09 September 2013

NAPE ARUSHA KOMBORA KWA WAPINZANI



 Na Eliasa Ally, Kilolo
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uendezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amesema vyama vya upinzani nchini, vitaendelea kuwa na ndoto ya kushika dola kwani havina sifa hiyo zaidi kuvuruga amani na kufanya vurugu.Alisema CCM inalaani vurugu zilizofanywa na upinzani wiki iliyopita bungeni mjini Dodoma na kuwataka watambue dhamana waliyonayo katika Bunge hilo kwa masilahi ya nchi, wapigakura.

Bw. Nnauye aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Ruahambuyuni, Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, wakati akizindua mbio za bendera ya CCM inayokimbizwa mkoani humo na kuwaeleza wananchi utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Aliongeza kuwa, wabunge wa upinzani wamepewa dhamana na wananchi ili kutetea masilahi yao si kupigana ngumi katika Ukumbi wa Bunge na kumtaka Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kutafuta ukumbi wa kupigania.
"Kama Bw. Mbilinyi anajiamini kwa kuwa na uwezo wa kupigana, atafute ukumbi ili wananchi walipe kiingilio si kuharibu sifa ya Ukumbi wa Bunge, lazima atambue thamani aliyonayo kwa wananchi.
" H a t a Mw e n y e k i t i w a CHADEMA (Freeman Mbowe), atafute kazi nyingine ya kufanya kama ubunge umemshinda... wananchi mnapaswa kufanya maamuzi magumu katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwanyima kura wabunge wa upinzani ambao hawaendi bungeni kujadili masilahi yao," alisema.
Alisema vyama vya upinzani vimegeuka kuwa vibaraka wa wakoloni vikitumika kugombanisha wananchi, kuvuruga amani, umoja na mshikamano uliopo.
Bw. Nnauye alisema, CCM itaendelea kutawala nchi, kushika dola kwani hawapo tayari kuona Tanzania ikiongozwa na watu wasio na chembe ya uadilifu na chanzo cha vurugu ambazo zinachangia vifo kwa baadhi ya wananchi.
"CHADEMA wanapoanzisha vurugu, viongozi wao huwa hawapatwi na madhara yoyote, matokeo yake husababisha vijana wasio na hatia kupoteza maisha katika vurugu zao na wao hukimbia," alisema Bw. Nnauye.
Alisema upinzani wamefanikiwa kuchukua baadhi ya majimbo kwa sababu ya wana CCM wenyewe kwa wenyewe kutoelewana katika majimbo husika, hivyo aliwataka kuwa na mshikamano ili kutotoa nafasi kwa upinzani katika Uchaguzi Mkuu 2015.
"Viongozi wa CCM katika ngazi zote, wana haki ya kuwabana kikamilifu Wakuu wa Wilaya ili watoe taarifa za maendeleo yaliyofanywa na Serikali yao, akikataa tunamuomba aachie ngazi mwenyewe.
"Viongozi wazembe wasioweza kutekeleza Ilani ya CCM, kuendana na kasi tunayotaka, hatumhitaji kwani wanatuangusha na kutufanya tueleweke vibaya kwa wananchi," alisema.

4 comments:

  1. utampaje nchi mtu asie na uvumilivu? uongozi ni busara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga (anonymous Sept 9, 9:00AM). Unamchokoz mtu makusudi alafu unasema avumilie. Asiyevumilia ni nani kati ya mchokozi aliyechokozwa. Kwanini CCM hawapendi kuacha uchokozi wa waziwazi. Wao ni wavumilivu? Km ni wavumilivu waachie dola wapizani wachukue.

      Delete
    2. Hivi unafikiri hao jamaa zako wataachiwa dola ili wakapigane kwenye vikao vya baraza la mawaziri? Upinzani una tija ila kuuachia dola ni balaa. Ona walivyokaa kisharishari

      Delete
  2. Ndiyo wale wale yaani hekima na subira hawana kazi vurugu na matusi hata tone la hekima hakuna,ngoja tuvute subira sijui mwaka wa kushika dola itakuwa vipi!

    ReplyDelete