09 September 2013

NJAA YASABABISHA WAKULIMA KULA MBEGUNa Jovither Kaijage, Ukerewe
TATIZO la njaa katika Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza limechukua sura mpya baada ya kuwepo taarifa za wakulima kula mbegu wanazopewa na halmashauri ya wilaya hiyo.Suala hilo limeibuliwa mwi s h o n i mwa wi k i katika kikao cha wadau wa maendeleo wa wilaya hiyo kilichojadili tatizo la njaa kwa muda mrefu.Ki k a o k i l i a n d a l iwa na mtandao wa asasi za kiraia wilayani Ukerewe ( U N G O N E T ) k w a kushirikiana na Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Mwanza (MPI) kwa kufadhiliwa na Shirika la Forum Syd .

Ofisa Kilimo wa Kata ya Namagondo, Kemimba Itogoza, alisema ni suala la kusikitisha kuona mkulima anafikia hatua ya kula mbegu alizopewa kupanda kwa sababu ya kukosa chakula.Akithibitisha kauli yake alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka juzi kata yake, ilipokea na kugawa kwa wakulima 100 kilo 250 za mbegu ya mtama, lakini zilizopandwa ni kilo 20 pekee huku nyingine zikisagwa na kuliwa na wakulima.
Alisema katika uchunguzi wake alibaini kuwa tatizo kubwa la upungufu wa chakula katika kata hiyo ndiyo sababu kubwa ya wakulima hao kula mbegu hizo na kuongeza kuwa inahitajika juhudi kubwa za kukabili tatizo hilo.
Na y e Al l y Ms umo , akichangia hoja hiyo alisema pengine tatizo hilo la wakulima kula mbegu linasababishwa na uamuzi wa ngazi za juu kufanyika bila kuishirikisha jamii husika ambayo wakati mwingine mbegu hizo hazikuwa na mahitaji muhimu kwao.Ofisa mazao wa wilaya hiyo, William Balyahele mbali ya kubainisha kuwepo upungufu wa tani tisa za chakula msimu huu wa kilimo, pia ametaka idara hiyo ipewe nguvu za kisheria katika kusimamia shughuli zake.
Alisema wilaya hiyo ina eneo la ardhi ya kilimo ya hekta 33,765.5, ambazo zikitumika kwa kilimo cha kitaalamu zinaweza kuzalisha kilo milioni 2 za mahindi kwa msimu mmoja wa kilimo huku mahitaji ya chakula kwa mwaka yakiwa kilo milioni 1.5. za nafaka.Akifafanua aliwataka wajumbe waeleze kama wako tayari kurejea katika kilimo cha shuruti na kuchapwa mijeledi kama ilivyokuwa enzi za ukoloni.

No comments:

Post a Comment