Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam
leo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya wafuasi 52 wa Shekhe Ponda Issa Ponda,
waliokata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela, waliyohukumiwa
na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, anaripoti Rachel Balama.
Katika rufaa yao hiyo, wafungwa hao,
kupitia kwa wakili wao, Mohamed Tibanyendela, wanapinga hukumu ya Mahakama ya
Kisutu, ambapo pamoja na mambo mengine, wanadai kuwa hakimu alikosea kisheria
kuchambua ushahidi wa pande zote uliowasilishwa mahakamani hapo.
Pia wanadai kuwa katika hukumu hiyo,
hakimu alijikanganya kwa kumwachia huru mmoja wa washtakiwa na kuwatia hatiani
washtakiwa wengine.Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa leo na
Jaji Salvatory Bongole.
Machi, mwaka huu, Hakimu Sundi Fimbo wa
Mahakama ya Kisutu aliwahukumu washtakiwa hao wa kesi ya kula njama na kufanya
maandamano isivyo halali kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia
katika makosa yaliyokuwa yakiwakabili.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa
hayo Februari 15, mwaka huu.Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni
Salum Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein
Athumani, Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid,
Jumanne Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji
Sheluhenda, Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili na Awadh Juma.
Wengine ni Omari Mkwau, Kassim Chobo,
Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum,
Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta na Bakari Athumani,
Mbwana Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma.
Wengine ni Omari Mkandi, Idrisa
Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Mussa Sinde, Issa Sobo,
Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman
Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu
Rashid wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya
tukio, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja
walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali.Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na
eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo
la kusababisha uvunjifu wa amani.
Shtaka la tatu ilidaiwa kuwa washtakiwa
wote kwa pamoja walikiuka amri ya Jeshi la Polisi ya kutoa zuio la kufanya
maandamano, n a k u f a n y a mk u s a n y i k o uliosababisha vurugu na
uvunjifu wa amani.Katika shtaka la
nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi
kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.
No comments:
Post a Comment