Na Mwandishi Wetu
KA M P U N I y a mitandao ya simu za
mkononi nchini, Airtel imetajwa kuwa moja kati ya kampuni ambazo zimekuwa
zishirikiana na Serikali kwa dhati katika harakati za kupambana na tatizo la
ajali za barabarani.Kauli hiyo
ilitolewa na Kamanda wa Kikosi cha Us alama Barabarani, Mohamed Mpinga, wakati
akieleza juhudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na kampuni hiyo.
Alisema Airtel
imeweza kutoa mchango mkubwa wa kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa
kiasi kikubwa."Airtel ni
wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani, kwa miaka mitano mfululizo na
hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini wa wiki ya nenda kwa usalama
barabarani.
"Airtel
pia imedhamini vipindi vya elimu ya usalama barabarani katika televisheni na
redio, pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na Jeshi la Polisi usalama
barabarani imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu = Kifo
inayowaonya waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati wakiendesha magari,"
alisema Mpinga.
Alisema mwaka jana Airtel ilidhamini
mashindano ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (bodaboda) yaliyokuwa na
lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel- Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akizungumza juu ya suala hilo
alisema "Airtel imeamua kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha
inatokomeza kabisa wimbi la ajali za barabarani.
Alisema idadi ya vifo vinavyotokea
barabarani ni kubwa mno na ndiyo maana Airtel imeamua kujikita katika kuokoa
maisha ya wateja wake na Watanzania kwa ujuma.Alisema Airtel itaendelea kushirikiana
na Jeshi la Polisi usalama barabarani kuhakikisha lengo la kupunguza ajali
linafanikiwa.
No comments:
Post a Comment