAR NA AZONTO
Na Zourha Malisa
MSANI I wa Gh a n a mwe n y e ma s k a n i nchini Uingereza, Fuse ODG, juzi amefanikiwa kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya shoo ya kihistoria, huku akipandisha mzuka kwa mashabiki waliohudhuria shoo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ustawi wa Jamii.

Fuse ODG, anayetamba na kibao cha Azonto pamoja na Antenna aliwateka mashabiki wake, baada ya kupanda jukwaani hapo na kucheza pamoja na mashabiki wa miondoko hiyo.Kwa kumuunga mkono msanii huyo, baadhi ya mashabiki waliohudhuria burudani hiyo, walipanda jukwaani hapo na kuanza kucheza naye pamoja na kumfundisha msanii huyo miondoko ya Kiduku, ambayo imezoeleka kuchezwa hapa nchini.
Msanii huyo alionekana kumudu kucheza kiduku, ambapo aliungana na baadhi ya mashabiki wake waliopanda jukwaani hapo.
Shoo hiyo imeonesha kufanikiwa kwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi, ambapo baadhi ya wasanii walitumbuiza huku msanii Hamis Ramadhan 'H Baba' alionesha mashabiki wake kuwa yeye ndiye mkali wa miondoko ya Bongo Bolingo Fleva.
Shoo hiyo ambayo iliandaliwa na kituo cha redio cha Times FM, pia ilinogeshwa na baadhi ya wasanii akiwemo Banana Zoro, kundi la Tip Top Connection likiongozwa na Madee pamoja na Tundaman, ambapo walipanda jukwaani hapo pamoja na msanii wa hip hop Chid Benz.

No comments:

Post a Comment