19 September 2013

SAKATA LA WAHAMIAJI HARAMU: SITTA AWATETEA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana kuhusu kutengwa kwa Tanzania katika nchi za Afrika
Mashariki pamoja na ‘Operesheni Kimbunga’ inayoendelea hapa nchini. Kulia ni Katibu mkuu wa
wizara hiyo Joyce Mapunjo.


  • APINGA VIKALI UTARATIBU UNAOTUMIKA KUWAONDOA
  • ASEMA UNAKIUKA HAKI ZA BINADAMU, UTAWALA BORA
  • AHOJI KWA MIAKA YOTE SERIKALI ILIKUWA WAPI

 Salim Nyomolelo na Anneth Kagenda

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekosoa utaratibu unaotumika kuwaondoa wahamiaji haramu nchini kupitia Operesheni Kimbunga, akisema ni kinyume cha haki za binadamu.Waziri Sitta amekuwa kiongozi wa kwanza nchini kukosoa utaratibu unaotumika kuondoa wahamiaji hao tangu Rais Jakaya Kikwete, aagize wawe wameondoka nchini ndani ya siku 14, vinginevyo wataondolewa kwa nguvu. Rais Kikwete alitoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Sitta aliwataka wakuu wa mikoa, wilaya, jeshi la polisi na uhamiaji kuwapa muda wa kutosha wahamiaji hao ili waweze kujiandaa kuondoka na mali zao ambazo walichuma kwa muda mrefu walioishi nchini kuliko kuwaswagaswaga.

"Haifai kwa hawa ndugu zetu ambao tumeishi nao kwa muda mrefu leo hii wanaswagwaswagwa jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu pamoja na utawala bora," alisema na kuongeza;"Je, Watanzania waliopo nje ya nchi wakiondolewa kwa nguvu kama hawa wenzetu wanavyofanyiwa tutafurahi?" Alisema kwa jambo hili Tanzania isionekane ina nongwa na nchi fulani kwani hata Rais Kikwete, wakati anatoa agizo hilo hakusema utaratibu huo utumike.

Alitoa mfano kuwa kuna mwanamke ambaye amefukuzwa nchini ambaye ni raia wa Rwanda akisema aliishi kwa zaidi ya miaka 30 nchini Tanzania na mtoto wake amesomea nchini na kuajiriwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)."Mtu kama huyu hakutendewa haki...mtu unamfukuza anaondoka na begi lake moja wakati ana mali zake nyingi...huyo ni lazima arudishwe ili ahakiki mali zake," alisema.

Alisema walioondolewa na kuacha mali zao nyingi pamoja na watoto watarudishwa nchini kufanyiwa uhakiki kama inavyofanyika kwa raia wa Malawi. Alishauri wahamiaji hao watakaorudi kufuata mali zao wapewe makazi ya muda na mali zao zisiporwe kwani watu hao hawakuwa majambazi.

"Kama umemuacha mtu ameishi nchini kwako kwa muda wa miaka 30 halafu leo unamfukuza kwa kumswagaswaga nani mwenye kosa? Na muda wote ulikuwa wapi?" Alihoji Sitta na kusisitiza kuwa; "Ndiyo maana tunasema aondolewe kwa utaratibu."Aliongeza kuwa miongoni mwa wahamiaji haramu waliofukuzwa baadhi yao waliwahi kuwa viongozi wa Serikali za vijiji na mitaa katika maeneo waliyokutwa wakiishi.

Waziri Sitta alisema tayari amepokea barua kutoka nchi za Burundi na Rwanda zikilalamikia utaratibu unaotumika kuwaondoa wahamiaji haramu hao."Oktoba 1 mimi na Waziri wa Mambo ya Ndani tutakuwa mpakani mwa Burundi na Rwanda ili kuangalia jinsi operesheni hiyo inavyotekelezwa na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hizo ili Tanzania isionekane ina malengo mabaya," alisema Sitta.

Alisema endapo utaratibu unaotumika wa kuwaondoa ukiendelea maadui wa Tanzania wataona njia hiyo inalenga kuwakomoa, jambo ambalo si la kweli.

18 comments:

  1. usingetaja tarehe...ungeibuka tu pale border

    ReplyDelete
  2. We Sitta unakumbuka shuka wakati kumekucha? Operation inaishia, waliodhuliwa wameshadhulumiwa, hamna kitu hapo. Ila vilio vya wale watu walioacha watoto wao, walioibiwa mali, walionyanyapaliwa kwa kuitwa wahamiaji haramu, walioibiwa mifugo, vitamrudi JK, nyie ngojeni tu. Kiongozi hawezi kufanya mambo hama haya!

    ReplyDelete
  3. kwa nini mnafanya mambo kama vile mpo kwenye majaribio? hivi kweli hamuoni kama mnawasababishia usumbufu kuwaondoa na kuwarudisha tena kufuatilia mali zao...mi naona mnafanya maigizo tu. acheni siasa mnatakiwa kuwa na maamuzi ya msingi!Nyie kama viongozi mlitakiwa kuliona hili jambo mapema sio kusubiri litokee ndo muanze kuchukua hatua.

    ReplyDelete
  4. laana ya ubaguzi lazima itawatafuna tu watanzania mkisha maliza kuwaondoa wote mtaanza kuondoana wenyewe kwa wenyewe.nawahangaa viongozi wa dini hasa christians especially walokore mko wapi yesu ni kielelezo cha ukimbizi wakati alipokuwa misri leo mnawaita watu waamiaji HARAMU? nchi hii siku moja itakuwa kama MJI WA NINAWI.maana watu hawana hofu na MUNGU.mnaswaga binadamu kama ngombe?YESU HATUSAIDIE HAWA VIONGOZI WENYE MAPEPO WASHINDWE KWA JINA LA YESU.

    ReplyDelete
  5. Katika hili tumeongeza maadui, kumbuka aliye acha mke, watoto na wajukuu hawezi kuisemea vizuri Tanzania, kutenganisha familia ni jambo lisilosaulika vichwani mwa wahanga. Katika kipindi cha medani ya siasa na uchumi cha star tv nilimsikia Makamba akisema kama mtu kaoa mtanzania na kupata watoto basi aondoke nao swali hao si watakuwa wahamiaji haramu watakokwenda?

    ReplyDelete
  6. tatizo letu tunakutupuka na bila kuangalia masuala ya haki za binadamu, mi naamini kikwete hakusema hatua zikichukuliwe kama wanavyofanya sasa, bali ni uoga unaowafanya wafanye vitu visivyofaa ili kuonyesha wanafanya kazi mbele ya boss wao (kikwete)

    mi naona ingefanyika busara kama maji yalishamwagika kinachobaki ni kuendana na hali husika na kuangalia utaratibu wa kufanya ulio sahihi kwa kila upande. kwa akili yangu finyu mi naona kitendo hiki ni lipizo la kupishana lugha kati ya viongozi wetu wawili wa nchi. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA ....... amin

    ReplyDelete
  7. Sitta siku zote ni mnafiki. Mbona tangu ujana wake alikuwa kwenye serikali hiyo hiyo anayoilaumu au kwa vile mkewe ana jina la Kizambia?

    ReplyDelete
  8. Nikweri wanafanyiwa wahamiaji haramu siyo ya kibinadamu,tumepata taarifa nyingi kuhusu hilo,rais alitoa agizo hili kwa nia nzuri,ila amewakabidhi swala hili watu ambao siyo makini,kwa hiyo tunasubiri rais naye atoe tamko,baada ya kuwa sitta ameliona hilo.na inabidi watanzania tumpongeze kwani amekuwa wa kwanza kuona haki za binadamu zinakiukwa.

    ReplyDelete
  9. Hao wahamiaji wengine walishakuwa kama watanzania na wameitumikia tanzania kama nchi yao wakihisi kwamba hakuna nchi yao tofauti na tanzania ila tu kukosa uraia na wengine wamekuwa nchini kabla ya uhuru na mwalimu alisema ambaye alikuwa nchini kabla ya uhuru ni raia wa tanzania ila yeye mwenyewe akatae sasa mbona tumeenda kinyume na agizo la mwalimu?ila la kusikitisha tumewafukuza kwa kuamrisha vitoto vidogo vya juzi juzi ambavyo havijui chochote na kupiga watu wazima vikongwe eti siyo wazawa hivi kama mtu ana ng'ombe 200atashindwa kuwa na uraia?lakini mpe furusa,naumuelimishe kwani wengi hawajui sheria.

    ReplyDelete
  10. Tunamuomba sasa rais mwenyewe atoe tamko baada sitta,na atangaze adhabu kali kwa wale viongozi walishiriki ktk zoezi hili,na wakakeuka haki za binadamu na wamechafua haiba ya tanzania,kwani nchi yetu ilikuwa inasifika kama mama mwenye huruma.na watu wakiipenda tanzania kwa ukarimu wetu .tumefanya wema kwa miaka mingi na kupata sifa kemukemu mtanzania alikuwa anatukuzwa kila mahala na sasa je niambie ukienda burundi itatukuzwa tena?rwanda uganda hata kenya.ndiyo tulifanya ubinadamu wa kuwapokea lakini tumeharibu zile thawabu na fadhila,kwa kuwafukuza kinyama.kwani unaweza kutenda mema miaka mingi kisha ukayaharibu kwa mda mfupi.tukumbuke hata ibilis alifanya mazuri menyi lakini yaliporomoka kwa dakika moja.angalia tusijute badaye.

    ReplyDelete
  11. Mi naamini watanzania si wanyama kiasi hiki, Tanzania ni nchi ya watu wastaarabu na wanaomuenzi Nyerere kwa kauli yake ya Binadamu wote ni ndugu zangu na afrika ni moja. Kwamba mipaka ni ya wakoloni, hukurupuki na kuanza kufanya safishasafisha ya wahamiaji kwa kuwapa wiki mbili. Yaani wiki mbili inatosha kwa wao kufilisi (wind up) maisha yao ya miaka 50 Tanzania? Legacy ya Kikwete itakuwa mbaya, akizeeka itamrudia, akistaafu hataalikwa popote kama mzee mwenye busara na utu.

    ReplyDelete
  12. Hivi mtu aliyefanya kazi hadi kastaafu ni mhamihaji au mtanzania?

    ReplyDelete
  13. Na uzalendo ndo huoo unatoweka TZ, mtoto kabaki bila mama na baba, atakuwa mzalendo kweli? Lakini wasomi wote ndani ya serikali na dola kwa ujumla wanashindwa kuona facts hizi na kushauri pale inapobidi? Ahsante Sitta, lakini kwanini usubiri hadi hapa wakati wakunyanyasika washanyanyasika? Jamani, Tanzania ilikuwa ndo kimbilio la wenye shida, Mungu katupa amani katufanya kimbilio. Ole wake anaeenda kwa akili yake mwenyewe, atadeal na hasira ya Mungu. Mgeni ana thamani kubwa sana, kama si mhalifu. Hekima inatakiwa sana kuliko hasira.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mimi pia namunga mkono sitta kwani mimi naishi nje baba na mamayangu wapo tz lakini sasa wameondoshwa na kudai eti ni wanyaru, pia wameporwa na wanasheria pesa eti wanawatetea hilo si halali kabisa niaibu kwa taifa letu

      Delete
    2. HALI ILIKUWA MBAYA KULE BIHARAMULO WATU WAMETUMIA CHUKI ZAO BINAFISI KUCHOMEA UTAMBI WATU BILA SABABU WATU WAMETOZWA PESA NYINGI MNO MIMI USHAIDI NINAO NAKAMA UNATAKA KUJUWA ZAIDI SIMU YANGU NI HII 0051-5373124 AU 0051-946888867 JAMAA YANGU WAMEKANUSHWA ETI SI WAZINZA NAKUPORWA MALI ZAO BAADHI YA WATU WAPO KWENYE HOSPITAL TEULE YA BIHARAMULO WAMELAZWA WAKO MAHUTUTI KWA VIPINGO NA BANDO WAMETISHIWA KUWAWA IWAPO WATATAMUKA LOLOTE KUHUSU HALI HIYO MIMI NINGEOMBA MFIKE HUKO MONE YANAYOTENDEKA NAFIKIRI HII SIYO TZ KWANI NI UNYAMA KABISA KABISA KAMA KWELI NI WAHAMIAJI HARAMU YANINI KUWAOMBA PESA? MIMI MPAKA SASA NAJARIBU KUTAFUTA NI JINSI GANI HAKI ITAPATIKANA KWANI WALE WOTE WALIOKAMATWA WAMEAAMBIWA ETI NI WAMEINGIA NCHI KINYUME CHA SHERIA SASA SHERIA NI IPI? SASA MBONA WAKILIPA PESA WANACHIWA SASA KISA AU MTU LAZIMA ALIPIE NGARAMA YA MAISHA? HII SIYO HALALI LAKINI TUKIFUATIA ZAIDI NI CHUKI ZA KISIASA TU KAMA NI UNGOVI WA CONGO SISI TUNAHUSIKANJE KAMA NI VITA YA CONGO TANGU NIMEZALIWA CONGO DAIMA IMEKUWA NI VITA TU SASA MWESHIMIWA JAKAYA MURISHO KIKWETE KAMA ANATAKA KUITETEA CONGO BASI WASIMAMISHE WAFARANSA KWANI NDO WANATIA SHIDA CONGO.WATU WENGI WAMEPOTEZA MAISHA MKOANI KAGERA JARIBUNI KUWA WENYE HAKI SI KUTAWALIWA NA UNYAMA KAMA WANASEMA ETI NI MAJAMBAZI HAO WATU WAMEISHI ZAIDI YA MIAKA AROBAINI KWETU HAKUKUWA SHIDA LA UJAMBAZI SASA IWEVIPI? AU MNATAKA KUSEMA WALE WANAOCHO MAKANISA KULE ARUSHA NI WAHAMIAJI HARAMU AU WANAOWAMWANGIA WATU TINDIKALI SI WATANZANIA? TUWE MAKINI TUSIWAHISIE WATU BILA UHAKIKA SASA UJAMBAZI MBONA UPO KOTE TANZANIA HADI KULE ZANZIMBAR SASA NA HUKO NI MKAPANI? AU KUNAAJENDA YA SIRI KUTOKA SERIKARI YA KIKWETE, LAKINI MUNGU NIMWENYE HAKI TUTAONA MWISHO WAKE SASA NA MELI ZILIZOPEPERUSHA BENDELA YA TANZANIA ZILIKUWA ZA WANYARWANDA AU ZILIKUWA WAHAMIAJI HARAUMU AU NI ZAWATU WA UNGANDA? HILO NALO TUJIHOJI MIMI NAFIKIRI KUWA KUNAWATU WAMEJIFICHA NYUMA YA HILO. SIMU 0051-946888867 NIPINGIENIKUPE UKWELI AU KAMA UNATAKA WEKA NAMBA YAKO MIMI NITAKUPINGIA NA KUKUPA DATA ZOTE

      Delete
  14. SHAME ON SITTA; HAIJAWAHI KUTOKEA WAZIRI YEYOTE KUMKOSOA RAIS WAKE HADHARANI KAMA ANAVYOFANYA SITTA. KAMA HAKUBALIANI NA RAIS WAKE ALIPASHWA KUJIHUDHURU KWANZA ILI AWE HURU KUSEMA LOLOTE AKIWA NJE KAMA RAIA WENGINE WA KAWAIDA, AU NA YEYE ANA DAMU YA WAHAMIAJI HARAMU??. HIVI HUYU SITTA SI ALIAPA KUWA MSAIDIZI WA RAIS? SASA HAPA ANAMSAIDIA RAIS AU ANAMUAIBISHA NA KUMDHARIRISHA! IWAPO YEYE ATAKUWA RAIS SI CABINET YAKE ITAKUWA NYUMBA YA KAMBARE, HATA NIDHAMU HAKUNA!

    ReplyDelete
  15. Sitta hajafanya makosa kumkosoa raisi. Tena kama raisi angekuwa na anafikiri angejiuzuru. Mkoani Kigoma, watu wameshikwa wakiwa na kadi za kupigia kura, na wameambiwa si watanzania. Hii ni dhahili kuwa viongozi waliochaguliwa hawakuchaguliwa kiharali.
    Sitta endelea kutoa maovu ya huyo mlopokaji asiyefikiria kwanza kabla ya kusema

    ReplyDelete
  16. SASA TAZAMENI JANGA JINGINE ASIKARI WETU KAUWAWA KULE CONGO NI HALALI?MIMINAFIKIRI WACONGO NAO WATUMIE BUSARA ZAO KUPATANA NA WAASI KWANI IKIWA WATABAKI KWENYE MAKOTI YA WANZUNGU MABO YATAEDELEA KUWA MABAYA KABISA, KWANI YOTE YANATOKANA WAFARANSA SASA WAKAE CHINI WAJUWI KUWA WAO NI WAAFRICA WAACHANE NAHIZO TABAKA WANAZOLETA WAFANSA NCHI KWAO SASA NANI ARAUMIWE KIFO HICHO? KWELI IMEKUWA MARA YA KWANZA KUONA NAKUSIKIA KUWA WAHAMIAJI HARAMU WAMEFUKUZWA KWA MAPANGA NA MITUTU HIYO KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU KABISA UJUWE KIKUBWA HAO MABWANA WAMEEDA HUKO BIMULO KUJISOMBEA MAPESA NA KISHA KURUDI DAR NAKAMA TUNAWAHUKUMU WATU KUWA HARAMU SI TUTUMIE SHERIA MIMI NIMEKUWA HUKU UHISPANIA MIAKA ZAIDI YA KUMI BILA VIBARI LAKINI MPAKA HAPO NILIPOWEZA KULEKEBISHA MIS DOCUMENTOS NA SASA NAFANYA KAZI HUKU BILA SHIDA KAMA MWISPAƑOL MIMI NINAWASIWASI KUWA SASA TZ IMEKUWA NAITIKADI ZA KISASUSI KABISA KWANI HAIKUWA HIVYO TANGU ZAMANI LEO HII NIPOONGEA KUNA WATZ WENGI TU NCHI PERU TENA WASIOKUWA NA VITABURISHO WALIFIKA KAMA NARCOTRAFICANTE WAUZA MADAWA YA KULEVYA WAMEKUWA MAGREZANI MIAKA NA MIAKA LEO WAKO HURU WAMEBAKI HAPA, BILA KUBUNGUZIWA, LEO TZ TUNATUKANA WATU KUWAITA HARAMU COMO HARAMU IPURO? ASI ES MIMI NAONGOPA SANA UNAJUWA NIKWAMBA MAASKARI WAMEJIPATIA PESA KWAHAO WANAODAIWA KUWA HARAMU LAKINI YOTE HAYO ITAKUWA RAANA YA RAIS, NASIKITIKA KWAMBA SASA AMEIPAKA MATOPE TZ MIMI HAPA NILIPO WATU WENGI WANANIULIZA KUWA TZ HAKUNA HAKI ZA BINADAMU SINALA KUSEMA. IMEKUWA AIBU SANA KWA MATAIFA MENGINE KUONA WATU WAPINGWA NAHATA KUWAWA NITISHIO KABISA. ILA BASI TUMUOMBE MUNGU ABADILISHE MIOYO YETU

    ReplyDelete