Na
Mwandishi Wetu
UO N G O Z I w a Mamlaka ya Ukanda M a a
l u m u w a Uwekezaji (EPZA) ume s ema u t a e n d e l e a kutekeleza mpango wa
Serikali wa maendeleo wa miaka mitano kwa kuhakikisha inaendelea kuweka
mazingira ya kuvutia wawekezaji katika sekta ya viwanda ili kuharakisha
shughuli za maendeleo nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm
Meru, alibainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam hivi karibuni, ambapo alifafanua maendeleo ya miradi na uwekezaji katika
ukanda huo kwa miaka sita iliyopita.Alisema EPZA inaweka nguvu kubwa kwenye
maendeleo ya viwanda kwa kuwa sekta hiyo ni msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi
yoyote duniani na kwamba Tanzania
haiwezi kuachwa nyuma kwa hilo kama
kweli inataka kupata maendeleo endelevu.
"Historia ni shahidi kuwa viwanda
ndiyo moja ya misingi muhimu ya maendeleo," alisema na kuongeza kuwa ndiyo
maana taasisi yake inafanya kila linalowezekana kuhakikisha sekta hiyo inakua
hapa nchini.
"Taasisi hii inatekeleza kwa
vitendo mpango huo wa maendeleo na tumedhamiria kuongeza nguvu zaidi,"
alisema.A l i s e m a m o j a y a vipaumbele
vya mpango wa maendeleo wa miaka mitano ni maendeleo ya viwanda na kuwa EPZA
inataka kuhakikisha kuwa hilo linafanikiwa kwa faida ya nchi nzima.
"Tunaunga mkono mpango wa
maendeleo wa miaka mitano, tumedhamiria kufanikiwa katika hili," alisema.
Alisema kuwa kuimarika kwa sekta ya viwanda nchini kutasaidia kuzalisha ajira
mpya, upatikanaji wa teknolojia mpya na kuongeza kipato cha nchi hivyo kukuza
uchumi na ustawi wa jamii.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa sekta
ya viwanda katika kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa nchi, taasisi yake
imejikita kuvutia wawekezaji wa ndani na nje katika sekta hiyo ili kunufaika na
fursa hizo.
Awali, alisema kuwa mpaka sasa wastani wa
viwanda vilivyowekeza kupitia
No comments:
Post a Comment